Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Vyakula vinavyofaa kuliwa katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Featured Image

Vyakula vinavyofaa kuliwa wakati huu wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni vingi, leo tutaanza kuchambua kimoja baada ya kingine, Mbali na Waislamu, uchambuzi huu unawafaa pia wale ambao siyo Waislamu. Chakula kilichozoeleka zaidi kwa futari ni tende. Baada ya kushinda kutwa nzima na Swaumu, kiwango cha sukari ya mwili hupungua na hivyo, kuhitaji kujazilizwa tena. Aina ya kwanza ya sukari itumikayo mwilini na hasahasa ubongoni ni glukosi.

Mshuko wa sukari walioupata wale ambao hawakula au kunywa kwa kipindi kirefu, unaweza kusababisha ulegevu wa mwili.

Pindi sukari inapoliwa kwa njia ya chakula au kinywaji, viwango vya glukosi ya mwili hujisawazisha vyenyewe na kumfanya mtu aliyefunga asijihisi kuchoka sana na huwa na nuru zaidi ya macho.

Ingawaje tende, mara nyingi, si chakula kinachopendelewa sana na watu wenye njaa, lakini ndicho chakula kisicho na mafuta, na ni chanzo madhubuti cha sukari.

Nusu ya sukari zitolewazo na tende ni kwa ajili ya glukosi pekee. Usambazaji wa haraka-haraka wa glukosi itokayo kwenye tende huusaidia mwili kuodokana upesi na hali ya ulegevu kiasi kwamba mtu aliyefunga huweza kujimudu sawasawa katika ibada.

Mbali ya glukosi, tende pia ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi ambazo huwezesha michakato ya umeng’enyaji mwilini kuendelea, na huzuia tatizo la kushindikana kwa michakato hiyo ya uyeyushaji wa chakula mwilini.

Vilevile tende ni chanzo kizuri cha potasiamu, madini ambayo ni muhimu kwa usawazishaji wa maji mwilini. Hivyo, wale ambao hawapendelei ladha ya tende wanaweza kupata manufaa ya chakula hiki kwa kula angalau tende moja, na wale wanaopendelea tende, basi wanaweza kula tatu, tano, na kadhalika.

KUNYWA MAJI

Mwili wa binadamu, kwa kiasi kikubwa, unajengwa na maji. Faida za maji ni kubwa. Kama unavyohijati sukari kujirudishia nishati upesi, ndivyo unavyohitaji maji kujijazilizia ili uweze kufanya kazi vizuri.

Siyo tu maji huurudishia mwili maji upesi na kukata kiu, bali pia ni kisafishio asilia cha uchafu na sumu ambazo zimejilimbikiza kwa muda fulani.Kwa kutwa nzima, mtu mzima mwenye afya nzuri, hushauriwa kunywa jumla ya vikombe vinane vya maji.

Hii haijumuishi yale maji yatokanayo na vyakula kama vile matunda na mbogamboga.

Kwa vile mtu aliyefunga huwa hanywi maji muda wote wa swaumu yake, basi naye anahitajika kufikisha kiwango hicho cha unywaji wa maji kabla ya daku na baada ya futari.

Inapendekezwa hivi, kwamba mwanzoni mwa kufuturu, mtu anywe kiasi kidogo cha maji (nusu kikombe au kikombe kimoja), na baada ya kufuturu, anywe maji kwa viwango vidogo muda baada ya muda (mathalani nusu kikombe au kikombe kimoja kila baada ya saa moja).

Hii itaepusha ujazo mkubwa wa maji tumboni kwa wakati mmoja na itarejesha maji mwilini kidogokidogo kabla ya swaumu inayofuata

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Athari za Moshi wa sigara kwa mtoto

Athari za Moshi wa sigara kwa mtoto

Utafiti uliofanyika nchini Marekani umebaini kwamba watu wazima wasiovuta sigara lakini walipokuw... Read More

Sababu na madhara ya tatizo la kukosa choo

Sababu na madhara ya tatizo la kukosa choo

Tatizo la kukosa choo (constipation) ni tatizo ambalo limekuwa likiwakumba watu wengi sana katika du... Read More
Mambo muhimu kujua Kuhusu Uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke

Mambo muhimu kujua Kuhusu Uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke

Naamini umeshawahi kusikia kuhusu changamoto ya uvimbe kwenye kizazi kwa Wanawake yaani Fibroids.... Read More

Chanzo na Matibabu ya Tatizo la Mtindio wa Ubongo (Kupooza ubongo)

Chanzo na Matibabu ya Tatizo la Mtindio wa Ubongo (Kupooza ubongo)

Tatizo la Mtindio wa Ubongo au Kupooza ubongo kitaalamu ni Cerebral plasy (CP), ni hali ya kupooz... Read More

Faida za matumizi ya Ukwaju kiafya

Faida za matumizi ya Ukwaju kiafya

Faida kuu za ukwaju ni kama ifuatavyo:

Huondoa sumu Mwilini

Chanzo kizuri cha viua ... Read More

Tiba kwa kutumia maji

Tiba kwa kutumia maji

⭕Tiba kwa kutumia maji⭕
💧💧💧💧💧💧💧💧💧

Hamuwezi kuamini! mar... Read More

Vitu vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume

Vitu vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume

Vifaa vya kieletroniki

Vifaa vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa ... Read More

Vyakula vya kukusaidia kupunguza uzito

Vyakula vya kukusaidia kupunguza uzito

Kuchagua vyakula sahihi kwa mlo wako inaweza kuwa changamoto na tungependa kuamini kwamba kupungua u... Read More
Umuhimu wa kula fenesi kiafya

Umuhimu wa kula fenesi kiafya

Fenesi ni miongoni mwa matunda ya msimu yenye umbo la kipekee huku likiwa na ladha tamu isiyomith... Read More

Madhara ya kutumia dawa za kuzuia mimba wakati wa hatari

Madhara ya kutumia dawa za kuzuia mimba wakati wa hatari

Watu wengi hasa vijana watakuwa wanafahamu dawa ambazo hutumiwa sana kuzuia ujauzito pale ambapo ... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia barafu

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia barafu

Barafu inaweza kuzipunguza chunusi zionekane ni ndogo na kupunguza madhara yatokanayo na chunusi.... Read More

Faida na jinsi ya kutumia mbegu ya Parachichi kiafya

Faida na jinsi ya kutumia mbegu ya Parachichi kiafya

Leo nimekuletea matumizi ya mbegu ya parachichi yenyewe yaani ile inayokuwa katikati ya tunda la ... Read More