Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Nia yako isishindwe

Featured Image

Nimejifunza jambo kubwa sana ambalo sote tuna lijua nalo ni "NIA".
Nimemtazama mwendesha pikipiki anaiwasha pikipiki kwa muda mrefu kwa kupiga kiki kwa kurudia rudia, akiamini lazima iwake ili aende anakotaka kwenda. Anajaribu kuwasha kwa kiki ikikataa anajaribu kwa starter, ikigoma anajaribu kuchomoa plug na kuangalia kama kuna tatizo, anajaribu tena na tena mpaka inawaka, anaanza safari yake.

Ingawa ametumia muda mwingi kuhangaika kuiwasha pikipiki yake lakini hakuzimia moyo na kuamua kuitelekeza ili atembee kwa miguu, ila alikua na "NIA" isiyozimika haraka mpaka atakapoona imewaka kwakua anaamini jana iliwaka, lazima na leo iwake hata kama imelala kwenye hali ya hewa ya namna gani.

Ikiwa tunakua na "NIA" ya kufanya mambo madogo madogo yatokee, na tunayasimamia kwa "IMANI" kabisa mpaka yanakua kweli, kwanini tunaogopa kusimamia mambo makubwa yatokee maishani mwetu?. Kwanini unadiriki kusema kwenu hakuna aliyewahi kufanikiwa, hakuna anae miliki gari ya thamanani, hakuna aliyejenga nyumba ya kifahari, hakuna…hakuna….

Kwanini "NIA" yako uilinganishe na kushindwa kwa hao wengine kwenu? Wewe ni mmoja wa tofauti, na ukiamua kujitenga kifikra mbali nao, na kufanya mambo makubwa kwa bidii bila kuzimia moyo, hakika utakua wewe kama wewe kuitwa MABADILIKO ya mafanikio katika hao wengi walioshindwa.

"NIA YAKO ISISHINDWE"

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Njia 8 za kupata mtaji kwa ajili ya Biashara yako

Njia 8 za kupata mtaji kwa ajili ya Biashara yako

Njia hizo ni kama ifuatayo!!

UJASIRIAMALI

Jifunze kanuni za fedha
kama ilivyoainishwa hapo chini.
Fedha inataki... Read More

Hofu inavyo tugharimu katika safari ya ujasiriamali na Jinsi ya kuiepuka

Hofu inavyo tugharimu katika safari ya ujasiriamali na Jinsi ya kuiepuka

Wengi wetu tunapenda Mafanikio, tunapenda kufika mbali tunapeda kuwa kama Mengi siku moja.

... Read More

Jiwekee Utaratibu utakaokuwezesha kuamua vizuri juu ya fedha utakazopata

Jiwekee Utaratibu utakaokuwezesha kuamua vizuri juu ya fedha utakazopata

Jiwekee utaratibu utakaokupa uzoefu wa kuamua vizuri juu ya fedha unazopata. Watu tumekuwa tukitu... Read More

Hichi ndicho unatakiwa uwe nacho kulingana na umri wako

Hichi ndicho unatakiwa uwe nacho kulingana na umri wako

20 - 25 =Iwe kama ni kielimu hujafikia malengo yako,sitisha mara moja tafuta kazi/biashara ya kuf... Read More

Angalia utofauti wa mawazo ya maskini na tajiri

Angalia utofauti wa mawazo ya maskini na tajiri

MASKINI NA TAJIRI WANA MAWAZO TOFAUTI.
Maskini hudhani utajiri ni chanzo cha matatizo.
... Read More

Sababu inayopelekea kushindwa kuishi maisha ya ndoto zako

Sababu inayopelekea kushindwa kuishi maisha ya ndoto zako

1. Hauko Tayari kuthubutu na kujiunga
2. Kutokujiamini
3. Kutopata sehemu sahihi ya kup... Read More