Jinsi ya kupika Biskuti Nyembamba (Wafer Bar) Za Chokoleti Na Njugu
Updated at: 2024-05-25 10:23:08 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Wafer Powder/gram wafer (unga wa biskuti uliosagwa wa tayari) - vikombe 2
Maziwa ya Mgando Matamu ya Kopo - 2 vikombe
Nazi iliyokunwa - ½ Kikombe
Chokoleti vipande vipande - 1 Kikombe
Njugu vipande vipande - ½ Kikombe
Siagi - 227 g
MAPISHI
Yeyusha siagi motoni kisha changanya na unga wa wafer acha kidogo motoni Mimina katika treya unayochomea itandaze vizuri, kisha mimina maziwa juu yake pamoja na njugu vipande , nazi iliyokunwa na vipande vya chokoleti. Choma (bake) kwenye oveni kwa moto wa 350ºC kwa dakika 20. Katakata tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Maharage yaliyochemshwa kiasi Spinach zilizokatwa kiasi Vitunguu maji 2 Nyanya 1/2 kopo Swaum/Tangawizi 1 kijiko cha chakula Curry powder 1 kijiko cha chai Olive oil Chumvi
Matayarisho
Kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia tangawizi/swaum kisha nyanya. Pika mpaka nyanya ziive kisha tia curry powder na chumvi. Vipike kiasi kisha tia maharage na maji kidogo kisha funika na uache vichemke. Baada ya muda tia spinach vipike pamoja na maharage mpaka ziive kisha ziipue. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuseviwa.
Jinsi ya kutengeneza biskuti za Matunda Makavu Na Cornflakes
Updated at: 2024-05-25 10:23:08 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - 4 Vikombe
Sukari - 1 Kikombe
Baking powder 1 kijiko cha chai mfuto
Siagi - 454 gms
Mayai - 2
Matunda makavu (tende, zabibu, lozi) - 1 Kikombe
Vanilla - 2 Vijiko vya chai
Cornflakes - ½ kikombe
JINSI YA KUANDAA
Changanya sukari na siagi katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy) Tia yai moja moja huku unachanganya mpaka iwe laini kama sufi. (fluffy) Tia unga, baking powder, matunda makavu, changanya na mwiko. Chota mchanganyiko wa biskuti kwa mkono kama (kiasi cha kijiko kimoja cha supu) fanya duara na uchovye katika cornflakes iliyopondwa kwa mkono (crushed) Zipange katika treya ya kupikia na zipike (bake) katika moto wa 375°F kwa muda wa kiasi dakika 15 huku unazitazama tazama.
Updated at: 2024-05-25 10:37:47 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Tambi (Spaghetti) Nyama ya kusaga Kitunguu maji Nyanya ya kopo Kitunguu swaum Tangawizi Carrot Hoho Lemon Chumvi Curry powder Mafuta Fersh coriander
Matayarisho
Katakata vitunguu maji, carrot, hoho, kisha weka pembeni. Saga vitunguu swaum na tangawizi pamoja kisha weka pembeni. Baada ya hapo injika sufuria jikoni, tia mafuta. Yakisha pata moto tia vitunguu maji kaanga mpaka vigeuke rangi ya kahawia kisha tia kitunguu swaum na tangawizi.baada ya hapo tia nyanya ya kopo na iache ichemke mpaka iive. Baada ya nyanya kuiva tia curry powder na chumvi. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia nyama ya kusaga na uiache ichemke mpaka iive.Baada ya nyama kuiva tia Corrot na hoho na uzipike kwa muda wa dakika 2.Na baada ya hapo mboga itakuwa imeivaa, iipue na katia fresh coriander. Baada ya hapo injika sufuria yenye maji jikoni. Yaache yachemke na kisha tia chumvi na mafuta ya mzaituni (olive oil) na tambi. Acha zichemke mpaka ziive kisha zichuuje maji na chujio na baada ya hapo zitakuwa tayari kuseviwa na nyama.
Updated at: 2024-05-25 10:37:44 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele (rice vikombe 2 na 1/2) Vitunguu (onion 2) Nyanya ya kopo (tin tomato kopo 1) Tangawizi (ginger paste kijiko 1 cha chakula) Kitunguu swaum (garlic paste kijiko 1 cha chakula) Paprika (kijiko 1 na 1/2 cha cha chai) Pilipil (scotch bonnet pepper 1) Curry powder (kijiko 1 cha chai) Maggi cubes 3(unaweza kutumia yenye ladha ya chicken, beef au vegetable. Inategemea unasevu na mchuzi wa aina gani) Chumvi (salt) Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Loweka mchele kwa muda wa dakika 10.Katakata vitunguu kisha weka pembeni, saga pamoja nyanya ya kopo,pilipili, tangawizi na kitunguu swaum kisha weka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu vikiiva tia curry powder, maggi cubes, chumvi na paprika na uchanganye vizuri. Kisha tia mchanganyiko wa nyanya na uupike mpaka uive. Baada ya hapo tia mchele na maji na uupike mpaka ukaribie kuiva kisha ugeuze na umalizie kwa kutia njegere na umalizie kuupika mpaka uive. baada ya hapo utakuwa tayari kuseviwa na mboga yoyote kama kuku, nyama, samaki au assorted meat (Mchanganyiko wa utumbo, makongoro na nyama), Hapo mimi nili-save na mchuzi wa kuku wa kienyeji.
Updated at: 2024-05-25 10:34:40 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Ndizi mbichi - 10
Nyama - kilo 1
Nazi ya kopo - 1
Chumvi - 1 Kijiko cha chakula
Ndimu - 1
Bizari ya manjano - 1 Kijiko cha chai
Pili pili mbichi - 3
Nyanya (tomatoes) - 2
Kitunguu maji - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chakula
Namna ya Kutayarisha Na Kupika
Kata nyama vipande vipande na uisafishe. Chemsha nyama weka chumvi, thomu, tangawizi na ndimu. Iache iwive. Kata kata nyanya na kitunguu, kisha mimina kwenye nyama inayochemka, weka na bizari nusu kijiko. Wacha supu iwive kisha weka pembeni. Ukumbusho: Hakikisha supu inakuwa kiasi na si nyingi. Menya maganda ndizi na uzikate vipande vipande vya kiasi. Zikoshe ndizi na uziweke ndani ya sufuria. Weka maji ndani ya sufuria kisha zichemshe ndizi mpaka ziwe laini kidogo. Zimwage maji ndizi kisha mimina supu na nyama ndani ya ndizi. Mimina nazi pili pili na bizari nusu kijiko ndani ya ndizi na uziweke kwenye jiko zichemke mpaka zibakie na urojo kiasi. Onja chumvi na uongeze kadri utakavyopenda. Weka pembeni zipoe. Pakua ndizi kwenye sahani au bakuli tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:57 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga 300gm
Siagi 225gm
Icing Sugar 60gm
Chokoleti iliyokoza (Dark Chocolate) - 225gm
Vanilla – Vijiko 2 vya chai
Yai -1
Baking Powder ½ kijiko cha chai
Njugu za vipande ½ kikombe cha chai
Njugu zilizosagwa ¼ kikombe cha chai
JINSI YA KUTAYARISHA
Piga sukari na siagi katika mashine ya keki mpaka iwe laini Kisha mimina yai na vanilla koroga vizuri Mwisho mimina unga na baking powder polepole mpaka ichanganyike. Kata kata umbo (shape) lolote unavyopenda (kama nyota, pembetatu,duara, kopa n.k) Panga kwenye treya na choma kwa moto wa 350°C , vikibadilika rangi kidogo tu vitoe Yayusha chokoleti tia kwenye bakuli ndogo. kisha paka kwa kijiko au chovyea upande mmoja mmoja wa biskuti kisha nyunyizia njugu za kipande na njugu ya unga. Panga kwenye sahani tiyari kunywewa na chai ya maziwa au kahawa.
Updated at: 2024-05-25 10:35:26 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIPIMO
Unga wa mchele 500g
Samli 250g
Sukari 250g
Hiliki iliyosagwa 1/2 kijiko cha chai
Arki (rose flavour) 1/2 kijiko cha chai
Baking powder 1 kijiko cha chai
Mayai 4
Maji ya baridi 1/2 kikombe cha chai
NAMNA YA KUTAYRISHA NA KUPIKA
1. Saga sukari iwe laini kiasi, changanya unga wa mchele, baking powder, hiliki na sukari.
2. Pasha moto samli mpaka iwe nyepesi kama maji mimina kwenye ule mchanganyiko wa unga wa mchele, kisha uchanganye pamoja na arki.
3. Ongeza mayai yaliopigwa endelea kuchanganya mpaka unga umeanza kuchanganyika vizuri.
4. Ongeza maji ya baridi sana kama nusu kikombe tu ili uchanganyike vizuri.
5. Kata kwa design unayotaka viwe vinene visiwe kama cookies za kawaida kama ilivyo kwenye picha na ukipenda utaweka kidoto kwa kutumia zaafarani katikati ya kileja kama inavyoonesha hapo juu.
6. Choma kwa moto wa baina ya 300F na 350F kwa dakika 15 mpaka 20 visiwe vyekundu toa na tayari kwa kuliwa
Jinsi ya kupika Mboga Za Majani Makavu (Aina Yoyote)
Updated at: 2024-05-25 10:37:57 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Mboga za majani makavu ¼ kg Mafuta vijiko vikubwa 3-4 Karanga zilizosagwa kikombe ½ Maziwa au tui la nazi kikombe 1 Kitunguu 1 Nyanya 2 Chumvi (kama kuna ulazima) Maji baridi
Hatua
• Loweka mboga za majani makavu na maji kwa dakika 10-15. • Osha , mboga na katakata nyanya na vitunguu. • Kangaa, pukusua na saga karanga zilainike. • Kanga kitunguu, weka nyanya, koroga zilainike. • Ongeza mboga zilizolowekwa na maji yake kwenye rojo, koroga na funikia mpaka maji yakaukie na ive. Punguza moto. • Koroga karanga zilizosagwa na maji, ongeza kwenye mboga ukikoroga kwa dakika 5. • Onja chumvi, pakua kama kitoweo. Uwezekano Weka nyanya kidogo. Tumia tui la nazi au krimu badala ya maziwa. Weka nyama au dagaa au Mayai badala ya Karanga.