Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Vichekesho vya kukuondoa mawazo leo

Featured Image

Soma vichekesho hivi;

Mwizi wa atm

Jamaa aliibiwa kadi yake ya benk akaulizwa kama ameripoti polisi akajibu "sijaripoti bado, mwizi mwenyewe hamfikii matumizi kama mke wangu.

Cheka kidogo

Njia rahisi kusahau matatizo yako (japo kwa muda mfupi) vaa viatu vinavyokubana.

Mlizi mbio mbio

Tulikuwa bar moja jana mlinzi kaingia spidi, akamwambia jamaa mmoja aliyekaa kaunta, Mlinzi: Mzee gari lako limeibiwa Mzee: Umemtambua aliyeiba? Mlinzi: Hapana lakini nimeandika namba za gari hizi hapa.

13, 13…

Jamaa alikuwa anapita nje ya wodi ya vichaa akasikia mtu anasema, 13, 13, 13, 13, 13, 13,….. akaamua kuchungulia kwenye kitundu alichokiona ajue kuna nini, ile kuchungulia tu akamwagiwa mchanga wa machoni, sauti ikabadili ikaanza 14,14,14,14,14……

WATAALAM

Jamaa alikuwa anaumwa sana, mkewe akamwita daktari, alipofika akamkuta jamaa kafumba macho;
Dokta: Huyu mbona amekwisha kufa?
Jamaa: Sijafa bwana
Mke: Hebu nyamaza bwana acha kubishana na wataalamu.

Ya leo mgonjwa

Dokta alipotembelea wodi ya mgonjwa wake aliyepata ajali. Mgonjwa akiwa amening'inizwa mikono juu akauliza "dokta ntaweza kweli kupiga kinanda nkitoka hospitali?"
Dokta: Bila shaka utaweza, wewe ni mpiga kinanda mzuri enh?
Mgonjwa: Hapana sijawahi kabisa bado.

4WD

Mwanaume alimnunulia pete ya almasi mkewe, rafiki akauliza "si ulisema anapenda gari yenye four wheel drive, mbona umenunua pete?" Mume akajibu "unadhani wapi ntapata rav4 feki?"

Ajali ilivyotokea

Trafiki polisi akihoji palipotokea ajali "ahaa! Sasa naanza elewa embu nielezee jinsi ajali ilivyotokea wewe ukiwa kama dereva mhusika." Dereva akajibu "hata sikumbuki nlifumba macho"

Faini ya kukojoa

Polisi alimdaka jamaa anakojoa pembezoni mwa ukuta.
Polisi: Wewe unajua panakatazwa kukojoa hapa?
Jamaa: Sasa nimebanwa nifanyaje?
Polisi: Faini yake elfu tano.
Jamaa akatoa noti ya elfu 10.
Polisi: Sasa chenji tunaipataje?
Jamaa: Tafuta chenji unipe changu.
Polisi: Basi kojoa tena…

Mume anaenda kazini

Jamaa kaamka asubuhi sana Jumamosi, mvua inanyesha kang'ang'ania kuwa anaenda ofisini. Kawasha gari yake, kufika njiani hali ilikuwa mbaya kaamua kurudi. Kafika home kavua nguo kaingia tena kitandani, kamnong'oneza mkewe aliyekuwa usingizini; "Yaani hali ya hewa huko nje mbaya sana" Mke: Si ndio nimemshangaa huyu mpumbavu eti kaenda kazini…

Hasira za mtoto

Baba na mtoto:
Baba: Mwanangu ukiwa na hasira unafanya nini?
Mtoto: Naenda chooni.
Baba: Chooni? Kufanya nini?
Mtoto: Kusafisha.
Baba: Halafu ndio hasira zinaisha?
Mtoto: Ndio. Nasafisha choo kwa mswaki wako.

Mgonjwa na Dokta

Mgonjwa: Dokta nimekuja nahisi ninaumwa Malaria na kifua.
Dokta: Sasa ushajua unaumwa nini hapa umefuata nini kwangu?
Mgonjwa: Sasa si nimekuja kwa dokta.
Dokta: Wanaojua kuwa wanaumwa kama wewe wanapitiliza maabara.

Pilau la bachela

Bachela mmoja aliyekua akiishi kwa muda mrefu peke yake kwenye nyumba aliyopanga siku moja alitaka kupika pilau kwa mara ya kwanza. Sasa asijue nini kinachobadilisha rangi ya wali kuwa rangi ya brown, yeye akapika kama kawaida (wali) kisha wakati wa kula akavaa miwani yenye rangi ambayo ukiuangalia wali unauona kama pilau wakati anakula.

Mwizi na chizi

Mwizi kaiba TV na kuanza kukimbia nayo, kumbe ile nyumba mlikuwa na chizi, akaanza kumkimbiza yule mwizi. Kila mwizi akiongeza mbio chizi nae huyo, mwishowe mwizi akasalimu amri na kusimama, yule chizi akamsogelea na kumwambia.. Daah umesahau remote hii hapa mwizi kafleti.

Chemsha bongo

Baba akimuuliza chemsha bongo mwanae anayesoma shule ya chekechea "haya niambie kitu gani hakiwezi kuliwa wakati wa breakfast?" Mtoto akajibu "hiyo mbona rahisi baba, si lunch na dinner"

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

Henry Mollel (Guest) on September 23, 2015

Hii imenikuna hadi nina furaha! πŸ˜ŠπŸ˜‚

Diana Mallya (Guest) on August 24, 2015

Hii ni ya maana sana! πŸ˜‚πŸ‘Œ

Richard Mulwa (Guest) on August 22, 2015

πŸ˜„ Kali sana!

Patrick Akech (Guest) on August 21, 2015

πŸ˜† Hii imenigonga kweli!

Rahma (Guest) on July 25, 2015

πŸ˜‚ Hii ni ya kuhifadhi!

Anna Mchome (Guest) on July 14, 2015

Hii ni joke ya ukweli kabisa! πŸ˜‚πŸ€£

Philip Nyaga (Guest) on July 10, 2015

Ucheshi wa hali ya juu! πŸ˜‚πŸ‘

Edith Cherotich (Guest) on July 2, 2015

πŸ˜† Kali sana!

Hamida (Guest) on June 28, 2015

Haha, hii ni ya kuhifadhi! πŸ“Œ

Jane Muthui (Guest) on June 12, 2015

πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜†

Mary Njeri (Guest) on June 4, 2015

Nimecheka hadi nimesahau shida zangu! πŸ˜…πŸ˜Š

Lydia Mzindakaya (Guest) on June 2, 2015

πŸ˜‚ Nitaiiba hii bila shaka!

Henry Sokoine (Guest) on May 23, 2015

πŸ˜‚πŸ˜‚

Hellen Nduta (Guest) on May 9, 2015

😁 Hii ni dhahabu!

Rose Kiwanga (Guest) on April 28, 2015

Hii imenifurahisha hadi ninacheka kwa sauti! πŸ˜„πŸ˜…

George Mallya (Guest) on April 27, 2015

Hii imenibamba sana! πŸ˜…πŸ€£

Rabia (Guest) on April 4, 2015

πŸ˜… Nilihitaji kicheko hicho!

Related Posts

Wanawake hii nayo ni romantic ?πŸ’ž

Wanawake hii nayo ni romantic ?πŸ’ž

Alaf wale Madem wanaowavua maboy wao KOFIA alaf wanakimbia nayo thinking its FUNNY and R... Read More

Kilichompata huyu jamaa akiwa anaangalia mpira mechi kali na mke wake

Kilichompata huyu jamaa akiwa anaangalia mpira mechi kali na mke wake

WIFE: Baibie, yule ni nani? Ni Chris Brown??
HUSBAND: Yule ni Theo Walco... Read More

Angalia kilichomkuta huyu msanii wa mziki na mashabiki wake

Angalia kilichomkuta huyu msanii wa mziki na mashabiki wake

Msanii mmoja anaitwa ''KINYA'' alikuwa ana perfom jukwaan..!!!
Kawaida kila msanii lazima aj... Read More

Soma alichojibiwa huyu mzee baada ya kudai kutaka kumsikiliza Nyerere

Soma alichojibiwa huyu mzee baada ya kudai kutaka kumsikiliza Nyerere

Mzee: Dereva ongeza sauti tumsikilize Mwalimu Nyerere!!

Dereva: ungemsikiliza mwalimu wa... Read More

Acha usumbufu…

Acha usumbufu…

UNAMNG'ANG'ANIZA MPENZI WAKO AKUWEKE KWNY PROFILE PICHA MLOPIGA PAMOJA

HIVI ULIDHANI MWL.NY... Read More

Baada ya kuumizwa kimapenzi haya ndiyo maneno

Baada ya kuumizwa kimapenzi haya ndiyo maneno

Mkishaumizwa ndo utasikia, Moyo sukuma damu sio mengine. wakati mnapenda mlizani moyo ul... Read More

Huu ndio Umuhimu wa English katika mapenzi

Huu ndio Umuhimu wa English katika mapenzi

HUU NDO UMUHIMU WA ENGLISH KATIKA MAPENZI

jaribu kumwita mpenzi wako "my sweet potato" a... Read More

Nani Mkali Hapa kati ya DEMU na MSHIKAJI?

Nani Mkali Hapa kati ya DEMU na MSHIKAJI?

"MAENEO FLANI ya KISHUA"

-Mshikaji kamwona demu mkali
anakatiza kitaa akamkubali akaam... Read More

Hakuna siku mbaya maishani kama hii

Hakuna siku mbaya maishani kama hii

Hakuna siku mbaya maishan kuona mtu uliyesoma naye darasa moja, anakupita na private car,, afu w... Read More

Huu ndio uhondo na raha ya kupanda daladala wajameni

Huu ndio uhondo na raha ya kupanda daladala wajameni

Wasiopanda dalaladala wanakosa uhondo wa kauli hizi
1. nitakupa
2. Atapewa mbele
3... Read More

Nilichokifanya leo

Nilichokifanya leo

Leo nmemlipa konda nauli, akasahau kunishusha kituoni. Na mimi nkakaa KIMYAAA kumkomoa…..

... Read More
Huyu mtoto kaongea point kweli, angalia anachomwambia baba yake

Huyu mtoto kaongea point kweli, angalia anachomwambia baba yake

Mtoto alimwuuliza baba yake,
Mtoto: Baba unaweza kumwachia hilo gari lako house boy/girl aka... Read More