Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Mambo 10 yanayosababisha wanawake washindwe kupata mimba au wawe wagumba

Featured Image

Ugumba ni nini ?
Hii ni hali ya wapenzi au mke na mume kutopata ujauzito. Ugumba unaweza kua primary infertility yaani mtu hajawahi kubeba mimba kabisa tangu azaliwe au secondary infertility yaani mtu ambaye amewahi kuzaa lakini kwa sasa ameshindwa kubeba ujauzito. utafiti uanonyesha katika kila ndoa tano au mahusiano matano ya kimapenzi basi uhusiano mmoja una matatizo ya uzazi ya kushindwa kuzaa.

Hali hii imekua ikiongezeka kadri miaka inavyosonga mbele kwa sababu mbalimbali kama mionzi ya mawasiliano yaani wi-fi , magonjwa mapya ya binadamu na kadhalika. Kwa wanawake utafiti mpya unasema uwezo wao wa kubeba mimba unaanza kupungua baada ya miaka 30 ya umri kutokana na kuanza kuishiwa nguvu kwa viungo vya uzazi.

Ugumba una vyanzo vingi sana ambavyo vingine havifahamiki mpaka leo lakini hebu tuone vyanzo muhimu vya ugumba.

Utoaji wa mimba.

Huenda hichi ndio kitakua chanzo kikuu cha ugumba miaka ijayo kwani siku hizi kila karibia kila mwanamke ana sababu za kutoa mimba, utoaji wa mimba una hatari nyingi ambazo huweza kuleta ugumba kama kuoza au kuharibika kwa kizazi baada ya kushambuliwa na bakteria, makovu yanayoletwa na vifaa vinavyotumika kutoa mimba kwenye mfuko wa uzazi na mlango wa uzazi huweza kusababisha ugumba usiotibika.

Matatizo ya mirija ya uzazi.

Ovari zimeunganishwa kwenye mirija ambayo hupitisha mayai kwenda kwenye mfuko wa uzazi..wakati mwingine mirija hiyo huziba kwa sababu mbalimbali hivyo mayai hushindwa kupita na kusababisha ugumba.mfano ugonjwa wa endometriosis, upasuaji na peritonitis.

Matatizo ya kizazi.

Kizazi ndio sehemu kuu ambayo mtoto hutunzwa na kuishi kwa miezi yote tisa, tatizo lolote linaloshambulia kizazi huleta ugumba. mfano, makovu ndani ya kizazi, uvimbe ndani ya kizazi, kugeuka kwa kizazi na magonjwa ya zinaa kama kaswende na kadhalika.

Kansa ya kizazi.

Kansa ya kizazi huzuia yai la mama lililorutubishwa kushindwa kujiweka kwenye kizazi ili kukua, hivyo huchangia sana mimba kuharibika au kutotungwa kabisa.

Matatizo ya mlango wa uzazi.

Oparesheni za kizazi, utoaji wa mimba na magonjwa ya zinaa huweza kusababisha kuziba kwa mlango wa uzazi hivyo mbegu za kiume kushindwa kabisa kupita kwenye mlango wa uzazi na kusababisha ugumba.

Matatizo ya vizaalishaji vya mayai [ovari].

Ovari ni kiungo ambacho kinatoa yai moja kila mwezi ili liweze kurutubishwa na mbegu ya mwanaume lakini kuna magonjwa ambayo yanaweza kusababisha ovari hiyo ikaugua na kushindwa kutoa mayai, mwanamke ana ovari mbili lakini moja ikiuugua tu na nyingine haifanyi kazi mfano ugonjwa wa ovarian cyst.

Magonjwa mengine ya mwili.

Magonjwa yeyote ya binadamu ambayo huingilia mfumo wa homoni za uzazi huleta ugumba mfano magonjwa ya ini,kisukari, hyperthyrodism, na kadhalika.

Matumizi ya sigara na pombe.

Uunywaji wa pombe sana na uvutaji wa bangi huzuia yai kutoka kwenye ovari, lakini pia uvutaji wa sigara hupunguza uwezo wa yai kutembea kutoka kwenye ovari kwenda kwenye mfuko wa uzazi na wakati mwingine husababisha mimba kutunga nje ya kizazi.

Msongo mkubwa wa mawazo.

Ukiwa unatafuta mtoto tayari ukiwa umepaniki kwamba huenda usimpate husababisha inasababisha mwili kutoa homoni kitaalamu kama cortisol ambazo huzuia kazi za homoni za uzazi kitaalamu kama gonadotrophin releasing hormone hivyo hali huzidi kua mbaya.

Uzito uliopitiliza.

mwili mkubwa unaingilia mfumo wa utengenezaji homoni za uzazi hivyo huweza kuleta ugumba katika umri mdogo sana, hivyo kupunguza uzito ni moja ya njia bora kabisa ya kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuzuia ugumba.

Kumbuka; kabla hujaanza kuzunguka kwa waganga wa kienyeji na mahospitalini ni bora kujichunguza kama uko kwenye hatari zilizotajwa hapo juu. hakuna dawa moja ambayo ina uwezo wa kutibu ugumba kwa watu wote bila kutibu chanzo chake kwanza…. hivyo naweza kusema kila mtu ana dawa yake ya ugumba kulingana na historia ya maisha yake na chanzo cha tatizo lake.

Ugumba unaweza kupona kabisa kulingana na chanzo cha tatizo na hali ya ugonjwa ilivyo na unaweza usipone kabisa kama ugonjwa umeshapea sana, ndio maana kuna watu wenye uwezo mkubwa sana wa kifedha, wasanii na wafanyabishara wakubwa lakini wameshindwa kupata watoto pamoja na kwenda mpaka nje ya nchi na kuonana na madaktari bingwa kwenye hospitali za kisasa kabisa.makala ijayo ntaongelea matibabu ya ugumba kwa kina, usikae mbali.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Faida ya kunywa maji yenye limao au ndimu kila siku

Faida ya kunywa maji yenye limao au ndimu kila siku

Watalam mbalimbali wa afya wanasema ya kwamba kwa kila siku ni vyema... Read More

Faida za mnyonyo na mazao yake

Faida za mnyonyo na mazao yake

Nyonyo Mbarika (Castor)
Mnyony(KiSwahili) Erand (KiHindi) Kastorka(KiRusi) ni mmea wa jamii ... Read More

Matumizi ya karoti na asali kutibu presha ya kushuka

Matumizi ya karoti na asali kutibu presha ya kushuka

Hatua za kufuata

1. Tengeneza glasi moja ya juisi ya karoti

2. ... Read More

Mchanganyiko wa asali na mdalasini una faida hizi

Mchanganyiko wa asali na mdalasini una faida hizi

Mchanganyiko wa mdalasini na asali unasaidia katika mambo ya aiana tofauti tofauti kama ifutavto:... Read More

Jinsi ya kuongeza wingi wa mbegu za kiume

Jinsi ya kuongeza wingi wa mbegu za kiume

Ili kuongeza mbegu za kiume zingatia haya yafuatayo;

Kula lishe bora

Chakula unacho... Read More

Faida 25 za kutembea kwa Miguu

Faida 25 za kutembea kwa Miguu

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili mfumo wa maisha ya watu pamoja na kuathiri afya zao kw... Read More
Sababu ya tatizo la Tumbo kujaa gesi na jinsi ya kujitibu

Sababu ya tatizo la Tumbo kujaa gesi na jinsi ya kujitibu

Tatizo la tumbo kujaa gesi husababishwa na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula ... Read More
Mambo ya Muhimu kufahamu kuhusu tatizo la mgongo wazi

Mambo ya Muhimu kufahamu kuhusu tatizo la mgongo wazi

Uti wa mgongo ulio wazi( Spinal bifida) ni hali ambayo mtoto anazaliwa nayo huku uti wa mgongo (m... Read More

Athari za Moshi wa sigara kwa mtoto

Athari za Moshi wa sigara kwa mtoto

Utafiti uliofanyika nchini Marekani umebaini kwamba watu wazima wasiovuta sigara lakini walipokuw... Read More

Vyakula vinavyoongoza kuongeza akili kwenye ubongo

Vyakula vinavyoongoza kuongeza akili kwenye ubongo

BILA shaka ubongo ni miongoni mwa viungo muhimu vya binadamu lakini ni watu wachache sana wanaout... Read More

Mambo muhimu kujua Kuhusu Uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke

Mambo muhimu kujua Kuhusu Uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke

Naamini umeshawahi kusikia kuhusu changamoto ya uvimbe kwenye kizazi kwa Wanawake yaani Fibroids.... Read More

Njia za kutibu shinikizo la chini la damu au presha ya kushuka

Njia za kutibu shinikizo la chini la damu au presha ya kushuka

👉Kutibu shinikizo la chini la damu kwa kutumia maji chum... Read More