Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Madhara ya dawa za kuulia wadudu maarufu kama viwatilifu

Featured Image

Dawa za kuulia wadudu maarufu kama viwatilifu zimetengenezwa kwa lengo la kuangamiza wadudu wanaoharibu mazao au wanaomdhuru binadamu. Hata hivyo kutokana na sababu kuwa lengo la dawa hizi ni kuangamiza, huathiri pia viumbe hai vingine akiwemo binadamu.

Takwimu kutoka shirika la afya duniani WHO zinabainisha kuwa kuna zaidi ya vifo 220,000 vitokanavyo na athari za sumu zilizoko kwenye dawa za kuulia wadudu—viwatilifu.

Ikiwa unataka kuweka afya yako salama, basi karibu nikushirikishe athari 8 kiafya za dawa za kuulia wadudu — viwatilifu.

1. Husababisha saratani.

Watafiti mbalimbali wa maradhi ya saratani wanaeleza kuwa dawa za kuulia wadudu zinachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha seli za saratani mara zinapoingia kwenye mwili wa binadamu.

Hatari hii hutokea zaidi pale ambapo mtu anakula vyakula vilivyoathiriwa na sumu za dawa za kuulia wadudu.

2. Huvuruga mfumo wa homoni.

Mwili wa binadamu huzalisha homoni mbalimbali zinazowezesha viungo mbalimbali kufanya kazi vyema.

Dawa za kuulia wadudu zinapoingia mwilini huathiri mfumo wa homoni wa binadamu na kuufanya usifanye kazi vyema.

3. Huathiri mfumo wa uzazi.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa matatizo ya uzazi kati ya wanaume na wanawake huchangiwa kwa kiasi kikubwa na athari za dawa za kuulia wadudu.

Inaelezwa kuwa sumu hizi zinapoingia mwilini kupitia matunda au mbogamboga huharibu mfumo wa uzazi na kusababisha ugumba au utasa.

4. Huharibu ubongo.

Madawa ya kuulia wadudu — viwatilifu huathiri pia mfumo wa ubongo hasa kwa watu wanaoyapulizia au kukaa nayo karibu kwa muda mrefu.

Maradhi kama vile Mild Cognitive Dysfunction (MCD) ambayo humfanya mtu ashindwe kutambua vyema maneno, rangi au namba huchangiwa kwa kiasi kikubwa na athari za dawa za kuulia wadudu.

5. Huathiri mama mjamzito na mtoto

Mama mjamzito anatakiwa kuchukua tahadhari nyingi sana wakati wa ujauzito ili kulinda afya yake na mtoto aliyeko tumboni.

Matumizi ya viwatilifu ndani ya nyumba au karibu na makazi kwa lengo la kuua wadudu kama vile mbu, chawa, kunguni, au utitiri kunaweza kumwathiri mama mjamzito na mtoto kwa kiasi kikubwa.

Inaelezwa kuwa sumu hizi zinaweza kusababisha mtoto kuzaliwa bila viungo vyote, kuzaliwa kabla ya wakati au hata kifo.

6. Huharibu viungo muhimu vya mwili

Kumekuwa na taarifa mbalimbali ulimwenguni zikieleza kuwa dawa za kuulia wadudu huharibu viungo muhimu vya mwili kama vile figo na ini.

Utafiti uliofanyika huko India ulibaini kuwa watu wengi waliokufa kutokana na maradhi ya figo waliishi katika mazingira yenye sumu za kuulia wadudu au kula vyakula vyenye mabaki ya sumu hizo.

7. Huathiri mfumo wa upumuaji

Kutokana na watu wengi kutumia dawa za kuulia wadudu bila kuvaa vifaa vya kujikinga, wengi huvuta sumu zilizoko kwenye dawa hizo na kusababisha kuathiri mfumo wa upumuaji hasa mapafu.

Hivyo ili kujikinga na athari hii inashauriwa kuvaa vifaa bora vya kuzuia kuvuta sumu zilizoko kwenye dawa za kuulia wadudu.

8. Huathiri ngozi

Kama ilivyo kwenye swala la kuathiri mfumo wa upumuaji, watumiaji wengi wa dawa za kuulia wadudu hawakingi ngozi zao kwa mavazi au vifaa maalumu vinavyoepusha athari za dawa hizo kwenye ngozi zao.

Ikumbukwe kuwa sumu zilizoko kwenye dawa za kuulia wadudu zinaweza kuingia mwilini kirahisi kupitia ngozi na kusababisha athari nyingi za kiafya.

Naamini umeona jinsi ambavyo dawa za kuulia wadudu — viwatilifu zinavyoweza kuathiri afya ya binadamu ikiwa hazitatumiwa kwa uangalifu na kwa kufuata kanuni muhimu za matumizi yake.

Ikumbukwe kuwa vifo vingi na matatizo mbalimbali ya kiafya hutokana na mwili wa binadamu kukutana na sumu mbalimbali, hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Faida za kula ukwaju

Faida za kula ukwaju

Ukwaju ni tunda maarufu sana ambalo hupatikana katika maeneo yenye uoto wa kitropiki. Kwa kingere... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia kitunguu swaumu

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu hujulikana kama kitu cha kushangaza katika tiba huko mashariki ya mbali, Kitunguu... Read More

Sababu ya tatizo la Tumbo kujaa gesi na jinsi ya kujitibu

Sababu ya tatizo la Tumbo kujaa gesi na jinsi ya kujitibu

Tatizo la tumbo kujaa gesi husababishwa na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula ... Read More
Mambo 8 ya kushangaza yanayofanywa na mwili wako kukulinda pasipo wewe kujua

Mambo 8 ya kushangaza yanayofanywa na mwili wako kukulinda pasipo wewe kujua

Mwili wa binadamu unafanya mambo
mengi ya kibaiolojia ambayo mara
nyingi ni vigumu kuya... Read More

Vyakula 7 vya kuepuka kula ili uwe na afya nzuri

Vyakula 7 vya kuepuka kula ili uwe na afya nzuri

Inasemwa kuwa “wewe ni kile unachokula” kwa kumaanisha kuwa mwonekano wetu na afya ya mwili n... Read More

Mambo ya Msingi kujua kuhusu rangi ya mkojo wako

Mambo ya Msingi kujua kuhusu rangi ya mkojo wako

Je unafahamu ya kwamba rangi ya mkoja inakupa matokea sahihi kuhusu afya yako? Kama jibu ni hapan... Read More

Faida 14 za kufunga chakula

Faida 14 za kufunga chakula

Watu wengi wanafahamu kuwa kufunga kula ni swala linalohusiana na imani zaidi. Wengi hawafahamu k... Read More

Sababu za magonjwa ya figo na jinsi ya kuondokana na janga la magonjwa ya Figo

Sababu za magonjwa ya figo na jinsi ya kuondokana na janga la magonjwa ya Figo

1.Usichelewe kwenda HAJA. Kutunza mkojo kweye kibofu chako kwa muda mrefu ni wazo ... Read More
Unachotakiwa kujua kuhusu Shinikizo la chini la damu

Unachotakiwa kujua kuhusu Shinikizo la chini la damu

Ugonjwa wa Shinikizo la chini la damu ambao hujulikana kama hypotension kwa Kiingereza ni hali am... Read More

Jinsi ya kufanya ili upate mtoto wa kike au wa kiume

Jinsi ya kufanya ili upate mtoto wa kike au wa kiume

Katika urutubishaji yai la mwanamke linabeba chromosome X yani XX. Na mbegu ya mwanaume inabeba c... Read More

Mambo 9 ya kuzingatia kuepuka ugonjwa wa saratani au Kansa

Mambo 9 ya kuzingatia kuepuka ugonjwa wa saratani au Kansa

Tafiti nyingi zilizolizofanywa zinaonesha kuwa sababu kuu zinazosababisha saratani ni mtindo wa mais... Read More
Umuhimu wa kupata chanjo

Umuhimu wa kupata chanjo

Siku zote sisi wanadamu huwa tunaambizana kuwa, kinga ni bora kuliko tiba, tukiwa na maana kwamba... Read More