Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Featured Image

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.

Share kwa wengine ili nao wazinduke.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kusimamia mzigo wa kazi na majukumu ya familia katika uhusiano

Jinsi ya Kusimamia mzigo wa kazi na majukumu ya familia katika uhusiano

Kusimamia mzigo wa kazi na majukumu ya familia katika uhusiano ni changamoto inayoweza kutokea kwa w... Read More
Njia za Kuimarisha Imani na Uaminifu katika Mahusiano

Njia za Kuimarisha Imani na Uaminifu katika Mahusiano

Mahusiano ni kitu muhimu sana katika maisha yetu. Lakini kuwa na uhusiano mzuri na mwenza wako ku... Read More

Kufurahia Furaha na Mafanikio ya Familia: Sherehe za Kushangaza

Kufurahia Furaha na Mafanikio ya Familia: Sherehe za Kushangaza

  1. Kufurahia Furaha na Mafanikio ya Familia: Sherehe za Kushangaza ni njia bora ya kuadhim... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kujenga katika Mahusiano ya Mbali

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kujenga katika Mahusiano ya Mbali

Mahusiano ya mbali ni changamoto kubwa sana kwa watu wengi, haswa katika ulimwengu wa leo ambapo ... Read More

Kujenga Ushirikiano wenye Kuaminiana na Kuunda Amani na Furaha katika Familia

Kujenga Ushirikiano wenye Kuaminiana na Kuunda Amani na Furaha katika Familia

Kujenga ushirikiano wenye kuaminiana na kuunda amani na furaha katika familia ni muhimu sana kwa ... Read More

Jinsi ya Kuwezesha Ushirikiano wa Kifedha katika Familia: Kukuza Ustawi na Utulivu

Jinsi ya Kuwezesha Ushirikiano wa Kifedha katika Familia: Kukuza Ustawi na Utulivu

Kuwezesha ushirikiano wa kifedha katika familia ni jambo muhimu sana katika kukuza ustawi na utul... Read More

Ujumbe kwa mabinti kuhusu uvaaji

Ujumbe kwa mabinti kuhusu uvaaji

Familia Kwanza: Wasichana wawili waliwasili kwenye Kikao huku wamevaa nguo ambazo zilikuwa zikion... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Familia katika Mahusiano

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Familia katika Mahusiano

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Familia katika Mahusiano

Kuwa na uhusiano mzu... Read More

Kuhamasisha Utunzaji wa Afya ya Kizazi katika Kufanya Mapenzi: Elimu na Ushauri

Kuhamasisha Utunzaji wa Afya ya Kizazi katika Kufanya Mapenzi: Elimu na Ushauri

Habari za leo wapendwa! Siku hii napenda kuzungumzia jambo muhimu kuhusu mapenzi na afya ya kizaz... Read More

Je, watu wanpendelea kutumia njia za asili za kupanga uzazi?

Je, watu wanpendelea kutumia njia za asili za kupanga uzazi?

Karibu kwenye makala hii kuhusu kwa nini watu wanapendelea njia za asili za kupanga uzazi. Kupang... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kujifunza na Kukuza Maarifa katika Familia Yako

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kujifunza na Kukuza Maarifa katika Familia Yako

Kujifunza ni muhimu sana katika maisha yetu. Kupata maarifa mapya ni njia bora ya kujiongezea uju... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha furaha na msisimko katika ndoa

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha furaha na msisimko katika ndoa

Ndoa ni muunganiko wa hisia na mahusiano kati ya wapenzi wawili. Lakini je, unajua jinsi ya kudum... Read More