Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Madhara yanayotokea kwa unyanyasaji wa jinsia kwa mtu

Featured Image

Unyanyasaji wa ujinsia una matatizo mabaya ya kimwili na
yanayochukua muda mrefu kwa mwathiriwa kupona. Unyanyasaji
wa jinsia mara nyingi humuumiza mwathiriwa, matendo ya
ubakaji, majaribio ya ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia kwa mtoto,
na ukeketaji kwa wanawake yanamhusu moja kwa moja mwili
wa mwathiriwa. Mwathiriwa anaweza kupata maumivu makali
wakati wa kitendo, viungo vyake vya uzazi akiwa mwanamume
au mwanamke kuna uwezekano ukapata majeraha wakati wa
ubakaji. Zaidi ya hayo mbakaji anaweza kumuumiza mwathiriwa
katika sehemu nyingie za mwili. Na jambo baya zaidi ukatili
wa kijinsia wakati mwingine unaweza kusababisha ulemavu wa
maisha na mara nyingine hata kifo cha mwathiriwa. Ubakaji
unaweza kusababisha mimba, na uenezaji wa magonjwa hatari
kama Virusi vya Ukimwi.
Watoto wanadhuriwa zaidi na vitendo vya ukatili wa ujinsia
katika miili yao kwa sababu ukubwa wa viungo vyao vya sehemu
za siri ni vidogo kuliko vile vya watu wazima.
Athari za kisaikolojia kwa mwathiriwa pia ni hatari sana. Uonevu
wa ujinsia kwa mwathirika unaweza kusababisha kuchanganyikiwa
na kupata kiwewe na hali ya hatari sana inayoweza kusababisha
mtu akapata kichaa katika miezi ya kwanza. Baada ya uonevu
wa ujinsia na hata baada ya miaka, mwathiriwa bado atakuwa
na kumbukumbu ya maumivu aliyopata na hivyo kukumbuka
katika akili yake. Waathiriwa wengi wa ubakaji wana matatizo
ya kutokuwa na uhusiano mzuri wa kujamiiana, kwani kila mara
atahusisha kujamiiana na alipobakwa. Ndiyo maana waathiriwa
wa ubakaji wanahitaji msaada, uelewa na uvumilivu toka kwa
wazazi wao, wenzi wao na marafiki.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Mtoa huduma wa afya anaweza kukataa kutibu?

Mtoa huduma wa afya anaweza kukataa kutibu?

Siyo haki kwa mtoa huduma wa afya kukataa kumtibu.
Kama kijana, una haki sawa ya kutibiwa ka... Read More

Njia za Kuwa na Uhusiano Wenye Furaha na Msichana

Njia za Kuwa na Uhusiano Wenye Furaha na Msichana

Leo, tutajadili njia za kuunda uhusiano mzuri na wa furaha na msichana. Kuwa na uhusiano mzuri na... Read More

Ualbino unarithiwa vipi?

Ualbino unarithiwa vipi?

Watoto wengi wanaozaliwa na ualbino, wazazi wao wana rangi
ya ngozi, nywele na macho inayafa... Read More

Kwa nini watu wanaamini kuwa Albino hawana maambukizo ya Virusi vya UKIMWI (VVU)?

Kwa nini watu wanaamini kuwa Albino hawana maambukizo ya Virusi vya UKIMWI (VVU)?

Imani hiyo si kweli kabisa. Inawezekana ni kupotoshwa kwa
makusudi wa ukweli kuhusu jambo hi... Read More

Magonjwa ya zinaa yanavyoenea

Magonjwa ya zinaa yanavyoenea

Magonjwa ya zinaa husababishwa na vijidudu vya magonjwa na huambukizwa kwa kukutana kimwili na mt... Read More

Inakuaje mwanaume anaonyesha dalili za magonjwa ya zinaa zaidi kuliko mwanamke?

Inakuaje mwanaume anaonyesha dalili za magonjwa ya zinaa zaidi kuliko mwanamke?

Wanaume mara nyingi huambukizwa sehemu za mrija wa mkojo. Katika sehemu hizi ni rahisi kusikia mw... Read More

Watu wanaoua Albino wanapata faida gani?

Watu wanaoua Albino wanapata faida gani?

Hakuna uchunguzi wa kisayansi ambao umeonyesha faida
yoyote inayopatikana kwa kuua Albino.Read More

Nifanyeje Kukabiliana na Mawazo yasiyofaa kuhusu Ngono?

Nifanyeje Kukabiliana na Mawazo yasiyofaa kuhusu Ngono?

Nifanyeje Kukabiliana na Mawazo yasiyofaa kuhusu Ngono? πŸ€”βœ‹

  1. Jua vipaumbele v... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili kuhusu upendeleo wako wa ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano?

Je, kuna umuhimu wa kujadili kuhusu upendeleo wako wa ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano?

Upendeleo wa ngono na kufanya mapenzi ni jambo muhimu katika mahusiano yetu ya kimapenzi. Inapasw... Read More

Kujamiiana au kufanya mapenzi salama

Kujamiiana au kufanya mapenzi salama

Mapenzi salama ni yale yanayofanyika bila wasiwasi wa kupata mimba zisizotarajiwa, magonjwa ya zinaa... Read More
Je, watu wanaoishi na hali ya ualbino wanaweza kuzaa watoto bila matatizo?

Je, watu wanaoishi na hali ya ualbino wanaweza kuzaa watoto bila matatizo?

Ulemavu wa watu wanaoishi na ualbino hauingiliani na uwezo
wa kuweza kuzaa. Tuelewe kwamba u... Read More

Kwa nini nao watu wanaishi kwenye ndoa wanapata maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Kwa nini nao watu wanaishi kwenye ndoa wanapata maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Kuna sababu kuu mbili i kwa wana ndoa kupata maambukizi i ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
Kw... Read More