Sababu ya tatizo la Tumbo kujaa gesi na jinsi ya kujitibu
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Tatizo la tumbo kujaa gesi husababishwa na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula mbalimbali tunavokula ambayo hujaa tumboni na kwenye utumbo mdogo. Hali hii husababisha tumbo kujaa au kuvimba na mtu hutoa gesi hiyo kwa njia ya ushuzi na kubeua.
Nini husababisha.
Tatizo ili mara nyingi husababishwa na huambatana na mambo yafuatayo:
1. Kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo huchelewesha tumbo kufunguka kwa ajili ya usagaji wa chakula.
2. Kunywa vinywaji vyenye Carbonates, cola na kula vyakula vyenye gesi kama maharage, bigiji, vitunguu, kabichi n.k
3. Msongo wa mawazo na hasira.
4. Kula haraka haraka na kula unaongea.
5. Uvutaji wa Sigara
6. Magonjwa na maambukizi katika mfumo wa chakula asa kwenye tumbo na utumbo ambayo huzuia kusagwa na kufyonzwa kwa chakula.
Jinsi ya kujitibu.
· Kunywa chai ya tangawizi au karafuu itasaidia kupunguza gesi.
· Unaweza kunywa glasi moja ya juisi ya Limao baada ya kula.
· Tafuna mbegu za maboga zinasaidia kulainisha mfumo wa chakula
· Lalia ubavu wa kushoto na pumua kwa kasi ili kupunguza gesi tumboni.
· Kunja miguu na ikalie uku ukinyoosha mikono na kuinamia mbele itasaidia.
· kuongeza kasi ya mfumo wa chakula kufanya kazi na kuondoa gesi.
· Fanya mazoezi mepesi ya kutembea na kuruka ruka.
· Kula na tafuna chakula taratibu na epuka vyakula vyenye gesi na mafuta mengi,.
· Nenda hospitali kama tatizo ili linaambatana na kuharisha, kutapika, maumivu makali ya tumbo, kinyesi chenye rangi tofauti au damu na maumivu ya kifua.
Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.
Related Posts
Kutumia mtindi na asali ni moja ya dawa rahisi zaidi za kutibu chunusi.
Unahitaji:
...
Read More
Mwanamke anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wak...
Read More
Mwili wa binadamu umeundwa kwa organs na mifumo mbalimbali ili kuuwezesha kufanya kazi sawia. Mfa...
Read More
Watu wengi hulitumia tunda la papai kwa sababu ya utamu wake. Hata hivyo mbali na kuwa na ladha n...
Read More
Siki ya tufaa (Apple cider vinegar) ni moja kati ya dawa zinazojulikana katika kutibu chunusi ahs...
Read More
Mara nyingi watu wanaugua maradhi mbalimbali, lakini wengi wao hawapendi kwenda hospitali kufanya...
Read More
Kuwa na harufu mbaya mdomoni ni kitendo kinachoweza kuathiri maisha ya mtu kimahusiano si kwa mpe...
Read More
☘☘piga chini kitambi☘☘
Mahitaji
🌹Tikiti🍉 1
🌹Tangawizi kid...
Read More
Yafuatayo ni magonjwa na njia za kujitibu kwa kutumia matunda
KUTUBU KIUNGULIA
Aliy...
Read More
Korosho zina faida hizi zifuatazo;
1. Zinakinga Maradhi ya Saratani Haswa kwenye matumbo ma...
Read More
Kifua kikuu ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya bacteria na kuenezwa kwa njia ya hewa. Mtu mwen...
Read More
Dawa nyingine nzuri kwa ajili ya chunusi usoni na mwilini ni limau. Limau linajitokeza kwenye vya...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!