Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Jinsi ya kutumia kondomu ya kike

Featured Image

Kondomu ya kike inafahamika kwa jina la „care“ na “Lady Peteta”. Hapa Tanzania hazipatikani sehemu zote na bei yake ni kubwa kidogo.
Kondomu ya kike huingizwa ukeni kabla ya kujamiiana. Kama unatumia kondomu ya kike, chana kwa uangalifu pembezoni mwa pakiti. Kondomu ina pete mbili za plastiki na uwazi upande wa juu. Pete moja imelegea ni ndogo na iko kwa ndani, upande usio na uwazi. Pete ya pili ni kubwa zaidi, imeshikiliwa na iko upande wa tundu. Shikilia kondomu upande uliozibwa na minya pete ya ndani kwa dole gumba na kidole cha pili na cha kati. Mara nyingine inaweza ikakuponyoka, (kuteleza) lakini endelea kujaribu hadi umeiminya vizuri. Tafuta mkao mzuri na ingiza kondomu ya kike. Huku bado unaminya kwa vidole vyako iongoze kondomu ndani ya uke wako. Ukiiachia pete ya ndani itashikilia kondomu ndani ya uke. Sasa ingiza kidole chako kwenye kondomu, sukuma pete mpaka inapogota kwenye mlango wa uzazi.
Kondomu ya kike inaweza kuvaliwa saa kadhaa kabla ya kufanya ngono na pia inaweza kuvuliwa baada ya muda wa kufanyika ngono kupita. Ili kuhakikisha kuwa uume umeingia sehemu husika, msaidie mwenzi wako kuongoza uume kuingia kwenye uke ili usipenye pembeni.
Baada ya kujamiiana, vua kondomu kwa uangalifu. Tupa kondomu iliyotumika kwenye choo cha shimo au uichome. Usitupe kondomu iliyotumika ovyo.
Kama ilivyo kwa kondomu ya kiume, kondomu ya kike itatumika kwa mafanikio zaidi pale ambapo wahusikia wanakuwa na makubaliano na maelewano juu ya matumizi yake.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, pombe ni moja ya sababu za kuenea kwa Virusi vya UKIMWI na VVU au magonjwa mengine yatokanayo na kujamiiana?

Je, pombe ni moja ya sababu za kuenea kwa Virusi vya UKIMWI na VVU au magonjwa mengine yatokanayo na kujamiiana?

Matumizi mabaya ya pombe ndiyo yanayosababisha kuenea kwa
VVU au magonjwa mengine yatokanayo... Read More

Jinsi ya Kukabiliana na Ushinikizaji wa Kufanya Ngono kabla ya Wakati

Jinsi ya Kukabiliana na Ushinikizaji wa Kufanya Ngono kabla ya Wakati

Jinsi ya Kukabiliana na Ushinikizaji wa Kufanya Ngono kabla ya Wakati

Karibu vijana wapend... Read More

Jinsi ya kufanya wazazi wamkubali mchumba

Jinsi ya kufanya wazazi wamkubali mchumba

Uhusiano mzuri na wazazi ni muhimu sana siyo katika masuala ya uchaguzi wa mchumba tu, bali katika m... Read More
Vidokezo vya Kufanya Msichana Ajiambie Kuwa Anakupenda

Vidokezo vya Kufanya Msichana Ajiambie Kuwa Anakupenda

Kila mwanamume anapenda kujua kama msichana anayempenda anahisi hivyo hivyo kumhusu. Lakini sio k... Read More

Nifanyeje kuepuka vishawishi vya kujamiiana kutoka kwa watu wengine, hasa wakubwa?

Nifanyeje kuepuka vishawishi vya kujamiiana kutoka kwa watu wengine, hasa wakubwa?

Vijana wengi wanajikuta wanatumbukia katika matatizo mazito kama kupata mimba mapema, utoaji wa m... Read More

Je, Ni Vipi Kuepuka Kufanya Ngono Kwa Shinikizo la Kutaka Kupendwa?

Je, Ni Vipi Kuepuka Kufanya Ngono Kwa Shinikizo la Kutaka Kupendwa?

Je, Ni Vipi Kuepuka Kufanya Ngono Kwa Shinikizo la Kutaka Kupendwa? 🤔

Kuna wakati maish... Read More

Je, mvulana atajuaje kama msichana ni bikira? Na pia, msichana anaweza kujitambua vipi kama ni bikira?

Je, mvulana atajuaje kama msichana ni bikira? Na pia, msichana anaweza kujitambua vipi kama ni bikira?

Mvulana hawezi kuthibitisha ubikira wa msichana kwa njia ya kumwangalia wala kwa njia ya kumwingi... Read More

Njia ya kuzuia mimba inayofaa kwa kijana anayeanza kujamiiana

Njia ya kuzuia mimba inayofaa kwa kijana anayeanza kujamiiana

Kila njia ya kuzuia mimba ina faida na hasara zake. Kwa mfano faida ya vidonge ni kwamba kama mwa... Read More

Kwa nini dawa hutengenezwa na kutumika hospitalini wakati zina madhara?

Kwa nini dawa hutengenezwa na kutumika hospitalini wakati zina madhara?

Baadhi ya dawa za kulevya pamoja na dawa za kutibu, hutumika hospitali kuokoa maisha na kupunguza... Read More

Afya ya uzazi ni nini?

Afya ya uzazi ni nini?

Afya ya uzazi inahusiana na mfumo wa uzazi wa mtu, na via vya uzazi kwa watu. Kwa hali hiyo basi ina... Read More
Njia za Kufanya Msichana Amevutiwa na Wewe kwa Muda Mrefu

Njia za Kufanya Msichana Amevutiwa na Wewe kwa Muda Mrefu

Habari wapendwa, leo tutazungumzia njia za kufanya msichana amevutiwa na wewe kwa muda mrefu. Kun... Read More

Kujikinga na Maambukizi ya UKIMWI: Njia za Kuepuka Hatari

Kujikinga na Maambukizi ya UKIMWI: Njia za Kuepuka Hatari

Kujikinga na Maambukizi ya UKIMWI: Njia za Kuepuka Hatari

  1. Jambo zuri ni kuwa na ... Read More