Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Je, kwa nini akina mama wajawazito hawatakiwi kunywa pombe?

Featured Image

Wanawake wajawazito ambao hunywa pombe au kuvuta sigara
wanahatarisha afya na maisha ya mtoto aliye tumboni. Mtoto aliye
tumboni hurutubishwa kupitia damu ya mama. Kama mama atavuta
sigara au kunywa pombe, sumu illiyopo katika sigara au pombe
inapoingia kwenye damu yake itamfikia mtoto pia. Pombe hushambulia
moyo uendeleao kukua na ubongo wa mtoto aliye tumboni.
Akina mama wanaokunywa kupita kiasi wakiwa wajawazito
wanaweza kupata watoto wenye magonjwa ya moyo au mtindio
wa akili, kwa sababu chembechembe za ubongo hazikui vizuri.
Mara nyingi watoto huzaliwa na upungufu katika mwonekano
wa sura. Kwa mtoto pombe ni sumu kali, hata kama ni kwa kiasi
kidogo, itamdhuru.

Mama anaekunywa pombe anaweza kuwa hajali au kusahau
kujilinda mwili wake na mtoto anayekua.
Kama akipata maambukizo ya VVU na mtoto pia anaweza
akapata virusi vya UKIMWI.
Wanawake wanaovuta sigara wakiwa wajawazito wana
uwezekano mkubwa wa kuzaa watoto ambao hufariki ghafla bila
sababu ya kueleweka katika mwaka wao wa kwanza wa maisha.
Watoto wa akina mama wanaovuta sigara mara nyingi huzaliwa
na umbo dogo kuliko wengine kwa sababu watoto walipata
chakula kidogo walipokuwa bado tumboni mwa mama zao.
Ujumbe upo wazi: Wanawake wanaotaka watoto wenye afya
wasivute kabisa sigara wala kunywa pombe wakiwa wajawazito.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kuwa na Furaha na Msichana Wako

Jinsi ya Kuwa na Furaha na Msichana Wako

Jinsi ya Kuwa na Furaha na Msichana Wako

Kuwepo kwa mtu ambaye unampenda na kujali ni jamb... Read More

Mtu anaweza kurithi uvutaji wa bangi?

Mtu anaweza kurithi uvutaji wa bangi?

Hapana, huwezi ukarithi uvutaji wa bangi. Lakini mara nyingi watoto huiga tabia za wazazi wao. Wa... Read More

Je, nikiambukizwa virusi vya UKIMWI na UKIMWI nifanye nini?

Je, nikiambukizwa virusi vya UKIMWI na UKIMWI nifanye nini?

Jambo la msingi ni kutokukata tamaa na kuwa na matumaini. Mara nyingine i inasaidia kama utakuwa ... Read More

Madhara yanayotokea kwa unyanyasaji wa jinsia kwa mtu

Madhara yanayotokea kwa unyanyasaji wa jinsia kwa mtu

Unyanyasaji wa ujinsia una matatizo mabaya ya kimwili na
yanayochukua muda mrefu kwa mwathir... Read More

Njia Rahisi za Kufanya Msichana Awe na Hamu ya Kuwa na Wewe

Njia Rahisi za Kufanya Msichana Awe na Hamu ya Kuwa na Wewe

Wapenzi, kama unapenda msichana fulani na unataka kuwa na uhusiano naye, inaweza kuwa ngumu kumsh... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Uaminifu katika Uhusiano wako na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Uaminifu katika Uhusiano wako na Msichana

Uaminifu ni tabia muhimu sana katika uhusiano wako na msichana. Kama unataka uhusiano wako ufanye... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Mawasiliano ya Kuaminika na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Mawasiliano ya Kuaminika na Msichana

Leo kwenye makala hii, tutazungumzia vidokezo vya kuwa na mawasiliano ya kuaminika na msichana. N... Read More

Kujikinga na Maambukizi ya UKIMWI: Njia za Kuepuka Hatari

Kujikinga na Maambukizi ya UKIMWI: Njia za Kuepuka Hatari

Kujikinga na Maambukizi ya UKIMWI: Njia za Kuepuka Hatari

  1. Jambo zuri ni kuwa na ... Read More

Je, inawezekana kujisikia huru kuelezea tamaa zako za ngono/kufanya mapenzi kwa mwenza wako?

Je, inawezekana kujisikia huru kuelezea tamaa zako za ngono/kufanya mapenzi kwa mwenza wako?

Karibu kwenye makala hii kuhusu swali la iwapo inawezekana kujisikia huru kuelezea tamaa zako za ... Read More

Nifanye nini ili kujua kama nina au sina maambukizi ya Virusi vya UKIMWI?

Nifanye nini ili kujua kama nina au sina maambukizi ya Virusi vya UKIMWI?

Ipo njia moja ya kuhakikisha kama umeambukizwa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI au hapana. Njia hii ni... Read More

Utoaji wa zawadi kwa kubadilishana na kujamiiana

Utoaji wa zawadi kwa kubadilishana na kujamiiana

Kutoa zawadi kwa mtu kwa kubadilishana ili kujamiiana
ni unyanyasaji mbaya. Iwapo mpokeaji w... Read More

Nini kinatokea wakati Virusi vya UKIMWI (VVU) vinapoingia mwilini na vinakwenda wapi katika sehemu ya mwili?

Nini kinatokea wakati Virusi vya UKIMWI (VVU) vinapoingia mwilini na vinakwenda wapi katika sehemu ya mwili?

Virusi hivi vinakaa katika chembechembe nyeupe zilizopo kwenye majimaji ya mwili i wa binadamu ha... Read More