Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Mambo ya kufanya ili kupona majeraha mapema

Featured Image

Hakuna mtu anayependa kupata majeraha au kuchelewa kupona majeraha. Kwa kuwa uhai na uzima wetu haupo mikononi mwetu, ni vyema tukafahamu kuwa kuna wakati tunaweza kuumia.

Kwa kutambua hili karibu nikufahamishe mambo matano unayoweza kuyafanya ili kuharakisha kupona majeraha.

1. Kula vizuri

Lishe bora ni muhimu wakati wote, lakini ni muhimu zaidi mara unapokuwa na majeraha. Ili uweze kupona majeraha mapema unahitaji ule matunda na vyakula vyenye protini, vitamini C, B12 pamoja na madini ya chuma kwa wingi.

Vyakula na matunda hayo ni kama vile machungwa, mapapai, mayai, maziwa, samaki, maharage, n.k. Kwa kula vyakula hivi mwili utaweza kutibu majeraha kwa haraka zaidi.

2. Pumzika vya kutosha

Kupumzika ni njia ya kuupa mwili nafasi ya kujijenga na kujitibu wakati wa majeraha. Kutokana na mtindo wa maisha au changamoto za kiuchumi, baadhi ya watu hawapati muda wa kupumzika wapatapo majeraha.

Hivi leo utamkuta mtu akiendelea na shughuli zake huku akiwa na plasta, au bandeji bila hata kujali. Ili uweze kupona mapema unahitaji kuupumzisha mwili kwa kiasi cha kutosha ili upone vyema.

3. Fuata maelekezo

Kutokana na majeraha uliyoyapata daktari anaweza kukataza usile au sifanye kitu fulani lakini wewe hutaki; je unafikiri utaweza kupona mapema?

Watu wengi hukatazwa vitu kama vile pombe au kazi ngumu mara wapatapo majeraha, lakini ni wachache ndiyo wanaoheshimu hili.

Ni lazima ufuate ushauri wa daktari ikiwa unataka kupona mapema.

4. Kunywa maji mengi

Maji huchukua takriban asilimia 70 ya mwili wa binadamu. Kunywa maji mengi uwapo na majeraha kutakuwezesha kupona majeraha yako mapema.

Maji huboresha kinga mwili, huboresha misuli pamoja na viungio (joints) mbalimbali hivyo kukuwezesha kupona majeraha mapema.

5. Ogea maji ya baridi

Tafiti mbalimbali zilizofanywa zimeonyesha kuwa kuna manufaa makubwa ya kuogea maji ya baridi. Manufaa haya pia yapo kwa mtu aliyepata majeraha.

Kuogea maji ya baridi kutasababisha mzunguko mzuri wa damu, hivyo viini lishe na tiba vitasafirishwa vyema kwenda kuponya majeraha; pia maji baridi hupunguza maumivu ya vidonda au majeraha.

Kwa hakika lishe bora ni tiba ya maradhi takriban yote. Katika makala hii umeona jinsi lishe bora pamoja na kuzingatia kanuni chache za msingi za afya kunaweza kukusaidia kupona majeraha mapema.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya kujisaidia unapotokwa na damu Puani

Jinsi ya kujisaidia unapotokwa na damu Puani

Unapotokwa na damu puani fanya yafuatayo;
1. Simama wima na inamisha kichwa kwa mbele, kusim... Read More

Visababishi, dalili, matibabu na kinga ya presha ya kushuka

Visababishi, dalili, matibabu na kinga ya presha ya kushuka

Hypotension ndio jina linalotumika kuelezea presha ya kushuka ambayo mpaka sasa chanzo chake hakijaw... Read More
Tabia 10 zinazoweza kuharibu figo

Tabia 10 zinazoweza kuharibu figo

1.Kubana mkojo kwa muda mrefu
2.Kutokunywa maji ya kutosha kila siku
3.Kutumia chumvi n... Read More

Sababu za magonjwa ya figo na jinsi ya kuondokana na janga la magonjwa ya Figo

Sababu za magonjwa ya figo na jinsi ya kuondokana na janga la magonjwa ya Figo

1.Usichelewe kwenda HAJA. Kutunza mkojo kweye kibofu chako kwa muda mrefu ni wazo ... Read More
Mambo muhimu kujua Kuhusu Uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke

Mambo muhimu kujua Kuhusu Uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke

Naamini umeshawahi kusikia kuhusu changamoto ya uvimbe kwenye kizazi kwa Wanawake yaani Fibroids.... Read More

Faida za kula karanga mbichi

Faida za kula karanga mbichi

Karanga ni muhimu sana katika afya ya mwili wa binadamu. Kiukweli karanga siyo chakula cha kupuuz... Read More

Mambo ya Muhimu kuyajua kuhusu maumivu ya Korodani

Mambo ya Muhimu kuyajua kuhusu maumivu ya Korodani

Kuna wakati mwanaume huweza kupata maumivu ya korodani, ambapo inawezekana ikawa ni maumivu kwa k... Read More

Madhara ya kubana mkojo muda mrefu

Madhara ya kubana mkojo muda mrefu

Utakubaliana na mimi kwamba, kitendo cha mtu kubanwa na haja ndogo siyo kitu cha hiyari kwamba sa... Read More

Mchanganyiko wa asali na mdalasini una faida hizi

Mchanganyiko wa asali na mdalasini una faida hizi

Mchanganyiko wa mdalasini na asali unasaidia katika mambo ya aiana tofauti tofauti kama ifutavto:... Read More

Matumizi ya mbaazi kama dawa

Matumizi ya mbaazi kama dawa

Mbaazi ni zao la chakula ambalo linalimwa sehemu nyingi sana hapa nchini, zao hili pia linaweza k... Read More

Vyakula vya kukusaidia kupunguza uzito

Vyakula vya kukusaidia kupunguza uzito

Kuchagua vyakula sahihi kwa mlo wako inaweza kuwa changamoto na tungependa kuamini kwamba kupungua u... Read More
Namna ya kuondokana na tatizo la kunuka Kikwapa

Namna ya kuondokana na tatizo la kunuka Kikwapa

Harafu ya jasho inakera, kibaya zaidi ni kuwa wewe mwenyewe husikii harufu hiyo ila wale walio ka... Read More