Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Nimwambie nini mtu anayejaribu kunishawishi nijihusishe na makundi ya watu wanaokunywa pombe na wavutaji sigara?

Featured Image

Kama umeamua kutovuta sigara wala kunywa pombe ni uamuzi
mzuri sana na wa kiafya. Ni haki yako binafsi kuchukua uamuzi
huu, kama vile watu wengine pia wanavyoruhusiwa kufanya
maamuzi kuhusu maisha yao wenyewe.

Mara nyingine ni vigumu sana, lakini kama umeamua hutaki
kujiunga na kundi la watu wavutao sigara au kunywa pombe ni
muhimu kusema hivyo. Jaribu kuwa wazi na kusema HAPANA.
Jaribu kueleza kwamba unataka kuishi maisha yenye afya bila
kutumia pombe na sigara na uwaeleze rafiki zako ni kwa nini.
Waambie kuwa unajua unachokifanya na kwamba umeridhika
kuwa uvutaji sigara na unywaji pombe unahatarisha afya yako,
unagharimu fedha nyingi na kukuzuia kufikia malengo yako.
Kama umeridhika na kuwathibitishia watu hao, hawatakusumbua
tena. Na kama unatafuta rafiki usisahau: Rafiki ni mtu anayejali,
kulinda na kuthamini maisha ya mwenzake! Kwa hivyo, ni kwa
vipi mtu ambaye anayekushawishi ufanye kitu cha kudhuru
afya yako kwa kusudi na haheshimu maamuzi yako awe rafiki
wa kweli?

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, mtu anaweza kuzuia kupata mimba baada yakujamiiana bila kinga (kufanya ngono zembe) kwa mfano amebakwa?

Je, mtu anaweza kuzuia kupata mimba baada yakujamiiana bila kinga (kufanya ngono zembe) kwa mfano amebakwa?

Kama umebakwa au kulazimishwa kujamiiana unaweza kupata
huduma katika hospitali, kituo cha a... Read More

Je, kuna matatizo yoyote kama mdomo wa msichana utagusana na shahawa?

Je, kuna matatizo yoyote kama mdomo wa msichana utagusana na shahawa?

Kama mpenzi wako hatakuwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa hakuna madhara ya kiafya. kama shaha... Read More

Jinsi ya Kukabiliana na Hisia za Kufadhaika na Utendaji wa Ngono

Jinsi ya Kukabiliana na Hisia za Kufadhaika na Utendaji wa Ngono

Jinsi ya Kukabiliana na Hisia za Kufadhaika na Utendaji wa Ngono πŸ’†πŸŒ‘οΈ

Karibu kijana... Read More

Nifanye nini ili kuepuka kubakwa na mpenzi/ rafiki?

Nifanye nini ili kuepuka kubakwa na mpenzi/ rafiki?

Kuna baadhi ya vidokezo ambavyo vinaweza kukusaidia: 1. Usikae faragha na mwenzi wako kabla hujawa t... Read More
Afya ya uzazi ni nini?

Afya ya uzazi ni nini?

Afya ya uzazi inahusiana na mfumo wa uzazi wa mtu, na via vya uzazi kwa watu. Kwa hali hiyo basi ina... Read More
Kuna fikra kuwa Albino ni watu wa kawaida je, kisayansi hii ni kweli?

Kuna fikra kuwa Albino ni watu wa kawaida je, kisayansi hii ni kweli?

Hii ni kweli kabisa. Watu wanaoishi na ualbino ni watu wa
kawaida kama binadamu wengine wote... Read More

Je, mvulana anaweza akafikia mshindo kwa njia ya kusugua uume na vidole na kuna madhara gani ukisugua uume na vidole?

Je, mvulana anaweza akafikia mshindo kwa njia ya kusugua uume na vidole na kuna madhara gani ukisugua uume na vidole?

Ndiyo, mvulana anaweza akafikia mshindo kwa njia ya kusugua uume na vidole. Anaposuguliwa uume na... Read More

Vidokezo vya Kuonyesha Shukrani kwa Msichana Wako

Vidokezo vya Kuonyesha Shukrani kwa Msichana Wako

Hivi karibuni, wanaume wengi wamekuwa wakikosa jinsi ya kuonyesha shukrani kwa msichana wao. Hata... Read More

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Kukosa Ujasiri wa Kujihusisha na Ngono?

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Kukosa Ujasiri wa Kujihusisha na Ngono?

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Kukosa Ujasiri wa Kujihusisha na Ngono? 🌈

Karibu kija... Read More

ATHARI ZA ULEVI KATIKA JAMII

ATHARI ZA ULEVI KATIKA JAMII

Watu wanokunywa kupitia kiasi huathiri jamii kwa njia mbalimbali. Madhara mengine hutokea kwa kuwa w... Read More
Ni hatua gani zinazochukuliwa na serikali ili kukomesha vitendo vya kuwinda Albino?

Ni hatua gani zinazochukuliwa na serikali ili kukomesha vitendo vya kuwinda Albino?

Kufuatia vitendo vibaya vya mauaji ya Albino, vilivyozuka
Tanzania tangu mwaka 2007 hadi sas... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili mawazo na hisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujadili mawazo na hisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Kwa wengi, ngono inaonekana kama kitendo cha kimwili tu bila ya umuhimu wa kujadili mawazo na his... Read More