Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Angalia jinsi muda wako unavyopotea

Featured Image

Kila mtu ambaye ni hai amepewa muda Wa masaa 24 kila siku,168 kwa wiki,672 kwa mwezi,8064 kwa miezi 12 au kwa mwaka.

Katika hayo masaa 24 unayoyapata kila siku unayatumiaje katika suala zima la kukufikisha katika ndoto na malengo au mafanikio yako?

Kwa nini kuna matajiri na maskini na wote tunapewa masaa 24???
Tucheki mgawanyo Wa masaa 24 ulivyo….katika masaa 24 unayopewa kwa siku masaa 8 ni ya kazi,masaa 8 ni ya kulala na masaa 8 ni ya kufanya mambo yako mengine.

Tuseme katika Masaa 8 kwa ajili ya mambo yako mengine labda masaa manne yanapotea katika foleni au purukushani za maisha kama kula nk.
Je haya mengine manne yanaenda wapi?Tunayapotezea wapi?
Kwenye mpira?kwenye movie?kwenye TV?kwenye mitandao ya kijamii?kukaa na kuwajadili wengine na mashosti?

Hivi unajua kwa siku una wastani Wa kupoteza masaa manne kwenye masaa yako 24??
Kwa wiki unapoteza masaa 28 hali kadhalika masaa 112 kwa mwezi hupotea.
Kwa mwaka mmoja wenye masaa 8760 una wastani Wa kupoteza masaa 1344 ambayo ni sawa na siku 56 kwa mwaka kwa makadirio ya haraka haraka.

Kwa maana nyingine kwa kutumia hii "concept" kila miezi 12 ya mwaka mzima unapoteza miezi miwili kwa mambo ambayo sio "productive".
Hii ni sawasawa na kupoteza mwaka mmoja ndani ya miaka 6…kwa maana nyingine kwa "the same concept" ya masaa 4 kwa siku kupotea ni kwamba unapoteza mwaka mmoja kwa mambo ambayo hayakusaidii chochote.

Hebu jiulize hapo ulipo una umri gani?umeshapoteza miaka mingapi kwa mambo ambayo sio productive??
Kama wewe ni mfanyakazi au muajiriwa ukifanya kazi kwa muda Wa miaka 40 au kwa muda Wa miaka 40 unapoteza miaka 6.6.

Je hebu jiulize muda wote huo unaoupoteza kwenye mambo ambayo sio "productive" ungekuwa ni muda ulioutumia vizuri kwa mambo ya uzalishaji mfano kuanza kidogo kidogo kujenga biashara yako sasaivi tungekuwa na mamilionea na mabilionea wangapi?
Ili uweze kujenga biashara ambayo ni "strong" inakuhitaji angalau uijenge kwa muda Wa miaka mitano kwa maana nyingine kwa kutumia masaa manne tu kwa siku ndani ya miaka 40 utakuta tayari wewe ni milionea na baada ya kustaafu ajira usingeanza kuangaishana na pensheni (kwanza ni shilingi ngapi) au kuanza kubembeleza kuomba uongezewe mkataba au kwenda kufanya tena part time employment…..kwa concept hiyo ni mamilionea wangapi tumewapoteza??

Ndio maana katika hii dunia yetu tunayoishi matajiri wote ni 3% na 97% ya watu waliobakia wanawafanyia kazi matajiri.
Matajiri waliweza kuiona hii concept kwa jicho la Tatu na wakaanza kuifanyia kazi and the rest is history.
Huwezi kumkuta tajiri anapoteza muda wake kwa mambo ya kizembe yasiyomuingizia chochote ndio maana matajiri wanazidi kuwa matajiri na maskini wanaendelea kuwa maskini.

Lakini bado muda na nafasi unayo sasa ukiamua na ukianza kuutumia muda wako ulio nao kwa ajili ya kuyatengeneza maisha yako.
Watu wengi hawako tayari kuumia na kujifunza biashara na kuielewa ndani ya miaka mitano itakayowapelekea kuwa matajiri na kuweza kuyafikia malengo na ndoto zao lakini wapo tayari kuajiriwa na kufa maskini ndani ya miaka 40.

Muda mzuri ndio sasa Wa kufanya maamuzi sahihi Wa kuyawekeza masaa manne kwenye biashara ili uje upate matokeo chanya.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

FURSA HAIJI MARA MBILI: Jinsi unavyoweza kupata faida au hasara ukitumia Nafasi au fursa uliyonayo

FURSA HAIJI MARA MBILI: Jinsi unavyoweza kupata faida au hasara ukitumia Nafasi au fursa uliyonayo

Kwenye maisha fursa moja tu inatosha kabisa
kubadilisha hali yako ya sasa na kukuweka kwenye... Read More

Ujumbe kwa leo

Ujumbe kwa leo

Kuna baadhi ya LEVEL huwezi kufika…Kuna MAFANIKIO huwezi kuyafikia…Kuna HELA huwezi kuzipata... Read More

Kuwa na kawaida ya kujiwekea Akiba ni njia na Siri ya kuwa tajiri

Kuwa na kawaida ya kujiwekea Akiba ni njia na Siri ya kuwa tajiri

Watu wengi wanajiuliza, “Siri ya utajiri ni nini?” Je ni mbinu gani zin... Read More

Salamu za kuaga mwaka na kukaribisha mwaka mpya

Salamu za kuaga mwaka na kukaribisha mwaka mpya

KWAHERI MWAKA JANA. UMENIFUNZA MENGI.

Mwaka umefika mwisho, zimebaki siku tatu tu
kuin... Read More

Kushindwa au vikwazo sio sababu ya kutofanikiwa

Kushindwa au vikwazo sio sababu ya kutofanikiwa

"Nilibakwa nikiwa na miaka 9 lakini leo mimi ni mmoja wa wanawake wenye ushawishi mkubwa duniani"... Read More

Jinsi Muda Unavyopotea, Jifunze kitu hapa

Jinsi Muda Unavyopotea, Jifunze kitu hapa

Kila mtu ambaye ni hai amepewa muda Wa masaa 24 kila siku,168 kwa wiki,672 kwa mwezi,8064 kwa mie... Read More

Njia 8 za kupata mtaji kwa ajili ya Biashara yako

Njia 8 za kupata mtaji kwa ajili ya Biashara yako

Njia hizo ni kama ifuatayo!!

Jifunze kanuni za fedha
kama ilivyoainishwa hapo chini.
Fedha inataki... Read More

JITAMBUE: Kipi hauna kati ya pesa na muda?

JITAMBUE: Kipi hauna kati ya pesa na muda?

Soma kidogo hapa.. Kuna watu wa aina NNE tunapoongelea pesa na muda.

1. WANA MUD... Read More

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha boss na mwajiri wake

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha boss na mwajiri wake

BARUA YA BOSI ILIBADILI FIKRA ZANGU KUHUSU PESA KATIKA DAKIKA ZA MWISHO ZA MAISHA YANG... Read More