Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Kwa nini vijana wanakatazwa kujamiiana?

Featured Image

Ujana ni kipindi cha mabadiliko kutoka utotoni kuelekea utu uzima, wakati wa kipindi hiki kijana hupata mabadiliko ya kimwili, kiakili na kimtazamo. Mwili na akili hupevuka. Ni kipindi muhimu cha kuweka msingi wa maisha ya baadaye. Vijana wanakatazwa kujamiiana kwa sababu matatizo mengi yanaweza kutokea kutokana na tendo hilo.

Kwanza kabisa kwa kujihusisha na kitendo cha kujamiiana vijana wanapoteza nguvu na muda ambao wangeweza kutumia kwa shughuli za maendeleo. Kwa mfano, kusoma, kufanya kazi, kushiriki katika shughuli za vikundi katika jamii au kucheza michezo.
Pili, matatizo ya mimba katika umri mdogo ni mengi. Mojawapo ni msichana kufukuzwa shule, au hata jamii kumtenga. Matatizo mengine ni ya kiafya kutokana na mwili wa msichana bado kuwa haujakomaa vyema.
Tatu, vijana wanakuwa bado hawajajiandaa kwa uzazi au kujitegemea. Sababu nyingine ya kuwakataza vijana kujamiiana ni ile ya hatari ya kuambukizana magonjwa ya zinaa ikiwa ni pamoja na Virusi vya UKIMWI. Magonjwa haya ni mabaya sana yanaweza kusababisha maumivu makali, ugumba au hata kifo.
Unapofikiria sababu zote hizo utaona kwamba kujamiiana katika umri mdogo kunaweza kuleta madhara mengi kwa afya yako na malengo yako maishani. Hivyo basi unapokatazwa kujamiiana ni kwa sababu ya matatizo haya. Hata hivyo, kama kwa vyovyote huwezi kuacha kujamiiana, hakikisha kwamba unajikinga wewe na mpenzi wako kwa kutumia kondomu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, kuna umuhimu wa kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujifunza kuhusu anatomi ya mwili wakati wa ngono/kufanya mapenzi? Ndiyo! Kwa... Read More

Kwa nini watu wasio na ualbino wanaogopa kuoa Albino kwa imani kuwa watawazalia watoto Albino?

Kwa nini watu wasio na ualbino wanaogopa kuoa Albino kwa imani kuwa watawazalia watoto Albino?

Ualbino ni hali ya
kurithi, hii inamaanisha
kuwa unapata ualbino
kutoka kwa wazazi... Read More

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wangu kuhusu Kujikinga na Mimba

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wangu kuhusu Kujikinga na Mimba

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wako kuhusu Kujikinga na Mimba

Karibu sana marafiki zangu! L... Read More

Je, watu wanapendelea kutumia vifaa vya burudani kama vile vyombo vya muziki au nuru ya rangi wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kutumia vifaa vya burudani kama vile vyombo vya muziki au nuru ya rangi wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, umewahi kufanya mapenzi ukatumia vifaa vya burudani kama vile vyombo vya muziki au nuru ya ra... Read More

Jinsi ya kutumia kondomu ya kike

Jinsi ya kutumia kondomu ya kike

Kondomu ya kike inafahamika kwa jina la „care“ na “Lady Peteta”. Hapa Tanzania hazipatika... Read More

Sababu za ukeketaji

Sababu za ukeketaji

Hakuna hata mmoja anayejua hasa kwa nini, na lini desturi
imeanza. Jamii inatoa maelezo tofa... Read More

Tofauti ya VVU na UKIMWI

Tofauti ya VVU na UKIMWI

Neno VVU ni i virusi au vijidudu vinavyosababisha ugonjwa wa UKIMWI. Neno hili kwa lugha ya Kii nger... Read More
Je, kuna umuhimu wa kujadili masuala ya usalama na faragha katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujadili masuala ya usalama na faragha katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujadili masuala ya usalama na faragha katika ngono/kufanya mapenzi?

H... Read More

Ninaweza kupata mimba wakati nipo kwenye hedhi?

Ninaweza kupata mimba wakati nipo kwenye hedhi?

Ili mwanamke aweze kushika mimba, i inabidi yai lililopevuka likutane na mbegu za kiume. Yai pevu... Read More

Jinsi ya Kuwa na Muda wa Kutuliza na Msichana

Jinsi ya Kuwa na Muda wa Kutuliza na Msichana

Kila mwanamume anataka kuwa na muda mzuri wa kutuliza na msichana wake. Lakini, wakati mwingine n... Read More

Njia za Kujenga Uhusiano Imara na Msichana

Njia za Kujenga Uhusiano Imara na Msichana

Kujenga uhusiano na msichana ni jambo muhimu katika maisha ya kimapenzi. Uhusiano unapokuwa imara... Read More

Je, mwanamke anaweza kufikia mshindo (kufika kileleni)?

Je, mwanamke anaweza kufikia mshindo (kufika kileleni)?

Ndiyo, mwanamke anaweza kufikia mshindo wakati wa kujamiiana. Dalili ya mwanamke kufikia mshindo ... Read More