Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

ATHARI ZA ULEVI KATIKA JAMII

Featured Image
Watu wanokunywa kupitia kiasi huathiri jamii kwa njia
mbalimbali. Madhara mengine hutokea kwa kuwa wanafanya
vitu ambavyo wasingevifanya iwapo wasingekuwa wamelewa.

Watu wakilewa, huweza kuwa na hasira, wagomvi hivyo basi
huwadhuru wengi kiakili na kimwili. Isitoshe, ajali nyingi za
kazini na barabarani hutokea watu wakiwa wamelewa. Mara
nyingi watu wasiokuwa na hatia na vilema hupoteza maisha yao
kutokana na ajali zinazohusiana na ulevi.

Watu wanaokunywa
pombe kupita kiasi hupunguza uangalifu na hivyo basi kuchangia
katika kuenea kwa VVU kwenye jamii. Watu wanaokunywa pombe
wanaweza pia kufanya ujambazi katika jamii. Pia wanaokunywa
kupita kiasi si wafanyakazi wa kutegemewa kwani hutumia
muda mwingi nje ya sehemu zao za kazi.

Watu waliozoea kunywa pombe nyingi hupoteza pesa zao nyingi
kununua pombe na muda wao mwingi kufikiria jinsi ya kupata
pesa za kunywea pombe.

Kutokana na gharama za kununua
pombe familia zao hukosa pesa za vitu muhimu kama kodi ya
nyumba, ada na sare za shule na chakula.

Vijana wanaokunywa pombe huanza kuiba pesa nyumbani kwao
ili kununulia pombe. Matumizi mabaya ya pombe mara nyingi
husababisha matatizo au kuvunjika kwa familia, au urafiki.

Vilevile husababisha matokeo mabaya shuleni au kuacha kabisa
shule, hali ambayo inaweza kusababisha kukosa nafasi za kazi,
kujitegemea wewe mwenyewe na kusaidia famila yako na jamii.
AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Ndoa ya kulazimishwa

Ndoa ya kulazimishwa

Ndoa ya kulazimishwa ni ile ambayo mwanamume au mwanamke
anaozwa bila yeye mwenyewe kukubali... Read More

Kwa nini ni Lazima Kufanya Ngono na Mtu Mmoja Tu?

Kwa nini ni Lazima Kufanya Ngono na Mtu Mmoja Tu?

Kwa nini ni Lazima Kufanya Ngono na Mtu Mmoja Tu? 🌸

Asante kwa kujiunga nami katika mak... Read More

Je, mapacha wanapatikanaje?

Je, mapacha wanapatikanaje?

Zipo aina mbili za mapacha, wale wanaofanana na wale wasiofanana. Karibu robo ya mapacha wote hufana... Read More
Je, Ni Sahihi Kutumia Dawa za Kuzuia Mimba?

Je, Ni Sahihi Kutumia Dawa za Kuzuia Mimba?

Je, Ni Sahihi Kutumia Dawa za Kuzuia Mimba? 🌼😊

Tunaelewa kwamba vijana wetu ni kikun... Read More

Je, kuna madhara yoyote pale utakapojaribu kutumia dawa za kulevya mara moja tu au utakapotumia kwa kiasi kidogo sana?

Je, kuna madhara yoyote pale utakapojaribu kutumia dawa za kulevya mara moja tu au utakapotumia kwa kiasi kidogo sana?

Kutumia dawa za kulevya kwa kiasi kidogo kunaweza kusilete madhara i ila mpaka tu pale utakapoyaz... Read More

Je, kuna madhara gani yatokanayo na uvutaji sigara kwa vijana hasa kijana Albino?

Je, kuna madhara gani yatokanayo na uvutaji sigara kwa vijana hasa kijana Albino?

Kuna madhara mengi ambayo hutokana na uvutaji sigara.
Madhara mengi yanampata mvutaji kwani ... Read More

Je, nikijamiiana na mtu mwenye virusi vya UKIMWI bila kutumia kondomu, nitapata virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Je, nikijamiiana na mtu mwenye virusi vya UKIMWI bila kutumia kondomu, nitapata virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Uwezekano wa kuambukizwa na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI ukijamii ana na mtu mwenye virusi vya UKI... Read More

Jinsi ya Kuwa na Uhuru katika Uhusiano wako na Msichana

Jinsi ya Kuwa na Uhuru katika Uhusiano wako na Msichana

Kila mtu anataka kuwa na uhuru katika uhusiano wao na msichana wao. Lakini wakati mwingine inawez... Read More

Inawezekana msichana akapata mimba kabla ya kuvunja ungo?

Inawezekana msichana akapata mimba kabla ya kuvunja ungo?

Msichana anaweza kupata mimba kabla ya kuvunja ungo, yaani kabla ya kuona hedhi kwa mara ya kwanz... Read More

Nani anavalisha kondomu ya kiume, je ni mwanamke au mwanaume?

Nani anavalisha kondomu ya kiume, je ni mwanamke au mwanaume?

Katika kufanya mapenzi iwe mwanaume anayeweka kondomu uumeni au iwe mwanamke anayeshugulika kuwek... Read More

Kwa nini Albino wanatengwa katika masuala ya mapenzi na wale watu ambao siyo Albino?

Kwa nini Albino wanatengwa katika masuala ya mapenzi na wale watu ambao siyo Albino?

Watu huogopa kujaribu vitu au mambo ambayo hawajayazoea
au yale ambayo yapo tofauti. Jinsi u... Read More

Je, watu wanaamini nini katika kuongeza mchezo wa hisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanaamini nini katika kuongeza mchezo wa hisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanaamini nini katika kuongeza mchezo wa hisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi? Kufanya ... Read More