Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha mume na mke

Featured Image

Mwanaume mmoja alimuoa mwanamke mrembo. Alikuwa akimpenda sana. Siku moja mwanamke alipatwa na maradhi ya ngozi. Kidogokidogo alianza kupoteza urembo wake.
.
.
.


Mume alipata safari na wakati akirudi alipata ajali iliyomfanya apoteze uwezo wake wa kuona. Hata hivyo, maisha yao ya ndoa yaliendelea kama kawaida. Lakini kadiri siku zilivyosonga mbele ndivyo mke alivyoendelea kupoteza urembo wake. Kwa kuwa mume alikuwa kipofu hakulijua hilo na hivyo hakuna kilichobadilika kwenye upendo wao. Aliendelea kumpenda, na mke alimpenda sana mumewe.
.
.
.


Siku moja mke alifariki dunia. Ilikuwa huzuni kubwa sana kwa mume.
Baada ya kumaliza taratibu zote za maziko, mazishi na kutandua msiba, alipanga kuhama kwenye mji huo na kwenda kuishi kwenye mji mwingine.
.
.
.


Mtu mmoja aliposikia habari hiyo alimwendea na kumuuliza: “Sasa utawezaje kutembea peke yako? Maana siku zote hizi mkeo alikuwa akikusaidia kukuonesha njia.”


Akajibu: “Mimi si kipofu. Nilifanya ionekane hivyo kwa sababu angejua kwamba ninauona mwili wake ulivyobadilika kuwa mbaya angepata maumivu makubwa zaidi kuliko ugonjwa wake wenyewe. Alikuwa mke mwema sana. Nilitaka aendelee kuwa na furaha.”
.
.
.


FUNZO:


Wakati fulani ni vizuri ukajifanya kipofu na kuyapuuza mapungufu ya mwenzako ili kumfanya awe mwenye furaha.


Meno huung’ata ulimi mara nyingi, lakini vinaendelea kuishi pamoja kinywani. Huo ndio moyo wa KUSAMEHEANA. Macho hayaonani, lakini yanatazama na kuona vitu kwa pamoja, hupepesa na kulia pamoja. Huo unaitwa UMOJA.


1. Ukiwa peke yako unaweza kuongea, lakini ukiwa pamoja na mwenzako mnaweza KUZUNGUMZA.


2. Ukiwa peke yako unaweza KUFURAHI, lakini ukiwa na mwenzako unaweza KUFURAHIA.


3. Ukiwa peke yako unaweza KUTABASAMU, lakini ukiwa na mwenzako mnaweza KUCHEKA.


Huo ndio UZURI wa mahusiano yetu kama binadamu. Tunategemeana.


Kiwembe kina ukali lakini hakiwezi kukata mti; shoka lina nguvu na imara lakini haliwezi kukata nywele.


*Kila mtu ni muhimu kulingana na kusudio na lengo la uwepo wake. Usimdharau mtu yeyote kwa hali yoyote, kwa sababu huwezi kuwa yeye.


Mwenyezi Mungu atujaalie nguvu na moyo wa kusamehe, kustahmiliana na kuishi kwa umoja.
.
Tafakari
Mm na ww tunaweza kufanya haya!!!






Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE




Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke





Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.





[products columns="2" ids="30827"]


AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kisasa na jadi na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kisasa na jadi na mpenzi wako

Mapenzi ni kitu kizuri sana na yanapokuwa ya kweli huwa na changamoto zake. Mojawapo ya changamot... Read More

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Msingi imara katika Mahusiano yako

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Msingi imara katika Mahusiano yako

Karibu kwenye makala hii ambayo itakupa mbinu mbalimbali kuhusu jinsi ya kujenga ushirikiano weny... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kiroho katika Familia: Kuunda Nafasi ya Ibada na Uwiano

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kiroho katika Familia: Kuunda Nafasi ya Ibada na Uwiano

Familia ni muhimu sana katika maisha yetu. Ni mahali pa kupata faraja, upendo, na msaada. Kwa hiy... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za tabia na mienendo ya watoto wenu na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za tabia na mienendo ya watoto wenu na mpenzi wako

Kama wazazi na wenzi, tunajua kuwa kuna tofauti katika tabia na mienendo yetu. Lakini pia, inawez... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Furaha na Ustawi wa Kila Mwanafamilia katika Familia Yako

Kuweka Kipaumbele cha Furaha na Ustawi wa Kila Mwanafamilia katika Familia Yako

Kuweka Kipaumbele cha Furaha na Ustawi wa Kila Mwanafamilia katika Familia Yako

Familia ni... Read More

Njia za Kuonyesha Msichana Wako Kuwa Ana thamani Kwako

Njia za Kuonyesha Msichana Wako Kuwa Ana thamani Kwako

Kama mwanaume, kuna mambo mengi ambayo unaweza kufanya ili kuonyesha msichana wako kuwa ana thama... Read More

Jinsi ya Kusimamia tofauti za maoni na migogoro katika uhusiano wa mapenzi

Jinsi ya Kusimamia tofauti za maoni na migogoro katika uhusiano wa mapenzi

Kusimamia tofauti za maoni na migogoro ni sehemu muhimu ya kujenga uhusiano wa mapenzi wenye afya. H... Read More
Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mipango ya kifedha

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mipango ya kifedha

Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mipango ya kifedha ni muhimu katika kudumisha ... Read More
Ujumbe kwa mabinti kuhusu uvaaji

Ujumbe kwa mabinti kuhusu uvaaji

Familia Kwanza: Wasichana wawili waliwasili kwenye Kikao huku wamevaa nguo ambazo zilikuwa zikion... Read More

Kwa Wanaume: Mbinu za Kufanya Kazi vizuri na Kupata Mafanikio

Kwa Wanaume: Mbinu za Kufanya Kazi vizuri na Kupata Mafanikio

Read More
Mahaba kwa wanawake wa siku hizi

Mahaba kwa wanawake wa siku hizi

Wanawake wengi siku hizi hawajui au hawataki kuonesha mahaba
Nimefanya kautafiti kangu kadogo ... Read More

Njia za Kujenga Uaminifu na Msichana katika Uhusiano

Njia za Kujenga Uaminifu na Msichana katika Uhusiano

Kama mwanamume, ni muhimu sana kujenga uaminifu na msichana katika uhusiano wako. Njia hii itakus... Read More