Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

ATHARI ZA ULEVI KATIKA JAMII

Featured Image
Watu wanokunywa kupitia kiasi huathiri jamii kwa njia
mbalimbali. Madhara mengine hutokea kwa kuwa wanafanya
vitu ambavyo wasingevifanya iwapo wasingekuwa wamelewa.

Watu wakilewa, huweza kuwa na hasira, wagomvi hivyo basi
huwadhuru wengi kiakili na kimwili. Isitoshe, ajali nyingi za
kazini na barabarani hutokea watu wakiwa wamelewa. Mara
nyingi watu wasiokuwa na hatia na vilema hupoteza maisha yao
kutokana na ajali zinazohusiana na ulevi.

Watu wanaokunywa
pombe kupita kiasi hupunguza uangalifu na hivyo basi kuchangia
katika kuenea kwa VVU kwenye jamii. Watu wanaokunywa pombe
wanaweza pia kufanya ujambazi katika jamii. Pia wanaokunywa
kupita kiasi si wafanyakazi wa kutegemewa kwani hutumia
muda mwingi nje ya sehemu zao za kazi.

Watu waliozoea kunywa pombe nyingi hupoteza pesa zao nyingi
kununua pombe na muda wao mwingi kufikiria jinsi ya kupata
pesa za kunywea pombe.

Kutokana na gharama za kununua
pombe familia zao hukosa pesa za vitu muhimu kama kodi ya
nyumba, ada na sare za shule na chakula.

Vijana wanaokunywa pombe huanza kuiba pesa nyumbani kwao
ili kununulia pombe. Matumizi mabaya ya pombe mara nyingi
husababisha matatizo au kuvunjika kwa familia, au urafiki.

Vilevile husababisha matokeo mabaya shuleni au kuacha kabisa
shule, hali ambayo inaweza kusababisha kukosa nafasi za kazi,
kujitegemea wewe mwenyewe na kusaidia famila yako na jamii.
AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, nini kitatokea iwapo mwanamke atatumia dawa za kulevya wakati wa ujauzito?

Je, nini kitatokea iwapo mwanamke atatumia dawa za kulevya wakati wa ujauzito?

Kama mama mjamzito atatumia dawa za kulevya basi humuathiri mtoto moja kwa moja. Mtoto aliye tumb... Read More

Vidokezo vya Kutafuta Tarehe ya Muda Mrefu na Msichana

Vidokezo vya Kutafuta Tarehe ya Muda Mrefu na Msichana

Leo hii tutazungumzia kuhusu masuala ya kutafuta tarehe ya muda mrefu na msichana. Inawezekana um... Read More

Vidokezo vya Kufanya Msichana Aonekuwa Muhimu katika Maisha Yako

Vidokezo vya Kufanya Msichana Aonekuwa Muhimu katika Maisha Yako

Mwanamke ni hazina kubwa katika maisha ya kila mwanaume. Ni kiumbe chenye thamani, cha thabiti na... Read More

Jinsi ya Kutambua Ishara za Kuwa Tayari kwa Ngono

Jinsi ya Kutambua Ishara za Kuwa Tayari kwa Ngono

Jinsi ya Kutambua Ishara za Kuwa Tayari kwa Ngono 😊

Karibu kijana, leo tutaongelea jamb... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Kina na Msichana

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Kina na Msichana

Wanaume wengi huwa na shida katika kuongea na wanawake, hasa katika mazungumzo ya kina. Hii mara ... Read More

Kwa nini wasichana wakiingia utu uzima damu zinaanza kutoka kwenye uke?

Kwa nini wasichana wakiingia utu uzima damu zinaanza kutoka kwenye uke?

Kutoka damu (hedhi) kwa mara ya kwanza kunaitwa kuvunja ungo na hii ni dalili ya mtoto wa kike kuing... Read More
Vidokezo vya Kuweka Uhusiano wako na Msichana Hai

Vidokezo vya Kuweka Uhusiano wako na Msichana Hai

Mapenzi ni kitu muhimu sana katika maisha ya kila mwanadamu, na kwamba uhusiano wa kimapenzi ni s... Read More

Je, Uvutaji wa sigara unafurahisha na kuchangamsha?

Je, Uvutaji wa sigara unafurahisha na kuchangamsha?

Ndiyo, lakini ni mwanzo tu na kwa muda mfupi; hii ni kwa
sababu mwanzoni nikotini iliyomo ka... Read More

Vidokezo vya Kujenga Urafiki Mzuri na Msichana Kabla ya Kuanza Uhusiano

Vidokezo vya Kujenga Urafiki Mzuri na Msichana Kabla ya Kuanza Uhusiano

Urafiki mzuri ni msingi muhimu wa kuanza uhusiano wa kimapenzi. Kujenga urafiki mzuri na msichana... Read More

Jinsi ya Kuwa na Ukaribu wa Kihisia na Msichana

Jinsi ya Kuwa na Ukaribu wa Kihisia na Msichana

Kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na msichana ni jambo zuri sana. Hata hivyo, kuwa na ukaribu wa ... Read More

Ni asilimia ipi ya Watanzani ambao wameambukizwa na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Ni asilimia ipi ya Watanzani ambao wameambukizwa na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Nchini Tanzania ni 7% ya watu wenye umri kati ya miaka 15-49 wana maambukizi ya Virusi vya UKIMWI... Read More

Kwa nini watu wengine hupenda kujamiiana na watu wa jinsi sawasawa? mapenzi ya jinsia moja

Kwa nini watu wengine hupenda kujamiiana na watu wa jinsi sawasawa? mapenzi ya jinsia moja

Ni vigumu kutoa jibu kamili kwa nini hisia hii i ii inatokea kwa watu wengine, kwa sababu wataala... Read More