Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Jiwekee Utaratibu utakaokuwezesha kuamua vizuri juu ya fedha utakazopata

Featured Image

Jiwekee utaratibu utakaokupa uzoefu wa kuamua vizuri juu ya fedha unazopata. Watu tumekuwa tukitumia fedha tunazopata bila kufikiria jinsi ya kugawa ktk matumiz badala yake baada ya kutumia ndio una/ninaanza kujuta Kwa nin nime/umetumia tofauti na mahitaji uliyonayo. Kiasi cha fedha ulichonacho chaweza kukufanya uwe maskini au tajir kutokana na maamuz unayofanya juu ya hiyo fedha. Ukitaka ufanikiwe na ukue kifedha jaribu kugawa fedha uliyopata Kwa mafungu yafuatayo:

A. Sadaka: ndani ya sadaka kuna; a. malimbuko, mith 3:9, b. zaka na c. dhabihu malaki 3:8. Hii inakusaida wewe kumpa Mungu nafasi ya kwanza mth 6:33
2.pia unaonyesha ya kuwa unahitaji msaada na hekima zaid ktk kugawa fedha zilizobaki. Hagai 1:2-11
3. Shukrani Kwa Mungu alivyokuwezesha kumb torat 8:11-20 4. Unaonyesha unahitaj msaada wa Mungu ktk kupata mbinu za kuongeza fedha ktk maisha yako mith 3:9,10. Ktk bahasha hii waweza kuweka 10% au zaidi kutokana na Roho mtakatifu akavyokuongoza.

B. Akiba, Uwe na tabia ya kujiwekea akiba Kwa ajil ya baadae au ukiwa mzee, kumb torat 28:8 na mwanzo sura ya 41 hadi 47 tunamwona Yusuphu alivyoweka akiba 20% ya mavuno ktk miaka saba ya baraka ambayo ilisaidia ktk miaka saba iliyofuata ya ukame. Hii inajusaidia kuweka akiba Kwa ajil ya maisha ya baadae Kwa kiwango maalum na Kwa mda Fulani zab 144:13a. Jifunze Kwa Chungu anayeweka akiba ya chakula wakati wa jua ambacho humsaidia wakati wa ukame mith 6:6-8. Omba Roho mtakatifu akuongoze kuweka akiba ili utumie pind ambapo hutakuw na pato.
C. Kuwekeza ;hii inakusaidia ili kujijengea tabia ya kuwa na mtaji wa kukusaidia kuzalisha pesa zaid Kwa kuanzisha mradi mwingine Luk 19:12.
D. Matumizi yaliyo ya lazima. Mungu ana uwezo wa kutupa tunachohitaji ila Mungu anataka tuwe na mahitaji Tito 3:14. Haya in matumiz ya kila siku kama chakula etc.

Unaweza ukaongeza bahasha maalumu Kwa ajil ya kuweka au kutunza fedha za kulipia madeni /ujenzi/ada kama kuna wanaosoma/ kodi ya nyumba/ maandalizi ya harusi etc.
Kugawa fedha katika Mafungu ya bahasha inakusaidia kuwa na utaratibu maalum wa kutumia fedha na pia inakusaidia kufanya maamuzi mazuri ju ya kila fedha unayopata.

SWALI: Je, fedha unayopata unagawaje kabla ya kutumia? Je, Unakumbuka bahasha no. 4 tu, au 4 &3 au 4 &2 au 1 &4 au 1,2& 4 au 1,3 &4 au 1,2,3&4. In Roho wa Mungu atakayekuongoza kugawa fedha na sio vinginevyo.

Unaweza sema sina mtaji wa kutosha au sina biashara yoyote au nimejaribu kufanya biashara au kuwekeza cjafanikiwa etc, hivyo ni visingizio. Unapingiza visingizio au manung'uniko unapelekea kukataa tamaa na pia unamzuia Roho Mtakatifu kukusaidia kuvuka ktk hali hiyo.
Jifunze kutoka Kwa watumwa hawa waliopewa mtaji na bwana wao na jinsi walivyotumia kuzalisha. Kila mmoja alipewa kiasi kadri ya uwezo wa uwezo wa mtu vivyo hivyo walitofautiana kupata faida ingawaje mmoja wao aliamua kufukia na mwisho alinyang'anywa na kupewa yule mwenye zaidi, Luka 19:12-26 na mth 25:14-29.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Ushauri wangu kwa leo: Zingatia hili, hamasika, badilika

Ushauri wangu kwa leo: Zingatia hili, hamasika, badilika

Tupo kwenye dunia ambayo tulikuta watu na tutawaacha watu.
Vyote tulivyovikuta vilianzishwa ... Read More

Ilinde ndoto yako

Ilinde ndoto yako

Watu wengi wanajiuliza, “Siri ya utajiri ni nini?” Je ni mbinu gani zin... Read More

MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI

MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI

✍🏽Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni ... Read More

Siri 39 za kuwa Milionea, Jinsi ya kupata pesa na kuwa tajiri

Siri 39 za kuwa Milionea, Jinsi ya kupata pesa na kuwa tajiri

1. Tafuta fursa kila kona. 2. Tumia kipaji chako. 3. Kuwa na nidhamu katika fedha - matumizi mazuri ... Read More
JINSI YA KUTENGENEZA BATIKI

JINSI YA KUTENGENEZA BATIKI

Batiki inatengenezwa kama ifuatavyo

MAHITAJI:

1.Vibanio vyenye urembo mbalimbali.Read More

Ni vizuri kujua haya

Ni vizuri kujua haya

👉🏿Degree au vyeti ulivyo navyo haviwezi kukupa mafanikio.
👉🏿Uzuri ulio nao hauwe... Read More

Mbinu 5 za kukunufaisha maishani

Mbinu 5 za kukunufaisha maishani

Mbinu 5 za kukufanikisha maishani Unaweza ukawa upo kwenye hali ya kulalamika maisha yako ni magumu ... Read More
Elimu tuu haitoshi kukunufaisha maishani na kukupa mafanikio

Elimu tuu haitoshi kukunufaisha maishani na kukupa mafanikio

EMBU SOMA HII KWA MAKINI SJUI NI KWELI? USIMAINDI LAKINI MAANA ITAKUGUSA TUU. MAFANIKIO YA MAISHA... Read More

FURSA HAIJI MARA MBILI: Jinsi unavyoweza kupata faida au hasara ukitumia Nafasi au fursa uliyonayo

FURSA HAIJI MARA MBILI: Jinsi unavyoweza kupata faida au hasara ukitumia Nafasi au fursa uliyonayo

Kwenye maisha fursa moja tu inatosha kabisa
kubadilisha hali yako ya sasa na kukuweka kwenye... Read More

JITAMBUE : Maisha yako ya kesho hayalingani na maisha yako ya jana, Anza sasa

JITAMBUE : Maisha yako ya kesho hayalingani na maisha yako ya jana, Anza sasa

THERE IS NO FUTURE IN THE PAST.** Ukitaka kufanikiwa usiangalie nyuma yako kunanini na ulishindwa... Read More