Updated at: 2024-05-25 17:06:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mwenzenu nilikatiwa umeme jana basi leo si nikaamua kwenda kununua luku ya 10,000. Kufika njiani nikatamani fursana nikaingia kijisupermarket mara sindo nakutana na ex wangu! Mshenzi yule kaniona mimi sijui alikua na mpango wa kununua vocha ya jero eti kabadili kanunua vocha ya buku tano ilimradi nione maisha yake safi tangu tuachane. Mambo ya kijinga spendi kudadeky nimetoa buku kumi nikanunua mipampers nami nijifanye nimeowa nina mtoto halafu huyoo nikashika njia yangu.
Sasa washkaji zangu tafadhalini mwenye mtoto au shida ya pampers naomba anunue kwangu maana leo nalala tena kiza πββ
Eti ni kweli hii ni sababu wanaume wana Upendo Sana?
Updated at: 2024-05-25 16:52:50 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wanaume wana upendo kwa kweli.
Mwanaume hata akipewa kundi la wanawake 90 achague mmoja!! Hata akichagua mzuri kupita wote bado roho itamuuma kuwaacha wale 89 waliobaki!!* Kwa namna hii wanaume wana Upendo Sana ππππππ
Updated at: 2024-05-25 17:51:30 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Lakini sisi wanaume hatuko fair β¦ Yani demu anang'ng'ana kujipodoa uso na sisi tunaangalia matako. πππmungu anatuona jamanππππππMakeup ya matako iletwe
Updated at: 2024-05-25 16:57:53 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ukimchoka mkeo, waweza kumtaftia sababu za kumuacha kama hizi
_ 1. Missed calls 16? Umeua betri la simu yangu. Kwa hiyo hata mimi unaweza kuniuaβ¦ It's Over!!! _ 2. Hata hunieshimu. Mi naongea na wewe lakini we upo bize unavuta pumzi? It's over! _ 3. Nimekupigia umepokea simu hapohapo. Huna subira. Itβs over!! _
4. Nilikwambia huwa napenda chakula cha moto lakini hujanipashia ice cream. Hunijali. It's over! _ 5. Nimekupa mayai mawili, moja uchemshe jingine ukaange. We umekaanga ambalo ulitakiwa kuchemsha na umechemsha ulilotakiwa kukaanga. Huniheshimu, Itβs over! _ 6. Nimekuita DARLING na wewe ukaniita HONEY. Yani kwa maana nyingine unamuita mama yangu NYUKI. Huheshimu wazazi wangu, fungasha kilicho chako. its over.
Kilichotokea baada ya mzungu na mbongo kukaa siti moja, bongo wasanii wengi
Mzungu akamdharau sana Mbongo nakujiona anajua kila kitu duniani!,
Akamwambia Mbongo waulizane maswali na Mbongo akishindwa anatoa sh.500 na endapo yeye atashindwa atatoa 100,000/=.
Mzungu akauliza ni nchi ipi ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya Dunia?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hajui.
Updated at: 2024-05-25 18:06:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mzungu akamdharau sana Mbongo nakujiona anajua kila kitu duniani!,
Akamwambia Mbongo waulizane maswali na Mbongo akishindwa anatoa sh.500 na endapo yeye atashindwa atatoa 100,000/=.
Mzungu akauliza ni nchi ipi ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya Dunia?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hajui.
Na yeye akamuuliza Mzungu ni kitu gani kikienda juu kina miguu minne na kikirudi chini kina miguu mitatu?
Mzungu akafikiria akakosa jibu akatoa 100,000/= kuashiria hajui ila akataka kujua, akauliza ni nini hicho?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hata yeye hajui!.
SHARE na marafiki kama umemkubali Mbongo kwa ujanja. Lakini unafikiri Mbongo huyu kwa akili hizi atakuwa ametokea mkoa gani!?.