Nikitafuta rafiki kwa nia ya kuoana (mchumba), je ni sifa gani niangalie kwa msichana/mvulana?
Date: April 17, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Kuchagua mchumba ni moja ya maamuzi ambayo kijana anahitaji kuyafanya kwa uangalifu mkubwa sana. Kwa sababu huyo ndiye atakayekuwa mwenzi wake wa maisha. Katika kuchagua mchumba kila mtu ana mawazo yake kuhusiana na kilicho muhimu kuzingatiwa. Mara nyingi mhemuko una nguvu zaidi kuliko uamuzi wa kimantiki
Hata hivyo, vifuatavyo ni kati ya vigezo ambavyo vinaweza kuangaliwa:
β’ Chagua mtu anayekuheshimu wewe na wengine; Chagua mtu unayemwamini;
β’ Chagua mtu ambaye unaweza kuongea, kujadiliana, na kuhojiana naye kwa uwazi bila kugombana;
β’ Chagua mtu mwenye umri unaokaribiana na wa kwako;
β’ Chagua mtu anayependelea vile unavyopendelea;
β’ Chagua mtu ambaye ataelewa matatizo yako na yuko tayari kukusaidia kuyatatua; na
β’ Chagua mtu mwenye afya nzuri.
Hii inamaanisha pia kumpata mtu ambaye kabla ya kuanza kujaamiana naye, atakuwa tayari kwenda kupima kwa hiari kujua hali yake ya VVU na pia kuwa tayari kutumia kinga kwa maana ya kondomu hadi hapo mtakapojua hali zenu.
Wafahamishe wazazi wako mtu uliyemchagua kama mchumba na mtambulishe kwao i ili wamfahamu na yeye awafahamu wazazi wako. Wakati huohuo na wewe jaribu kuwafahamu wazazi wake. Usifanye uchumba wa haraka. Pata muda wa kutosha kumwelewa rafiki yako.
Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.
Related Posts
Yai mmoja hupevuka siku 14 kabla ya hedhi i i inayofuata. Baada ya yai kukomaa ndani ya kokwa la upa...
Read More
Je, Ni Vipi naweza Kuepuka Shinikizo la Kufanya Ngono Katika Mahusiano? πΌ
Habari za leo...
Read More
Je, umewahi kufikiria jinsi watu wanavyoelewa na kuheshimu mchakato wa uponyaji wakati wa ngono a...
Read More
Inawezekana kwa msichana au mwanamke aliyebakwa kupata
mimba. Uwezekano wa kupata mimba ni s...
Read More
Viungo vya uzazi vya ndani vinaonekana katika michoro inayofuata:
Read More
Kwa mwanaume, dalili ya kufikia mshindo ni uume kusimama halafu kumwaga manii . Manii kutotoka wakat...
Read More
Kila siku, tunaishi katika jamii ambayo ina maadili na kanuni za kufuata katika uhusiano wa ngono...
Read More
Ndiyo, watashtakiwa! Wakati mwingine wazazi huwatuma
watoto wao kuchukua au kununua pombe au...
Read More
Kwa nini inapendekezwa Kufanya Ngono na Mtu Mmoja Tu? π
Karibu vijana wenzangu! Leo tut...
Read More
Ndiyo, unaweza kuambukizwa ukitumia nyembe kali au sindano kwa kuchangia pamoja na mtu mwenye vir...
Read More
Jinsi ya Kujilinda na Mimba Bila Kusababisha Madhara ya Kiafya? ππΌ
Karibu kijana! Le...
Read More
Ndiyo, mwanamke anaweza kufikia mshindo wakati wa kujamiiana. Dalili ya mwanamke kufikia mshindo ...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!