Updated at: 2024-05-25 16:24:29 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wasichana na wanawake wanaweza kulewa kwa ujumla. Mara nyingi, hulewa pombe haraka kuliko wanaume. Hii inatokana na uzito mdogo wa miili yao, na kiasi cha mafuta na maji katika miili yao. Kilevi husambaa kiasi kikubwa katika miili ya wanawake. Maini yao huharibika kirahisi zaidi kuliko maini ya wanaume.
Kutokana na kilevi, wanawake au wasichana huwa wepesi kufanya vitu ambavyo wasingefanya kama wasingelewa. Wanaume hutumia nafasi hii kuwashawishi kufanya mapenzi bila kuchukua tahadhari yoyote kama vile kutumia kondomu ili kupunguza maambukizo ya VVU.
Updated at: 2024-05-25 16:24:05 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Haki za binadamu ni haki zinazohusiana na mambo ya msingi na
asili ya uhuru na heshima ya ubinadamu ambapo watu wote wamepewa
haki ya kupata heshima kama
binadamu. Mara mtu azaliwapo
mume au mke hupata
haki hizi. Haki hizi
zinatambuliwa kimataifa
na zina usawa kwa watu
wote. Nchi mbalimbali
zimetia saini na kuidhinisha
haki hizi za kimataifa
na kufanya ni sehemu
ya sheria zao
pamoja na kuweka sera
zinazolinda haki hizi.
Haki za uzazi zina misingi yake katika haki za binadamu na pia
zinahusiana na haki za mtu mmojammoja.
Kupata habari juu ya ujinsia na mada zinazohusu afya
ya uzazi.
Mwanamke au mwanaume kuamua kwa uhuru na
kuwajibika, kama unataka kujamiaana lini na nani.
Uhuru wa maamuzi.
Kuamua kwa hiari na kuwajibika juu ya idadi na muda wa
kupishana katika kupata watoto.
Kupata huduma za afya ya uzazi kwa urahisi.
Haki za kufanya maamuzi kuhusu afya ya uzazi, kwa
uhuru, bila kunyanyaswa, kulazimishwa, bila kutumia
nguvu pamoja na maamuzi nani wa kufunga naye ndoa.
Kujilinda kutokana na mila zenye madhara kama vile
ukeketaji wa wanawake.
Haki hizi zimerekebishwa tangu mkutano uliofanyika Cairo mwaka
19941.
Kwa nini nao watu wanaishi kwenye ndoa wanapata maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI?
Updated at: 2024-05-25 16:22:29 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna sababu kuu mbili i kwa wana ndoa kupata maambukizi i ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Kwanza, i inawezekana kuwa mmoja kati yao alikuwa tayari na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kabla ya siku ya kuoana. Kwani hata mtu aliyeambukizwa na Virusi vya UKIMWI anaweza kuonekana mwenye afya nzuri i na kuwa navyo mwilini siku ya harusi. Hii ni pale ambapo awali alifanya ngono na mtu aliyeambukizwa Virusi i ama alivipata kwa kupitia njia nyingine kwa mfano, njia ya damu i siyo salama.. Kama mtu aliwahi kufanya ngono kabla, njia pekee ya kuhakikisha kuwa hana virusi kabla ya kufunga ndoa ni kwenda kupima damu. Pili, wanandoa hao wanaweza kuambukizwa baada ya kufunga ndoa, pale ambapo mwenzi mmoja atafanya mapenzi na mtu mwingine. Kama mmoja wao au wote wawili watafanya ngono na mpenzi mwingine (mahusiano nje ya ndoa) wanaweza kupata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
Watu wanaoishi na ulemavu wanapewa huduma za upasuaji hasa wakati wa kujifungua?
Updated at: 2024-05-25 16:24:07 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Upasuaji unafanyika kwa wanawake wote ambao wamegundulika kuwa na tatizo la kujifungua kwa njia ya kawaida. Hii inafanyika bila kujali hali yao kwa maana kwa watu wenye ulemavu na wasio na ulemavu. Kila mwanamke atapata huduma hiyo kama itakuwepo sehemu anapoishi. Tatizo lililopo hapa Tanzania kwa sasa hivi hasa sehemu zilizojitenga ni umbali wa kufikia huduma hii. Umbali huu unamfanya mama aliyeanza uchungu wa kujifungua kushindwa kuweza kufika kwa muda unaotakiwa.
Updated at: 2024-05-25 16:22:00 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ndoto nyevu ni kitu kinachowatokea vijana wakiwa usingizini. Haiwezekani kuzuiwa kwa sababu uko usingizini, lakini labda ingekuwa vizuri wewe kujiuliza kwa nini unataka kuzuia jambo hili, haswa ukizingatia kwamba ndoto nyevu hazidhuru afya yako kabisa na kwamba ni dalili kuwa sasa unakuwa mtu mzima, yaani mwanaume.
Kwa nini Albino wanawekwa katika kundi la watu wenye ulemavu?
Updated at: 2024-05-25 16:24:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ulemavu maana yake ni hitilafu katika mwili au akili inayomwekea mipaka mtu asiweze kufanikisha shughuli fulani katika maisha yake. Albino wanatambuliwa kama watu wenye ulemavu Tanzania hasa kwa ajili ya uwezo wao wa kutokuweza kuona vizuri. Dalili za kutokuwa na uwezo wa kuona hutofautiana kuanzia wale ambao hawaoni karibu, wasioweza kuona mbali na wale ambao wanashindwa kuona vizuri au kuona mawingumawingu.
Je, ni kweli kuwa madhara ya uvutaji moshi wa sigara yako ni kidogo kuliko yale yatokananyo na kuvuta moshi kutoka kwa mvutaji?
Updated at: 2024-05-25 16:24:26 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Uvutaji wa aina zote una madhara. Kama utavuta sigara na kuvuta moshi kwa kutumia mdomo hadi kwenye mapafu yako utapata madhara moja kwa moja kwenye viungo vyako. Kama nitasimama karibu na mvutaji na kuvuta moshi, kuna madhara ambayo siyo ya moja kwa moja. Kwa upande mwingine kama jirani wa mvutaji unaweza kuvuta sumu nyingi itokanayo na tumbaku kwa sababu hakuna kitu cha kuichuja. Sigara za viwandani zina kishungi ambacho huchuja tindikali mbalimbali zenye sumu, kama vile kaboni na asidi ya magamba ya miti, ambazo zina madhara kwa mapafu.
Matatizo yanayotokana na ujauzito katika umri mdogo
Updated at: 2024-05-25 16:22:21 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wataalamu wanashauri kwamba msichana anastahili kuanza kubeba mimba kuanzia umri wa miaka 18 hadi 20. Kabla ya umri huu, mwili wa msichana bado haujakomaa vizuri. Viungo vya uzazi bado ni vidogo na ngozi ni laini. Vilevile mfupa wa nyonga bado mwembamba kiasi cha kumwezesha mtoto kupitia wakati wa kuzaliwa. Wasichana chini ya miaka 18 wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata matatizo, hasa wakati wa kujifungua. Matatizo hayo ni pamoja na mapigo ya moyo kuwa juu, kuumwa uchungu kwa muda mrefu, kukwama kwa mtoto, kujifungua kwa njia ya operesheni, kujifungua kabla ya wakati na watoto kuzaliwa na uzito mdogo. Mwili huwa na mahitaji makubwa wakati wa ujauzito na kujifungua na mwili wa wasichana wenye umri chini ya miaka 18 huwa haujakomaa vya kutosha kwa kazi ya kubeba mimba. Mbali ya shida za kiafya, kuna matatizo mengine yatokanayo na kupata mimba mapema. Mara nyingi msichana na mwenzie wanakuwa bado wanasoma shule, msichana hufukuzwa shule na hata hutengwa katika jamii . Vijana mara nyingi hawana mapato ya kumlea na kumtunza mtoto, na mahali pa kuishi huwa hawana. Vilevile mvulana mara nyingi hayuko tayari kuchukua jukumu la kuwa baba. Kwa sababu hizi zote, ni vizuri zaidi mimba zitungwe baada ya msichana kufikia umri wa miaka 18.
Updated at: 2024-05-25 16:24:28 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Watu wanokunywa kupitia kiasi huathiri jamii kwa njia
mbalimbali. Madhara mengine hutokea kwa kuwa wanafanya
vitu ambavyo wasingevifanya iwapo wasingekuwa wamelewa.
Watu wakilewa, huweza kuwa na hasira, wagomvi hivyo basi
huwadhuru wengi kiakili na kimwili. Isitoshe, ajali nyingi za
kazini na barabarani hutokea watu wakiwa wamelewa. Mara
nyingi watu wasiokuwa na hatia na vilema hupoteza maisha yao
kutokana na ajali zinazohusiana na ulevi.
Watu wanaokunywa
pombe kupita kiasi hupunguza uangalifu na hivyo basi kuchangia
katika kuenea kwa VVU kwenye jamii. Watu wanaokunywa pombe
wanaweza pia kufanya ujambazi katika jamii. Pia wanaokunywa
kupita kiasi si wafanyakazi wa kutegemewa kwani hutumia
muda mwingi nje ya sehemu zao za kazi.
Watu waliozoea kunywa pombe nyingi hupoteza pesa zao nyingi
kununua pombe na muda wao mwingi kufikiria jinsi ya kupata
pesa za kunywea pombe.
Kutokana na gharama za kununua
pombe familia zao hukosa pesa za vitu muhimu kama kodi ya
nyumba, ada na sare za shule na chakula.
Vijana wanaokunywa pombe huanza kuiba pesa nyumbani kwao
ili kununulia pombe. Matumizi mabaya ya pombe mara nyingi
husababisha matatizo au kuvunjika kwa familia, au urafiki.
Vilevile husababisha matokeo mabaya shuleni au kuacha kabisa
shule, hali ambayo inaweza kusababisha kukosa nafasi za kazi,
kujitegemea wewe mwenyewe na kusaidia famila yako na jamii.
Updated at: 2024-05-25 16:24:01 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ubakaji ni tendo la kutumia nguvu katika ngono ambapo mbakaji anatumia nguvu kuonyesha ubabe wake. Ubakaji ni kosa la jinai i na huadhibiwa kisheria. Kama mtu hayuko tayari kufanya ngono na analazimishwa kukubali kufanya hivyo hii , i inahesabiwa kama ubakaji, hata kama anayekulazimisha ni rafiki, ndugu, jirani, mume au mtu usiyefahamiana naye.