Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Jinsi ya kuongeza mvuto kwa mpenzi wako

Featured Image

Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka. Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?

Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.

Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO

Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO

Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.

Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.

Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI

Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.

Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Ushawishi wa Teknolojia katika Kufanya Mapenzi: Changamoto na Fursa za Zama za Kidijitali

Ushawishi wa Teknolojia katika Kufanya Mapenzi: Changamoto na Fursa za Zama za Kidijitali

  1. Teknolojia imebadilisha jinsi watu wanavyofanya mapenzi. Kwa sasa, kuna zana nyingi za ... Read More

Jinsi ya Kuwa Mfano Bora katika Familia: Kuwa Mtu wa Kuigwa

Jinsi ya Kuwa Mfano Bora katika Familia: Kuwa Mtu wa Kuigwa

Karibu kwenye makala hii ya jinsi ya kuwa mfano bora katika familia yako. Kuwa mtu wa kuigwa ni m... Read More

Kujenga Ushirikiano wenye Nia ya Kujifunza na Kukuza Maarifa katika Familia

Kujenga Ushirikiano wenye Nia ya Kujifunza na Kukuza Maarifa katika Familia

Karibu kwenye makala hii inayoangazia umuhimu wa kujenga ushirikiano wenye nia ya kujifunza na ku... Read More

Njia za Kujenga Ushirikiano wa Karibu na Kuweka Nafasi ya Mazungumzo katika Familia

Njia za Kujenga Ushirikiano wa Karibu na Kuweka Nafasi ya Mazungumzo katika Familia

Katika familia, ushirikiano wa karibu na mazungumzo ni muhimu sana kujenga uhusiano mzuri kati ya... Read More

Jinsi ya Kusimamia tofauti za maoni na migogoro katika uhusiano wa mapenzi

Jinsi ya Kusimamia tofauti za maoni na migogoro katika uhusiano wa mapenzi

Kusimamia tofauti za maoni na migogoro ni sehemu muhimu ya kujenga uhusiano wa mapenzi wenye afya. H... Read More
Jinsi ya Kufanya mipango ya baadaye na ndoto za pamoja na mpenzi wako

Jinsi ya Kufanya mipango ya baadaye na ndoto za pamoja na mpenzi wako

Kufanya mipango ya baadaye na ndoto za pamoja na mpenzi wako ni njia nzuri ya kujenga malengo ya pam... Read More
Jinsi ya Kuunda Mazingira ya Kuwawezesha Watoto kufikia Malengo Yao

Jinsi ya Kuunda Mazingira ya Kuwawezesha Watoto kufikia Malengo Yao

Kuwawezesha watoto kufikia malengo yao ni jambo muhimu sana katika kuhakikisha kuwa wanakuwa na m... Read More

Njia za Kukuza Ushirikiano wa Kijamii na Urafiki katika Familia

Njia za Kukuza Ushirikiano wa Kijamii na Urafiki katika Familia

Njia za Kukuza Ushirikiano wa Kijamii na Urafiki katika Familia

Katika familia, ushirikian... Read More

Njia za Kujenga Mawasiliano Mazuri na Kuwasiliana kwa Heshima katika Familia

Njia za Kujenga Mawasiliano Mazuri na Kuwasiliana kwa Heshima katika Familia

Njia za Kujenga Mawasiliano Mazuri na Kuwasiliana kwa Heshima katika Familia

Familia ni ki... Read More

Njia za Kupata Msichana Anayeshiriki Maslahi yako na Malengo

Njia za Kupata Msichana Anayeshiriki Maslahi yako na Malengo

Kupata msichana ambaye anashiriki malengo yako na ana maslahi sawa nawe ni muhimu sana kwa mafani... Read More

Kupata Urahisishaji na Kusaidia katika Masuala ya Kufanya Mapenzi: Njia za Kuomba Msaada

Kupata Urahisishaji na Kusaidia katika Masuala ya Kufanya Mapenzi: Njia za Kuomba Msaada

Kupata urahisishaji na kusaidia katika masuala ya kufanya mapenzi ni muhimu sana kwa wapenzi wote... Read More

Jinsi ya Kupenda na Kuwaunga Mkono Watoto wa Kambo: Kuleta Umoja katika Familia

Jinsi ya Kupenda na Kuwaunga Mkono Watoto wa Kambo: Kuleta Umoja katika Familia

Kupenda na kuwaunga mkono watoto wa kambo ni muhimu sana kwa ustawi wa familia. Watoto wa kambo w... Read More