Baada ya kumkuta mwanamme mwingine chumbani kwake na mke wake cheki huyu anachokifanya
NAKUA(BABA) karudi kazini mwanae mdogo akamuwahi, DOGO: Baba usiingie ndani kina jini chumbani kwenu NAKUA: Hakuna kitu kama hicho DOGO: Kweli baba kuna jini liko kwenye kabati lenu la nguoβ¦.
Updated at: 2023-04-29 22:53:31 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
NAKUA(BABA) karudi kazini mwanae mdogo akamuwahi, DOGO: Baba usiingie ndani kina jini chumbani kwenu NAKUA: Hakuna kitu kama hicho DOGO: Kweli baba kuna jini liko kwenye kabati lenu la nguoβ¦.
NAKUA kaingia ndani kamkuta mkewe kalala kitandani kajifunika shuka gubigubi hadi kichwani. Kaenda kwenye kabati kufungua mlango , akamkuta rafiki yake wa miaka mingi yuko uchi ndani ya kabati NAKUA: Aise unajua we fala sana, we rafiki yangu miaka yote hiyo halafu unamtisha mwanangu eti wewe jini, hebu toka huko nenda kwenu kacheze michezo hiyo na mwanao.
Angalia alichokifanya huyu mtu baada ya kuokota wallet ya thamani
Updated at: 2024-05-25 17:15:08 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station "naitwa Juma nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki7, ATM card na karatasi yenye PIN ya ATM card na kijimfuko cha dhahabu" Mtangazaji akasema, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama anakusikiliza? Jamaa akajibu; hapana, ninaomba kumuombea dedication wimbo wa R.Kelly usemao "U SAVED ME" umfikie popote alipo!!
Hii ndio maana ya Matatizo, usiombee hili likukute
Updated at: 2024-05-25 16:53:58 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Matatizo ni nini???
`Matatizo ni pale unapokuwa umefika ukweni usiku na haja kubwa ikakubana na hukuwa unajua choo kilipo, ukatoka nje na kujisaidia kwenye majani kumbe ni mboga asubuhi ukasikia mama mkwe anasema kuna mjinga kajisaidia kwenye mboga na kaangusha pochi yake hapohapo haa! Vile unajisachi pochi hamna na kulikuwa na passport,vitambulisho, kadi ya benki, pesa zaidi ya laki 2 na nusu, funguo za nyumba yako, ` π€π€π€π€π€π€π€π€π€
Updated at: 2024-05-25 17:06:20 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Umeenda kutembea ukweni kwako baada ya chakula chausiku unapewa chumba chakulala inapofika usiku unatakakutoka kwenda kujisaidi kwasababu taa zimezimwa unapamia vyombo vya chakula sebleni kipindi unajalibu kupapasa uviweke sawa mala taa inawashwa na mama mkwe anaona umeshika vyombo anakwambia, baba kama ukushiba ungesema
Updated at: 2024-05-25 17:50:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
CHEKA KIDOGO Majambaz waliliteka gar moja lililokua limeshehen abiria Baada ya abiria kusachiwa na majambaz hao na kukutwa hawana pesa, majambaz wakasema kila m2 atapigwa viboko (bakora) kutokana na namba ya shati alilovaa Aliyekua hana namba atasalimika Kaz ikaanza, jamaa alievaa jez ya ROONEY wa Man U akapigwa fimbo 10, mwengine alievaa nguo ya 50cent akapigwa 50, n.k, sasa kwa pemben kulikua na jamaa analia sn yaani kila akijiangalia, kumbe alikua amevaa fulana limeandikwa LOWASA 2015 duuuh! Unajua kilichotokea ngoja niweke cm chaji kwanza.