Kilichotokea baada ya mzungu na mbongo kukaa siti moja, bongo wasanii wengi
Mzungu akamdharau sana Mbongo nakujiona anajua kila kitu duniani!,
Akamwambia Mbongo waulizane maswali na Mbongo akishindwa anatoa sh.500 na endapo yeye atashindwa atatoa 100,000/=.
Mzungu akauliza ni nchi ipi ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya Dunia?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hajui.
Updated at: 2024-05-25 18:06:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mzungu akamdharau sana Mbongo nakujiona anajua kila kitu duniani!,
Akamwambia Mbongo waulizane maswali na Mbongo akishindwa anatoa sh.500 na endapo yeye atashindwa atatoa 100,000/=.
Mzungu akauliza ni nchi ipi ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya Dunia?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hajui.
Na yeye akamuuliza Mzungu ni kitu gani kikienda juu kina miguu minne na kikirudi chini kina miguu mitatu?
Mzungu akafikiria akakosa jibu akatoa 100,000/= kuashiria hajui ila akataka kujua, akauliza ni nini hicho?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hata yeye hajui!.
SHARE na marafiki kama umemkubali Mbongo kwa ujanja. Lakini unafikiri Mbongo huyu kwa akili hizi atakuwa ametokea mkoa gani!?.
Updated at: 2024-05-25 18:10:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kakubaliana vizuri na msichana fulani hivi kuwa aibuke gheto, mchizi kajipanga vizuri kabisa…. mara saa nne hivi mdada kasema hana nauli. Mshkaji kajikunja kamtumia Elfu tano maana mwenye shida alikuwa ni yeye…… Baada ya nusu saa yule dada akamtumia meseji. "Jamani mpenzi, kumbe baba hatoki nilijua atatoka… sorry bae sitaweza kuja kwa leo… sooo sorry!" Mshkaji jiii! hajajibu kitu…..
Baada ya muda kidogo meseji ikaingia katika simu ya binti, akajua mchizi kajibu. Mh! kutazama ni meseji kutoka Mpesa.
"CA90F0511 IMETHIBITISHWA Tshs 5000 ILIYOTUMWA KIMAKOSA KATIKA ACCOUNT YAKO IMETOLEWA SALIO LAKO NI Tshs 5"
Halafu ndo ikaingia meseji ya mshkaji. "BASI POA SIKU NYINGINE KAMA VIPI"
#dada wa watu mashavu yakamshuka… hakuamini kilichotokea…. yaani jamaa keshawapigia Voda na pesa fasta imezuiliwa……
Alichokifanya jamaa baada ya kuokota wallet yenye pesa za kumwaga
Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station
"Naitwa John nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki 7, ATM Card na kikaratasi chenye PIN ya ATM Card na kijimkufu cha dhahabu kinene hivi…"
Updated at: 2024-05-25 18:04:09 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station
"Naitwa John nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki 7, ATM Card na kikaratasi chenye PIN ya ATM Card na kijimkufu cha dhahabu kinene hivi…"
Mtangazaji akasema:- Akhasante sana John, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama ana kusikiliza akutafute kwa No. Gani!?
John: Hapana, mi nilikuwa namshukuru tu maana amenitoa kwenye matatizo na ninapenda kumuombea Dedication wimbo wa Snura "MAJANGA" umfikie popote pale alipo…!!!
Eti ni kweli hii ni sababu wanaume wana Upendo Sana?
Updated at: 2024-05-25 16:52:50 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wanaume wana upendo kwa kweli.
Mwanaume hata akipewa kundi la wanawake 90 achague mmoja!! Hata akichagua mzuri kupita wote bado roho itamuuma kuwaacha wale 89 waliobaki!!* Kwa namna hii wanaume wana Upendo Sana 😂😂😂😂😂😂
Updated at: 2024-05-25 17:09:54 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa: Mambo honey, upo ok? Mrembo: Sipo ok my dear Jamaa: Una tatizo gani baby? Mrembo: Nimetoka hospitali kupima, nna mimba. Jamaa: Weeh usiniletee balaa hiyo mimba imeingiaje wakati huwa tunatumia kinga? Mrembo Kwani nani kakwambia mimba ni yako, hebu tuliza mshono huo.