Eti kwa nini Watu hawapostigi hii? Hata selfie sijaonaga
Updated at: 2024-05-25 16:59:02 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vijana mkiwa mnaendesha magari mna post mukiwa mpo beach mna post mkiwa kwenye masherehe mna post Lakin mkiwa mmeenda kwa mganga siwaoni kupost mitunguli na vibuyu vya mganga unakuwa je wa zee tena. 😀😀😀😀
Wachaga wana mambo mbele ya hela, angalia hii bili ilivyomchanganya MASSAWE
MASSAWE alienda na marafiki zake bar kunywa, baada ya kumaliza kutumia akaletewa bili kama ifuatavyo:
Manka 35,000
Marieta 20,000
Kekuu 30,000
Kitime 15,000
Updated at: 2023-04-29 22:52:15 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
MASSAWE alienda na marafiki zake bar kunywa, baada ya kumaliza kutumia akaletewa bili kama ifuatavyo: Manka 35,000 Marieta 20,000 Kekuu 30,000
Kitime 15,000 Kinabo 10,000 TOTAL 110,000/= MASSAWE akaicheki akasema "Wote nitawalipia lakini huyo "TOTAL" Yesuu simlipii. Kwansa anamiliki sheli kibao sa mafuta hapa bongo. Shensi taip ! Na amekunywa nyingi kuliko wote alipe mwenyewe…
Updated at: 2024-05-25 18:09:37 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?
MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee. MALAIKA: Kwa nini? MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni. Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?
Ungekua wewe ni mwalimu ungemshauri nini huyu mwanafunzi?
Updated at: 2024-05-25 18:09:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.
MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
MWAL: Na wewe James??
JAMES: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiwe……"
Akameza mate kisha akaendelea….
"Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali."
MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??
Updated at: 2024-05-25 16:53:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
1, mwanaume kuoga haraka haraka ili uwahi kuangalia igizo, huo ni UMAMA..😂
2, mwanaume kupiga picha umeng'ata Lips na Unapiga na Camera Beauty Plus huo ni UMAMA..😂
3, Mwanaume kuangalia tamthilia na Jamai Raja na Maigizo kwenye chanel ya sinema zetu wakati mechi za kombe la dunia zinaendelea, pia nawe ni MMAMAA…😂😂
4, Mwanaume kuandika 'Jomon' badala ya Jamani, kuandika 'Pw' badala ya Poa, kuandika 'Thatha' badala ya Sasa, kumwandikia mwanaume mwenzio 'Mambo my' Huu ni UDADA, tena UDADA wa CHUO..😂 . 5, Mwanaume kunywa soda au Juice na kubakisha, kununua chakula halafu unakibakisha, kubagua bagua chakula na kujamba hovyo hovyo baada ya kushiba, huo nao ni UMAMAA..😂 . 6, Mwanaume kumuuliza mwanaume mwenzio anapata faida gani kuangalia Mpira, pia nawe ni MMAMA… . 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂