Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Je, kuna madhara gani ya kunywa pombe kwa vijana hasa kijana Albino?

Featured Image

Athari za pombe kwa mtu anayeishi na ualbino ni sawa na zile
zinazowapata watu wengine.
Mtu akiwa katika hali ya ulevi anaweza kuzembea katika
kufanya uamuzi sahihi kwa mfano kuhatarisha maisha yake
kwa kuendesha baiskeli yake kimchoromchoro, kujamiiana
bila kuvaa kondomu na kadhalika. Mbali na hayo, watu wenye
matatizo ya kunywa pombe husahau kujiweka katika hali nzuri
kwa maana hawajali kula chakula. Tabia hii inamuweka katika
hatari ya kuandamwa na maradhi.
Pombe zinaweza pia kuingiliana na maisha/uhusiano wa kimwili.
Mwanzo kabisa pombe inaweza kukusisimua na kukufanya
mchangamfu (kutoona aibu), lakini kadiri unavyoendelea
kunywa unaanza kusinzia na kwa upande wa wanaume wengine,
uume kukosa nguvu. Unaweza kushawishika kutoa aibu uliyo
nayo kwa kunywa pombe lakini mara nyingi hii haileti mvuto
kutoka kwa wenzi wako.

Kunywa pombe pia kunaleta uharibifu wa kudumu kwenye ubongo
ambao unamfanya mtu kupata matatizo ya kumbukumbu.
Pombe imewekwa kwenye kundi la vilevi tegemezi. Mwili
ukishazoea pombe, ni rahisi sana watu kutumia pesa zote
kwa ajili ya pombe na kusahau kufanya mambo mengine
yatakayomletea maendeleo katika maisha yake.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, kuna dawa yoyote ya kutibu ugumba?

Je, kuna dawa yoyote ya kutibu ugumba?

Hakuna jibu la ujumla kwa swali hili, kwa sababu tiba ya ugumba inategemea chanzo maalum cha ugum... Read More

Nani anavalisha kondomu ya kiume, je ni mwanamke au mwanaume?

Nani anavalisha kondomu ya kiume, je ni mwanamke au mwanaume?

Katika kufanya mapenzi iwe mwanaume anayeweka kondomu uumeni au iwe mwanamke anayeshugulika kuwek... Read More

Je, ni njia gani zinaweza kuleta hisia za kihisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, ni njia gani zinaweza kuleta hisia za kihisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, ni njia gani zinaweza kuleta hisia za kihisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi? Swali hili lin... Read More

Magonjwa yatokanayo na sigara

Magonjwa yatokanayo na sigara

Kuna matatizo na magonjwa mengi na ya aina mbalimbali
unayoweza kuyapata kutokana na utuvaji... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Tarehe ya Kimapenzi na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Tarehe ya Kimapenzi na Msichana

Kama wewe ni miongoni mwa wanaume wanaotaka kuwa na tarehe ya kimapenzi na msichana, kuna vidokez... Read More

Jinsi ya Kusimamia Uchungu wa Kupendwa na Msichana

Jinsi ya Kusimamia Uchungu wa Kupendwa na Msichana

Jinsi ya Kusimamia Uchungu wa Kupendwa na Msichana

Kupendwa na msichana ni jambo la kufura... Read More

Inakuwaje, baadhi ya Albino wana macho yanayochezacheza?

Inakuwaje, baadhi ya Albino wana macho yanayochezacheza?

Wapo baadhi ya Albino wenye macho ya kuchezacheza na
ambayo hayawezi kulenga pamoja. Hii ina... Read More

Afya ya uzazi ni nini?

Afya ya uzazi ni nini?

Afya ya uzazi inahusiana na mfumo wa uzazi wa mtu, na via vya uzazi kwa watu. Kwa hali hiyo basi ina... Read More
Je, nini imani ya watu katika kutumia michezo ya ngono/kufanya mapenzi kama njia ya kuimarisha uhusiano wako?

Je, nini imani ya watu katika kutumia michezo ya ngono/kufanya mapenzi kama njia ya kuimarisha uhusiano wako?

  1. Je, ni sahihi kutumia michezo ya ngono/kufanya mapenzi kama njia ya kuimarisha uhusiano wak... Read More
Vidokezo vya Kuwa na Uhusiano Mzuri na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Uhusiano Mzuri na Msichana

Mara nyingi, wanaume wamekuwa wakipata wakati mgumu kuwa na uhusiano mzuri na msichana. Inawezeka... Read More

Kwa nini wanaume wengi hupenda kufanya mapenzi baada ya kulewa; na wasichana wengi hupatwa na vishawishi?

Kwa nini wanaume wengi hupenda kufanya mapenzi baada ya kulewa; na wasichana wengi hupatwa na vishawishi?

Pombe ina tabia ya kufanya ubongo kushindwa kufikiri, na
kushindwa kujizuia na vishawishi vy... Read More

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wako kuhusu Matumizi ya Kinga (Condom)

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wako kuhusu Matumizi ya Kinga (Condom)

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wako kuhusu Matumizi ya Kinga (Condom) 😊🌺

Karibu kweny... Read More