Updated at: 2024-05-25 18:09:37 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?
MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee. MALAIKA: Kwa nini? MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni. Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?
Angalia wanachokifanya Zuzu na msichana chumbani kwenye giza
Zuzu: Mambo Anna! Anna: Poa! Zuzu: Kuna kitu nataka nikuonyesheβ¦ Anna: Kitu gan? Zuzu: Twende chumbani kwako (wakaenda) Anna: Haya nionyesheβ¦
Updated at: 2024-05-25 18:07:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Zuzu: Mambo Anna! Anna: Poa! Zuzu: Kuna kitu nataka nikuonyesheβ¦ Anna: Kitu gan? Zuzu: Twende chumbani kwako (wakaenda) Anna: Haya nionyesheβ¦
Zuzu: Funga mlango na madirisha kwanza (akafunga) Anna: Haya nionyeshe sasa!.. Zuzu: Zima taa kwanza (akazima) Anna: Mhmβ¦nionyeshe sasa! Zuzu: Haya njoo hapa kitandaniβ¦ Anna: Ok, nionyeshe! Zuzu: Ona nimenunua saa ambayo inawaka yenyewe gizaniβ¦ Acha mawazo mabaya ww???
MLEVI; "Nakunywa bia tano! MCHUNGAJI; "Bia moja bei gani!? MLEVU; "2500/ MCHUNGAJI; "Ulianza lini kunywa bia!? MLEVI; "Miaka 18 iliyopita!
MCHUNGAJI; "Kwa hiyo kwa siku unatumia zaidi ya 10,000?? MLEVI; "Ndio! MCHUNGAJI; "Kama u gekuwa unatunza hiyo pesa 10,000 kwa siku leo hii si ungekuwa na Range Rover!? MLEVI; "Samahani, naweza kukuuliza swali!? MCHUNGAJI; "Uliza! MLEVI; "Unakunywa bia!? MCHUNGAJI; "Hapana! MLEVI; "Nionyeshe Range Rover yako! MCHUNGAJI; "akasepa"
Alichokisema mwizi baada ya kushinda bahati nasibu
Updated at: 2024-05-25 17:06:08 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hapa mtaani kuna mwizi sugu ameshinda mil.10 za bahati nasibu ??. Alipoulizwa atafanya nini na hela nyingi hizo Akasema anataka kupanua shughuli zake. Mimi sijamuelewa na sasa hivi watu wameanza kuhama mtaaβ¦ ππ
Updated at: 2024-05-25 16:55:49 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ukioa mke asiyesoma hata hili unaweza kufanya
KUOA MKE AMBAE HAJASOMA RAHA SANA LEO NIMEMUAMBIA MWEZI HUU HATUTOLIPWA MSHAHARA KWAKUA HAUNA TR 30 KAENDA KUNGALIA KARENDA KARUDI ANANIAMBIA HAMNA SHIDA MME WANGU TUTAVUMILIA TU