Mme amemfuma fundi wa kitanda na mke wake, cheki walichokua wanafanya
Kuna mama mmoja ameolewa na wanapendana sana na mmeo. siku moja mme wake alisafiri kikazi (safari ya zaidi ya mwezi) nje ya mkoa. Siku mmeo anarudi, yule mama alimtafuta fundi seremala amrekebishie chaga za kitanda zilikuwa zimeharibika, kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya above +18
Updated at: 2024-05-25 18:14:06 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna mama mmoja ameolewa na wanapendana sana na mmeo. siku moja mme wake alisafiri kikazi (safari ya zaidi ya mwezi) nje ya mkoa. Siku mmeo anarudi, yule mama alimtafuta fundi seremala amrekebishie chaga za kitanda zilikuwa zimeharibika, kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya above +18.
Wakati fundi anaendelea na kazi kumbe mmeo huyu dada alishafika. hakutaka kumjulisha mkeo, kwa nia nzuri tu ya kumfanyia suprise, kwani alikuja na mazaga zaga kibao. Hiyo aliingia kwa kunyatia hadi kwenye mlango wa chumbani kwao. Ghafla akasikia mazungumzo ya mkeo na fundi ndani. Mazungumzo yalikuwaje? fuatilia hapa chini
Mama X: Fanya haraka mme wangu amekaribia Fundi: Nakaribia kumaliza, nisaidie kuchomeka vizuri upande wako (akikusudia chaga) Mama X: Mbona haiingii Fundi: Ingiza kwa upande upande Mama X: Sukuma kwa nguvu Fundi: Angalia usiumie Mama X: Hamna shida imeingia
Wakati jamaa akiendelea kusikiliza mlangoni, fundi akaweza godoro juu ya kitanda na mama x akajitupa kitandani kujaribu kama kimetengamaa. mara chaga akachomoka na kuanguaka chini. Nini kilifuata
Mama x: Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii iiiii(miguno) "my God, mbona hivi" Fundi : Pole sana Mama X: sasa? Fundi: Ngoja nichomeke tena Mama X: Yaan wewe, utaacha mme wangu afike hatujamaliza Fundi: Usijali namaliza sasa hivi
Baada ya dakika chache, fundi akamuaga mama na kumwambia tayari, sasa naona umefurahi. Kutoka tu mlangoni akakutana uso kwa uso na jamaa amekunja ndita kama matuta ya viatu. Gues what happened?
Kitu gani kitatokea kisia toa maoni yako kama ni ww ungefanyaje?
Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
"Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana."
Padri, "Endelea…"
Updated at: 2023-04-29 22:53:14 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani peke yake. Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama {confess} "Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana." Padri, "Endelea…"
"Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa kufungwa. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu,nikatoa bastola nikamuua….. Yesu atanisamehe?"
Padri: "Utasamehewa." "Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona kilichotokea akasema anapiga polisi simu. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye pia… Yesu atanisamehe hilo?" Padri: "Utasamehewa."
Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe?" Padri:"Utasamehewa."
"Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua? Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.
Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe na hilo?"
Kimyaa…. "Padri yesu atanisamehe?" kimya….
Jamaa akatazama kwenye confession booth padri hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.
Jamaa, "Sasa baba mbona umekimbia?" Padri kwa taabu akajibu, "Nilitazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu……."
Updated at: 2024-05-25 17:03:30 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Bosi wangu karudi safari yake kutoka serengeti..! Si akanitumia picha, lakini ilikuwa network yenyewe tabu.. kwahio picha haikufunguka na kwa vile niliona itachelewa kufunguka na ataona sikumjibu basi nami..
Nikampelekea msg nikamuandikia umependeza saana bosi mashaallah…!! sasa baada tu ya kumfika msg.. na huku picha ikafunguka kumbe picha ya Sokwe..!! Basi Kaniambia kesho niende ofsini kwake kuna barua yangu.. Nahisi hyo barua ina pesa, hapa cjalala, nmekosa usingizi kabisa,nawaza ninunulie nn hyo pesa.Na kesho asubuhi sa 12 asubuhi atanikuta ofisini kwake naisubiri barua, sipendagi ujinga mimi.
Updated at: 2024-05-25 17:54:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kama umesoma st Kayumba utakuwa una aidia na haya…
1.Unaenda shule umechelewa unakuta mwalim anakamata wachelewaj unaamua urudi nyumbani 2.unachukua kimbegu cha ubuyu unasugua sakafuni af unamuunguza mwenzio 3.mkiruhusiwa tu unakimbia unataka uwe wa kwanza kwenye njia yenu y kurudia nyumban 4.MTU akikukera unamfungia shule (mnapigana baada ya kufunga shule) 5.MTU akikunyima kitu chake unamwambia "Ahaa eeh utaona sa nne" 6.wadada wembamba ndo wanaongoza kwa kusuta wenzao 7.ukiibiwa daftar jipya unalia kuliko hata uliloandika 8.unajaza mapeni kwenye mkebe(compass) na mengine hayaandiki 9.vifaa vingine kwenye mkebe hujawahi hata kuvitumia mfano bikari labda utolee mwiba😂 10.hakuna habari nzur kama kuambiwa Leo hamna shule mwalim haupo 11.habari mbaya zaidi n kurud nyumban kutoka shule una njaa af unaambiwa chakula mgeni kaja tumempa 12.mtoto wa mwalim utamgundua tu kwanzia sweta begi na viatu vyake 13.usiombee umpige mtoto wa mwalim utataman uache shule 14.unatengeneza kifutio cha ndala af unatishia eti kinafuta hadi peni😂 15.ukaguzi na huna ufagio.. unaomba chelewa kwa watu af unaongeza kijiti katikati 16.siku ukienda na ufagio wanakagua maji, ukienda na naji wanakagua kuni au mbolea😆 😂 Dah shule zetu hizi kiboko!!
MZEE:"sasa huyu mgeni sijui alale wap?"
MKE:"saa hizi ni usiku akalale na Bebi."
jamaa akaona huyo Bebi pengne mtoto anakojoa kitandani au akalia asije msumbua usiku
Updated at: 2024-05-25 18:02:06 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MZEE:"sasa huyu mgeni sijui alale wap?"
MKE:"saa hizi ni usiku akalale na Bebi."
jamaa akaona huyo Bebi pengne mtoto anakojoa kitandani au akalia asije msumbua usiku
JAMAA:"msipate tabu mi ntalala hapa kwenye kochi" akalala
asubh wanakunywa chai akaibuka mrembo,jamaa akapigwa bumbuwazi almanusra ajimwagie chai.
BINTI:"Naitwa BEBI,we unaitwa nani?"
Jamaa akasema mimi naitwa Fara…..!
Updated at: 2024-05-25 17:48:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tukiwa kanisani mdada alikuwa amelala , akaamka akasikia Pastor anasema " SIMAMA" Yule dada akasimama akashangaaa kanisa zima linamtizima kwa mshangao akiwemo mumewe, akaangalia kanisa zima akashtuka kujiona yeye peke yake ndiye aliesimama Pastor akaendelea vizur endelea kusimama, tumepata mmoja hadi sasa aliyesimama narudia kwa mara ya mwisho kama hujasikia vizuri " kama wew umewahi kumsaliti au bado unasaliti ndoa yako SIMAMA" Binti akazimia