Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Jinsi ya kutumia kondomu ya kike

Featured Image

Kondomu ya kike inafahamika kwa jina la „care“ na “Lady Peteta”. Hapa Tanzania hazipatikani sehemu zote na bei yake ni kubwa kidogo.
Kondomu ya kike huingizwa ukeni kabla ya kujamiiana. Kama unatumia kondomu ya kike, chana kwa uangalifu pembezoni mwa pakiti. Kondomu ina pete mbili za plastiki na uwazi upande wa juu. Pete moja imelegea ni ndogo na iko kwa ndani, upande usio na uwazi. Pete ya pili ni kubwa zaidi, imeshikiliwa na iko upande wa tundu. Shikilia kondomu upande uliozibwa na minya pete ya ndani kwa dole gumba na kidole cha pili na cha kati. Mara nyingine inaweza ikakuponyoka, (kuteleza) lakini endelea kujaribu hadi umeiminya vizuri. Tafuta mkao mzuri na ingiza kondomu ya kike. Huku bado unaminya kwa vidole vyako iongoze kondomu ndani ya uke wako. Ukiiachia pete ya ndani itashikilia kondomu ndani ya uke. Sasa ingiza kidole chako kwenye kondomu, sukuma pete mpaka inapogota kwenye mlango wa uzazi.
Kondomu ya kike inaweza kuvaliwa saa kadhaa kabla ya kufanya ngono na pia inaweza kuvuliwa baada ya muda wa kufanyika ngono kupita. Ili kuhakikisha kuwa uume umeingia sehemu husika, msaidie mwenzi wako kuongoza uume kuingia kwenye uke ili usipenye pembeni.
Baada ya kujamiiana, vua kondomu kwa uangalifu. Tupa kondomu iliyotumika kwenye choo cha shimo au uichome. Usitupe kondomu iliyotumika ovyo.
Kama ilivyo kwa kondomu ya kiume, kondomu ya kike itatumika kwa mafanikio zaidi pale ambapo wahusikia wanakuwa na makubaliano na maelewano juu ya matumizi yake.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Msichana ambaye hajawahi kujamiiana anaitwa bikira, je mvulana huitwaje?

Msichana ambaye hajawahi kujamiiana anaitwa bikira, je mvulana huitwaje?

Neno “bikira” ni mtu yeyote ambaye hajawahi kujamii ana maishani mwake, awe mwanamke au mwana... Read More

Madhara ya dawa za kulevya yanadumu kwa muda gani?

Madhara ya dawa za kulevya yanadumu kwa muda gani?

Ni vigumu sana kujibu swali hili kwa sababu muda wa madhara hutegemea sababu mbalimbali kama vile... Read More

Nini kifanyike ili kurekebisha matatizo ya macho ya Albino?

Nini kifanyike ili kurekebisha matatizo ya macho ya Albino?

Kuishi kwa kushindwa kuona sawasawa ni changamoto ya
msingi waliyonayo Albino, inaathiri eli... Read More

Je, kwa nini watu waanzao kutumia dawa za kulevya hupenda kuendelea kuzitumia?

Je, kwa nini watu waanzao kutumia dawa za kulevya hupenda kuendelea kuzitumia?

Hii ndio hasa sababu kwa nini dawa za kulevya ni hatari! Mara unapozizoea unakuwa na ugumu wa kue... Read More

Njia za Kufanya Tarehe ya Kwanza Iwe ya Kusisimua na Msichana

Njia za Kufanya Tarehe ya Kwanza Iwe ya Kusisimua na Msichana

Unapokwenda kwenye tarehe ya kwanza na msichana, ni muhimu sana kufikiria njia za kufanya tarehe ... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili masuala ya afya ya uzazi katika uhusiano?

Je, kuna umuhimu wa kujadili masuala ya afya ya uzazi katika uhusiano?

Je, kuna umuhimu wa kujadili masuala ya afya ya uzazi katika uhusiano? Jibu ni ndio, kwa kweli! M... Read More

Kufikia mshindo au kufika kileleni kwa mwanamke na mwanamme wakati wa kufanya mapenzi

Kufikia mshindo au kufika kileleni kwa mwanamke na mwanamme wakati wa kufanya mapenzi

Je, mwanamke anaweza kufikia mshindo?

Ndiyo, mwanamke anaweza kufikia mshindo wakati wa kuj... Read More
Je, Ni Vipi naweza Kuepuka Shinikizo la Kufanya Ngono Katika Mahusiano?

Je, Ni Vipi naweza Kuepuka Shinikizo la Kufanya Ngono Katika Mahusiano?

Je, Ni Vipi naweza Kuepuka Shinikizo la Kufanya Ngono Katika Mahusiano? 🌼

Habari za leo... Read More

Je, watu wanapendelea kutumia muda mrefu katika kujenga msisimko kabla ya kufanya ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kutumia muda mrefu katika kujenga msisimko kabla ya kufanya ngono/kufanya mapenzi?

Habari yako rafiki yangu? Leo nataka kuzungumzia suala ambalo limekuwa likiwasumbua wengi kwa mud... Read More

Je, kuna vitu fulani ambavyo hupendezwa nayo katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna vitu fulani ambavyo hupendezwa nayo katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna vitu fulani ambavyo hupendezwa nayo katika ngono/kufanya mapenzi? Ndio, kuna mambo mengi... Read More

Je, kuna madhara yoyote pale utakapojaribu kutumia dawa za kulevya mara moja tu au utakapotumia kwa kiasi kidogo sana?

Je, kuna madhara yoyote pale utakapojaribu kutumia dawa za kulevya mara moja tu au utakapotumia kwa kiasi kidogo sana?

Kutumia dawa za kulevya kwa kiasi kidogo kunaweza kusilete madhara i ila mpaka tu pale utakapoyaz... Read More

Jinsi ya Kuanza Mazungumzo na Msichana Unayempenda

Jinsi ya Kuanza Mazungumzo na Msichana Unayempenda

Kuanza mazungumzo na msichana unayempenda inaweza kuwa vigumu, lakini pia inaweza kuwa jambo la k... Read More