Njia zipi zinaweza kumletea mwanamke mshindo haraka, na zipi zinamletea mwanaume mshindo haraka? Njia za kufika kileleni
Updated at: 2024-05-25 16:22:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jambo la msingi kabisa ni kwamba wote wawili kuwa tayari kwa kujamii ana. Yaani kupendana na kujaliana sana, halafu kuwa tayari kwa tendo hilo kimwili, kimawazo na kiakili. Kutokuwa tayari kwa kufanya mapenzi, kwa mfano kwa sababu ya kuogopa ujauzito, inamzuia mtu yeyote kufikia mshindo. Kama wote wawili mpo tayari, kufikia mshindo au kutofikia kunategemea maandalizi ya awali ya mapenzi. Mnatakiwa kukubaliana jinsi mtakavyofanya mapenzi i i ili kila mmoja wenu aweze kufurahia na kuridhika. Kwa uhakika, kila mwanamke na mwanaume anazo sehemu maalumu ambazo ukigusa basi ni rahisi sana kufikia mshindo. Upeo wa hali ya kujamiiana pia unaweza kufikia kwa kupiga punyeto. Kwa mfano, mwanaume anaweza kugusa uume wake au mwanamke anaweza kusugua taratibu kinembe mpaka anafikia mshindo. Kupiga punyeto ni njia i iliyo salama ya kumaliza hamu ya kutaka kufanya mapenzi na haina athari mbaya kiafya.
Je, watu wanaoishi na hali ya ualbino wanaweza kuzaa watoto bila matatizo?
Updated at: 2024-05-25 16:24:07 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ulemavu wa watu wanaoishi na ualbino hauingiliani na uwezo wa kuweza kuzaa. Tuelewe kwamba ulemavu huu uko tu kwenye ngozi na siyo kwenye via / mfumo wa uzazi. Kwa maana hiyo basi; Albino anaweza kuzaa watoto wenye afya nzuri. Pia wanaweza kuzaa watoto wenye ngozi ya kawaida (blackii) kama mzazi mwenzie hatakuwa amebeba vinasaba vya ualbino.
Madhara yanayotokea kwa unyanyasaji wa jinsia kwa mtu
Updated at: 2024-05-25 16:24:00 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Unyanyasaji wa ujinsia una matatizo mabaya ya kimwili na yanayochukua muda mrefu kwa mwathiriwa kupona. Unyanyasaji wa jinsia mara nyingi humuumiza mwathiriwa, matendo ya ubakaji, majaribio ya ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia kwa mtoto, na ukeketaji kwa wanawake yanamhusu moja kwa moja mwili wa mwathiriwa. Mwathiriwa anaweza kupata maumivu makali wakati wa kitendo, viungo vyake vya uzazi akiwa mwanamume au mwanamke kuna uwezekano ukapata majeraha wakati wa ubakaji. Zaidi ya hayo mbakaji anaweza kumuumiza mwathiriwa katika sehemu nyingie za mwili. Na jambo baya zaidi ukatili wa kijinsia wakati mwingine unaweza kusababisha ulemavu wa maisha na mara nyingine hata kifo cha mwathiriwa. Ubakaji unaweza kusababisha mimba, na uenezaji wa magonjwa hatari kama Virusi vya Ukimwi. Watoto wanadhuriwa zaidi na vitendo vya ukatili wa ujinsia katika miili yao kwa sababu ukubwa wa viungo vyao vya sehemu za siri ni vidogo kuliko vile vya watu wazima. Athari za kisaikolojia kwa mwathiriwa pia ni hatari sana. Uonevu wa ujinsia kwa mwathirika unaweza kusababisha kuchanganyikiwa na kupata kiwewe na hali ya hatari sana inayoweza kusababisha mtu akapata kichaa katika miezi ya kwanza. Baada ya uonevu wa ujinsia na hata baada ya miaka, mwathiriwa bado atakuwa na kumbukumbu ya maumivu aliyopata na hivyo kukumbuka katika akili yake. Waathiriwa wengi wa ubakaji wana matatizo ya kutokuwa na uhusiano mzuri wa kujamiiana, kwani kila mara atahusisha kujamiiana na alipobakwa. Ndiyo maana waathiriwa wa ubakaji wanahitaji msaada, uelewa na uvumilivu toka kwa wazazi wao, wenzi wao na marafiki.
Updated at: 2024-05-25 16:22:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Magonjwa ya zinaa husababishwa na vijidudu vya magonjwa na huambukizwa kwa kukutana kimwili na mtu mwenye vijidudu hivyo. Katika Tanzania magonjwa haya yameenea sana haswa kwa vijana.. Hivyo kama una wasiwasi wewe au mpenzi uliyekutana naye kimwili kuwa na ugonjwa kama huo, muhimu mwende kupimwa. Magonjwa hayo yasipotibiwa kikamilifu yanaweza kuleta madhara makubwa. Magonjwa ya zinaa mara nyingi yanasababisha ugumba.
Ni katika umri gani vijana wana haki ya kujihusisha na mambo ya kujamiiana?
Updated at: 2024-05-25 16:24:04 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kujamiiana ni uamuzi wa mtu binafsi. Ni uamuzi wako na hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kukuamulia. Lakini unapoamua kujamiiana hakikisha kwamba ni maamuzi uliojulishwa na kwamba unaelewa matokeo ya kujamiiana. Usisahau kuchukua hadhari muhimu. kumbuka kutumia kondomu kujikinga wewe na mwenzi wako kutokana na mimba usizotarajia na magonjwa kama vile Virusi vya UKIMWI. Madhari mwili wako unaendelea kukua, kujamiiana bila ya kondomu ni hatari zaidi kuliko mtu mzima, kwa sababu maambukizo mengine haswa kwa vijana yanaweza kukuletea matatizo kama vile ugumba baadaye katika maisha. Pia jiulize mwenyewe kwa uangalifu kama kweli unataka kujamiiana. Ni muhimu pia kujadiliana na mwenzi wako na kuwa na hakika kama wote wawili mnataka kujamiiana. Usijamiiane kwa sababu tu unafikiria kwamba watu wengine wanajamiiana au unajitosa kwa kuwa unashawishiwa na marafiki au watu wazima.
Je, ni kweli ukinywa maziwa baada ya kuvuta sigara huwezi kudhurika?
Updated at: 2024-05-25 16:24:25 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hapana. Hii si kweli kwa sababu maziwa hayawezi kuondoa uharibifu uliosababishwa na nikotini mdomoni na kwenye moyo, mapafu au kwenye ubongo. Kunywa maziwa baada ya kuvuta sigara kunaweza kusaidia kupunguza mchomo tumboni uliosababishwa na tindikaili.
Je, nikioga mara baada ya kujamiiana, nitaweza kuwatoa wadudu wa ugonjwa wa zinaa na nisiambukizwe?
Updated at: 2024-05-25 16:22:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hapana, huwezi kuwatoa wadudu wa magonjwa ya zinaa kwa njia ya kuoga baada ya kujamiiana. Wadudu hao hawakai sehemu ambazo unaweza ukawaondoa, wanaingia mwilini moja kwa moja na wanakaa kwenye damu.
Mara wakishaingia kwenye damu, inabidi mtaalamu wa kiafya afanye uchunguzi na akutibu kikamilifu.
Mabadiliko gani yanatokea kwenye miili ya wavulana Wakati wa makuzi au wakati wa kubalehe?
Updated at: 2024-05-25 16:24:31 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wakati wa makuzi au kipindi cha kubalehe, wavulana hupitia mabadiliko mbalimbali ya kimwili, kihisia, na kiakili. Mabadiliko haya yanaletwa na ongezeko la homoni, haswa testosterone. Hapa chini ni mabadiliko muhimu yanayotokea kwenye miili ya wavulana wakati huu wa kubalehe:
Ukuaji wa Viungo vya Uzazi: Testicles (korodani) na uume hukua na kuongezeka kwa ukubwa.
Uzalishaji wa Manii: Wavulana huanza kuzalisha manii, na hivyo kuweza kutungisha mimba.
Ukuaji wa Nywele: Nywele huanza kuota katika sehemu mbalimbali za mwili kama usoni, kwapani, sehemu za siri, na kifuani.
Sauti Ya Kunong'ona: Kuna mabadiliko ya sauti ambapo sauti huanza kubadilika na kuwa nzito.
Ukuaji wa Misuli na Mifupa: Kunakuwa na ongezeko la ukuaji wa misuli na mifupa, na mara nyingi wavulana hukua urefu na mapana.
Mwili Kujaa: Wavulana hupata ongezeko la uzito na uwezo wa mwili kufanya kazi za nguvu unaimarika.
Mabadiliko ya Kihisia na Kiakili: Wavulana hupitia mabadiliko ya kihisia, ikiwemo kuanza kuvutiwa kimapenzi na wenzao, pia huweza kupitia mihemko isiyo thabiti.
Chunusi: Kwenye uso na sehemu nyingine, chunusi zinaweza kutokea kutokana na mabadiliko ya homoni.
Ukuaji huu ni sehemu ya kawaida ya kukua na kila mvulana hupitia mabadiliko kwa kasi na namna yake mwenyewe.
Mabadiliko ya kimwili
Utaongezeka urefu na uzito, mikono na mabega yatakuwa na nguvu zaidi, uume na korodani zitaongezeka ukubwa;
Ngozi yako i takuwa na mafuta zaidi na unaweza kuota chunusi usoni;
Kuota nywele sehemu za siri, makwapani na hatimaye usoni na kwenye kifua
Kubadilika sauti na kuwa nzito; na
Uume kusimama / kudinda mara kwa mara na utaanza kuota ndoto nyevu
mabadiliko ya kihisia
Utaanza kuwa na hisia za kutaka kujamii ana, moyo kwenda mbio, na kuwa na msisimko ukimwona msichana unayekuvutia
Mvutio kwa wasichana utaongezeka na utaanza kujali namna unavyotaka kuonekana; na
Kuanza kujiamini, kutotaka kulazimishwa kufanya mbaadhi ya vitu na wewe kutaka kuonekana kama mtu mzima anayeweza kufanya maamuzi pekee yake
Mabadiliko haya ni jambo la kawaida kwa mvulana balehe. Kumbuka, kila mvulana anapitia mabadiliko haya katika nyakati tofauti na ukali / nguvu tofauti.
Updated at: 2024-05-25 16:22:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Sababu mojawapo ni kuwa bangi hulimwa hapa nchini na hivyo hupatikana kwa urahisi. Bangi huuzwa kwa bei nafuu kuliko dawa nyingine za kulevya. Vilevile, vijana wengi huwaona wakubwa wao wakitumia na hii huwafanya waone kuvuta bangi ni kitu halali.
Sababu nyingine ni i i imani potofu kwamba ukivuta bangi unaweza kuwa jasiri wa kufanya kazi na kusoma sana. Lakini yote haya ni uzushi na si kweli kwani watu husahau madhara ya muda mrefu yasababishwayo na uvutaji bangi. Sababu nyingine i inayowafanya Watanzania watumie bangi ni utegemezi wa kisaikolojia, kwani baada ya kuvuta bangi kwa muda, mtu huanza kujisikia hawezi i kuhimili msukumo wa kawaida wa maisha na kuishi bila bangi. Kwa maana hiyo muathirika huendelea na uvutaji bangi.
Je, nini imani ya watu katika kufanya mazoezi ya kujenga ujasiri wakati wa ngono/kufanya mapenzi?
Kuna siri kubwa ya mafanikio katika ngono - ujasiri! Na je, unajua nini watu wanaamini kuhusu kufanya mazoezi ya kujenga ujasiri wakati wa ngono? Twende tukachunguze!
Updated at: 2024-05-25 16:17:49 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo tutazungumzia jambo la muhimu sana, ambalo ni kujenga ujasiri wakati wa ngono. Hivi karibuni, kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu imani ya watu katika kufanya mazoezi ya kujenga ujasiri wakati wa ngono/kufanya mapenzi. Imani hii ina athari kubwa sana kwenye maisha ya ngono na uhusiano wa kimapenzi.
Kujenga ujasiri wakati wa ngono kunaweza kusaidia kuondoa wasiwasi na hofu ambayo inaweza kusababisha utendaji mbaya wa kimapenzi.
Mazoezi ya kujenga ujasiri yanaweza kusaidia kuongeza hamu ya ngono na kufanya uzoefu wa kimapenzi uwe wa kufurahisha zaidi.
Kujenga ujasiri wakati wa ngono kunaweza kusaidia kuondoa hofu ya kushindwa na kujenga imani kwa mwenzi wako.
Mazoezi ya kujenga ujasiri yanaweza kusaidia kujenga uhusiano mzuri wa kimapenzi na kukuza furaha na utulivu kwenye uhusiano wako.
Mazoezi ya kujenga ujasiri yanaweza kusaidia kutumia mbinu za kimapenzi ambazo zinaweza kuwa na manufaa kwa wote wawili.
Kujenga ujasiri wakati wa ngono kunaweza kusaidia kuepuka hali ya kutofurahishwa kimapenzi na hivyo kusaidia kuzuia matatizo ya kimapenzi kwenye uhusiano wako.
Mazoezi ya kujenga ujasiri yanaweza kusaidia kuondoa hisia za aibu na hofu ambayo inaweza kusababisha kushindwa kwenye tendo la ngono.
Kujenga ujasiri wakati wa ngono kunaweza kusaidia kujenga ujasiri kwa ujumla kwenye maisha yako ya kila siku.
Mazoezi ya kujenga ujasiri yanaweza kusaidia kutoa fursa ya kujifunza zaidi kuhusu mwili wako na mwili wa mwenzi wako.
Kujenga ujasiri wakati wa ngono kunaweza kusaidia kujenga uhusiano wa kimapenzi wenye usawa na hivyo kusaidia kuepuka migogoro.
Kwa hiyo, ni muhimu sana kuweka imani katika kujenga ujasiri wakati wa ngono/kufanya mapenzi. Kumbuka, hakuna kitu cha kuogopa kwenye ngono. Kila mtu ana haki ya kufurahia uzoefu wa kimapenzi bila kujali jinsia au mwelekeo wa kimapenzi.
Je, una imani gani katika kufanya mazoezi ya kujenga ujasiri wakati wa ngono/kufanya mapenzi? Je, umewahi kujaribu mazoezi kama haya kabla? Tujulishe kwenye sehemu ya maoni hapa chini.