Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Featured Image

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.

Share kwa wengine ili nao wazinduke.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kijinsia wenye Kuridhisha katika Mahusiano

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kijinsia wenye Kuridhisha katika Mahusiano

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kijinsia wenye Kuridhisha katika Mahusiano

Katika mahusiano ya ... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maamuzi muhimu ya kifamilia

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maamuzi muhimu ya kifamilia

Kuwajibika na kufanya maamuzi muhimu ya kifamilia ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kudumu. Hapa kuna ... Read More
Jinsi ya kujua kama mwanamke anakupenda kweli kwa dhati

Jinsi ya kujua kama mwanamke anakupenda kweli kwa dhati

Yafuatayo ni maswali ya kujiuliza ili kujua kama mwanamke anakupenda kweli.

Anajitoa kwa ... Read More

Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii katika Familia: Kuweka Muda kwa Ajili ya Marafiki

Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii katika Familia: Kuweka Muda kwa Ajili ya Marafiki

Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii katika Familia: Kuweka Muda kwa Ajili ya Marafiki

Famili... Read More

Je, watu wanapendelea kujaribu mbinu za kuleta msisimko wa kihisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kujaribu mbinu za kuleta msisimko wa kihisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Leo, tutazungumzia kuhusu mbinu za kuleta msisimko wa kihisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi. Ni... Read More

Kusaidiana na Maendeleo ya Kiroho na mke wako

Kusaidiana na Maendeleo ya Kiroho na mke wako

Kusaidiana na maendeleo ya kiroho na mke wako ni muhimu katika kukuza uhusiano wenu na kuimarisha dh... Read More
Siri za kumpata mpenzi bora

Siri za kumpata mpenzi bora

Jinsi ya kupata mpenzi bora
1_ lazima na wewe uwe bora kwanza
Read More

Jinsi ya Kusaidiana katika kujenga na kudumisha afya na ustawi na mpenzi wako

Jinsi ya Kusaidiana katika kujenga na kudumisha afya na ustawi na mpenzi wako

Kusaidiana katika kujenga na kudumisha afya na ustawi na mpenzi wako ni muhimu kwa uhusiano wenye ng... Read More
Jinsi ya Kukuza Ushirikiano wa Kifamilia katika Nyakati za Shida

Jinsi ya Kukuza Ushirikiano wa Kifamilia katika Nyakati za Shida

Kukuza ushirikiano wa kifamilia ni jambo muhimu sana, hasa katika nyakati za shida. Katika ulimwe... Read More

Jinsi ya Kuunganisha Kupitia Mchezo: Furaha na Uhusiano wa Familia

Jinsi ya Kuunganisha Kupitia Mchezo: Furaha na Uhusiano wa Familia

Karibu kwenye makala hii ambayo itakufundisha jinsi ya kuunganisha kwa furaha na uhusiano wa fami... Read More

Siku Maalum za Kufurahia na Kusherehekea na Familia Yako

Siku Maalum za Kufurahia na Kusherehekea na Familia Yako

Kila familia ina siku maalum za kufurahia na kusherehekea pamoja. Siku hizi zinabeba uzito wa kih... Read More

Kujenga Mazoea ya Kujifunza na Kukuza Ukuaji katika Familia Yako

Kujenga Mazoea ya Kujifunza na Kukuza Ukuaji katika Familia Yako

  1. Kujenga mazoea ya kujifunza na kukuza ukuaji katika familia yako ni moja wapo ya mambo ... Read More