Cheki huyu mwanamke anavyomkomoa mme wake baada ya kumsaliti
Updated at: 2024-05-25 17:16:59 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MKE: Mbona unanukia pafyumu ya kike? MUME: Yaa kuna mwanamke tulikuwa tumeminyana ndani ya daladala MKE: Na lipstiki kwenye shati? MUME: Tulikumbatiana na wageni toka Zambia walitembelea ofisi yetu MKE: Na ile kondom iliyotumika kwenye mfuko wa suruali? MUME: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi MKE: Lazima niulize mie huwa nahakikisha nimeacha kila kitu hukohuko ndio narudi nyumbani MUME: Umesema nini wewe? MKE: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi. 😄😄
Huyu mchungaji ni noma, cheki alichomwambia pedeshe
Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki; MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu atakubariki zaidi
Updated at: 2024-05-25 18:06:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa
kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;
MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za
kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa
mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu
atakubariki zaidi
PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri
mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu,
huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya
kulevya.
MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia
kwa kujenga eneo la choo we toa tu!!!
Updated at: 2024-05-25 17:15:58 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Pale unapokuwa umefulia sana…
Mgeni anakutembelea Maskani kwako….Unaamua Kuchukua Ile Sh 600 iliyobaki na kwenda Dukani Kumnunulia Soda Unaondoka na Chupa Mbili Unanunua Fanta Moja kwaajil ya Mgeni na Ile Chupa ya Sprite Unaijaza Maji ili Ukirudi Uweze kumpa Kampani Mgeni……Unafika Seblen Unampa Ile soda ya Fanta Mgeni anakuambia Fanta huwa situmii Nipe hiyo sprite …..Bwana….Bwana. …Bwana….Weee 😂😂😂😂😂😂😂😂
Updated at: 2024-05-25 18:09:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Misemo ya kina dada
walianza na halohalooo! Wakaja unalo babu weee! Ikafuata utajijuuu! Ikafupishwa utajiJJ! Mara ghafla kantangazeee! Haikukaa sana kansajiriii! Ikatoka nyingine nishiiiiida!
Updated at: 2024-05-25 17:06:20 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Umeenda kutembea ukweni kwako baada ya chakula chausiku unapewa chumba chakulala inapofika usiku unatakakutoka kwenda kujisaidi kwasababu taa zimezimwa unapamia vyombo vya chakula sebleni kipindi unajalibu kupapasa uviweke sawa mala taa inawashwa na mama mkwe anaona umeshika vyombo anakwambia, baba kama ukushiba ungesema
Updated at: 2024-05-25 17:02:59 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
JE WAJUA?
Sungura, panya na Jamii zao huwa na mwendo wa kukimbia na kuruka muda wote na umri wao wa kuishi ni miaka 15. Kobe ni mnyama mwenda pole, asiye na papara wala pilika, muda mwingi hujificha na kupumzika ndani ya jumba lake akikwepa maadui. Umri wa kuishi kobe hufikia hadi miaka 300. FUNZO: Mazoezi ni kiinimacho na uongo mtupu. Jipumzikie mwaya!!! 🏃🏾🏃🏿
Updated at: 2024-05-25 18:10:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kakubaliana vizuri na msichana fulani hivi kuwa aibuke gheto, mchizi kajipanga vizuri kabisa…. mara saa nne hivi mdada kasema hana nauli. Mshkaji kajikunja kamtumia Elfu tano maana mwenye shida alikuwa ni yeye…… Baada ya nusu saa yule dada akamtumia meseji. "Jamani mpenzi, kumbe baba hatoki nilijua atatoka… sorry bae sitaweza kuja kwa leo… sooo sorry!" Mshkaji jiii! hajajibu kitu…..
Baada ya muda kidogo meseji ikaingia katika simu ya binti, akajua mchizi kajibu. Mh! kutazama ni meseji kutoka Mpesa.
"CA90F0511 IMETHIBITISHWA Tshs 5000 ILIYOTUMWA KIMAKOSA KATIKA ACCOUNT YAKO IMETOLEWA SALIO LAKO NI Tshs 5"
Halafu ndo ikaingia meseji ya mshkaji. "BASI POA SIKU NYINGINE KAMA VIPI"
#dada wa watu mashavu yakamshuka… hakuamini kilichotokea…. yaani jamaa keshawapigia Voda na pesa fasta imezuiliwa……