Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Ushauri kwa mtu aliyebakwa

Featured Image

Jambo la kwanza jaribu kumwondoa hofu mwathiriwa na
muliwaze maana amepata jambo la kutisha. Na iwapo mtu
amejeruhiwa sana mpeleke katika kituo cha huduma za afya
kilicho karibu mara moja. Vinginevyo ongozana na rafiki
yako kwenda kituo cha Polisi na kutoa taarifa kuhusu jambo
lililotokea. Polisi watampa fomu ambayo ataipeleka kwa mtoa
huduma. Ni muhimu usijioshe kwa maji kabla hujachunguzwa na
mtaalamu wa afya kwani kufanya hivyo kutaondoa ushahidi wa
kubakwa.
Kwa kuwa kupitia utaratibu huu
inakuwa vigumu mwathiriwa
anahitaji msaada wa karibu
na uangalizi. Mzazi au rafiki
anahitajiwa aongozane naye
na kumsaidia, kwa mfano
kuhakikisha kuwa katika kituo
cha polisi msichana ahojiwe na
polisi wa kike.
Mtu aliyebakwa anahitaji
kusaidiwa kihisia ili aweze
kusahau mawazo na jambo
liliomtokea. Kwa mwathirika, ni
muhimu apewe ushauri nasaha
ili aendelee kujihisi kwamba yeye bado yupo kama mtu wa
kawaida. Ni muhimu pia kuzishughulikia habari za mwathiriwa
kwa siri. Usimweleze kila mtu kilichotokea. Waeleze wale tu
ambao unafikiri wanaweza kusaidia kama daktari, mwalimu au
mzazi. Usiulize maswali ya kwa nini maana inaweza ikaonekana
ni kosa la mwathiriwa. Badala yake zungumza na huyo mtu kwa
utaratibu, polepole, peke yake na mpe uangalifu wa kutosha.
Hakikisha kwamba hutoi lawama yoyote kwa mwathiriwa.
Kubakwa kamwe siyo kosa la mwathiriwa.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, Ni Sahihi Kufanya Mapenzi na Mpenzi Wangu wa Shule?

Je, Ni Sahihi Kufanya Mapenzi na Mpenzi Wangu wa Shule?

Je, ni sahihi kufanya mapenzi na mpenzi wangu wa shule? πŸ€”

Habari vyote vijana! Leo tuta... Read More

Je, ni kweli kuwa madhara ya uvutaji moshi wa sigara yako ni kidogo kuliko yale yatokananyo na kuvuta moshi kutoka kwa mvutaji?

Je, ni kweli kuwa madhara ya uvutaji moshi wa sigara yako ni kidogo kuliko yale yatokananyo na kuvuta moshi kutoka kwa mvutaji?

Uvutaji wa aina zote una madhara. Kama utavuta sigara na
kuvuta moshi kwa kutumia mdomo hadi... Read More

Jinsi mimba inavyopatikana

Jinsi mimba inavyopatikana

Ukitaka kuelewa jinsi mimba i inavyopatikana, lazima uelewe mzunguko wa hedhi wa mwanamke. Baada ... Read More

Jinsi ya Kumvutia Msichana kwa Njia ya Kipekee

Jinsi ya Kumvutia Msichana kwa Njia ya Kipekee

Mtoto wa kike anapenda mambo mazuri na ya kipekee, kwa hivyo ikiwa unataka kumvutia msichana kwa ... Read More

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Kubaguliwa Kuhusiana na Ngono?

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Kubaguliwa Kuhusiana na Ngono?

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Kubaguliwa Kuhusiana na Ngono? 🌟

Habari rafiki! Leo t... Read More

Je, kuna wataalamu Tanzania wanaowasaidia watu wenye matatizo ya dawa za kulevya?

Je, kuna wataalamu Tanzania wanaowasaidia watu wenye matatizo ya dawa za kulevya?

Ndiyo. Kuna mashirika yasiyo ya kiserikali (AZISE)
yanayotoa ushauri nasaha kwa watumiaji wa... Read More

Njia za Kujenga Uaminifu na Msichana katika Uhusiano

Njia za Kujenga Uaminifu na Msichana katika Uhusiano

Kama mwanamume, ni muhimu sana kujenga uaminifu na msichana katika uhusiano wako. Njia hii itakus... Read More

Mapenzi salama ni yapi?

Mapenzi salama ni yapi?

Mapenzi salama ni yale yanayofanyika bila wasiwasi wa kupata mimba zisizotarajiwa, magonjwa ya zi... Read More

Ni dawa zipi zilizopigwa marufuku Tanzania na nini hutokea pale mwingizaji anapokamatwa?

Ni dawa zipi zilizopigwa marufuku Tanzania na nini hutokea pale mwingizaji anapokamatwa?

Hapa Tanzania matumizi, umilikaji, usafirishaji na kuhusika katika dawa za kulevya kama vile bang... Read More

Kama watu wanataka kuacha kuvuta sigara au kunywa pombe wafanyeje?

Kama watu wanataka kuacha kuvuta sigara au kunywa pombe wafanyeje?

Kwanza kabisa, watu ni kweli wawe wamedhamiria kuacha. Hii inataka uamuzi wa wazi na nia imara kwa s... Read More
Haki zinazokiukwa iwapo mvulana au msichana wamelazimishwa kuoa au kuolewa

Haki zinazokiukwa iwapo mvulana au msichana wamelazimishwa kuoa au kuolewa

Nani na lini unaoa ni maamuzi yako binafsi wewe mwenyewe,
hata kama rafiki na wazazi wanakus... Read More

Je, kama mwanamke na mwanaume wanapata watoto wa jinsia moja tu, ni kosa la nani?

Je, kama mwanamke na mwanaume wanapata watoto wa jinsia moja tu, ni kosa la nani?

Hakuna mwenye kosa, kwa sababu jinsia ya mtoto i inategemea na bahati na hamna uwezekano wa kupan... Read More