Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Mapenzi salama ni yapi?

Featured Image

Mapenzi salama ni yale yanayofanyika bila wasiwasi wa kupata mimba zisizotarajiwa, magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Mapenzi salama yanaweza kuwa ni vitendo vya kumaliza hamu bila uume kuingizwa ukeni. Ngono ya kuingiza uume ukeni inaweza kuwa ngono salama kama tahadhari husika zinatumika.
Vitendo vya kumaliza hamu bila kujamiiana ni kupiga busu, kukumbatia, kunyonyana ndimi, kushikana mikono na kupiga punyeto. Matendo haya yote ni salama kabisa kuhusiana na mimba zisizotarajiwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Ili kuhakikisha mnafanya mapenzi salama wakati mnahusisha mwingiliano kati ya uume na uke, lazima mchukue tahadhari. Tahadhari mojawapo ni uaminifu katika mapenzi, kwa maana wewe uwe mwaminifu na yeye awe mwaminifu. Lakini pia inabidi muwe na uhakika kwamba wote wawili hamjaambukizwa magonjwa wakati mnapojamiiana kwa mara ya kwanza. Tahadhari nyingine ni kutumia kondomu. Kondomu inazuia mimba pamoja na magonjwa ya zinaa. Kuwa mwaminifu pekee yake haitoshi kama mmoja wenu au wote wawili mliwahi kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi ambao haukuwa salama. Kama kweli mnataka kuwa upande wa uhakika wote ni vyema kwenda kupima Virusi vya Ukimwi kwa hiari.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Vidokezo vya Kuwa na Uwazi katika Uhusiano wako na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Uwazi katika Uhusiano wako na Msichana

Kuwa na uwazi katika uhusiano wako na msichana ni jambo muhimu kwa sababu inajenga uaminifu na up... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Uvumilivu katika Uhusiano wako na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Uvumilivu katika Uhusiano wako na Msichana

Kuwa na uhusiano mzuri na msichana ni jambo ambalo kila mwanaume anataka. Hata hivyo, wakati mwin... Read More

Jinsi ya Kupata Msichana Mzuri na Sifa za Ndani za Thamani

Jinsi ya Kupata Msichana Mzuri na Sifa za Ndani za Thamani

Jinsi ya Kupata Msichana Mzuri na Sifa za Ndani za Thamani

Kupata msichana mzuri na sifa z... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili masuala ya afya ya uzazi katika uhusiano?

Je, kuna umuhimu wa kujadili masuala ya afya ya uzazi katika uhusiano?

Je, kuna umuhimu wa kujadili masuala ya afya ya uzazi katika uhusiano? Jibu ni ndio, kwa kweli! M... Read More

Je, kuna umuhimu wa kuelewa na kuheshimu mipaka ya kisaikolojia katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kuelewa na kuheshimu mipaka ya kisaikolojia katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Kuelewa na kuheshimu mipaka ya kisaikolojia katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi ni muhimu sa... Read More

Je, Ni Sahihi Kufanya Mapenzi na Mpenzi Wangu wa Shule?

Je, Ni Sahihi Kufanya Mapenzi na Mpenzi Wangu wa Shule?

Je, ni sahihi kufanya mapenzi na mpenzi wangu wa shule? πŸ€”

Habari vyote vijana! Leo tuta... Read More

Je, watu wanapenda kujaribu nafasi mpya za ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapenda kujaribu nafasi mpya za ngono/kufanya mapenzi?

  1. Je, watu wanapenda kujaribu nafasi mpya za ngono/kufanya mapenzi?

Hivi karibu... Read More

Inakuwaje, baadhi ya Albino wana macho yanayochezacheza?

Inakuwaje, baadhi ya Albino wana macho yanayochezacheza?

Wapo baadhi ya Albino wenye macho ya kuchezacheza na
ambayo hayawezi kulenga pamoja. Hii ina... Read More

Je, mwanamke ambaye ana hedhi kila mwezi, inawezekana kuwa mgumba?

Je, mwanamke ambaye ana hedhi kila mwezi, inawezekana kuwa mgumba?

Ndiyo, i inawezekana kwamba mwanamke anayepata hedhi yake kila mwezi akawa mgumba. Na vilevile i ... Read More

Je, kuna umuhimu wa kuwa na uelewa wa afya ya uzazi na uzazi katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kuwa na uelewa wa afya ya uzazi na uzazi katika ngono/kufanya mapenzi?

Habari yako rafiki! Leo, ningependa kuzungumza nawe kuhusu umuhimu wa kuwa na uelewa wa afya ya u... Read More

Je, kuna madhara gani ya kunywa pombe kwa vijana hasa kijana Albino?

Je, kuna madhara gani ya kunywa pombe kwa vijana hasa kijana Albino?

Athari za pombe kwa mtu anayeishi na ualbino ni sawa na zile
zinazowapata watu wengine.
Read More

Kunyonyana ulimi kunaweza kuchangia kupata virusi vya UKIMWI?

Kunyonyana ulimi kunaweza kuchangia kupata virusi vya UKIMWI?

Uwezekano wa kuambukizwa virusi vya UKIMWI kwa kunyonyana ndimi ni mdogo sana. Kwa kubadilishana ... Read More