Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Mapenzi salama ni yapi?

Featured Image

Mapenzi salama ni yale yanayofanyika bila wasiwasi wa kupata mimba zisizotarajiwa, magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Mapenzi salama yanaweza kuwa ni vitendo vya kumaliza hamu bila uume kuingizwa ukeni. Ngono ya kuingiza uume ukeni inaweza kuwa ngono salama kama tahadhari husika zinatumika.
Vitendo vya kumaliza hamu bila kujamiiana ni kupiga busu, kukumbatia, kunyonyana ndimi, kushikana mikono na kupiga punyeto. Matendo haya yote ni salama kabisa kuhusiana na mimba zisizotarajiwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Ili kuhakikisha mnafanya mapenzi salama wakati mnahusisha mwingiliano kati ya uume na uke, lazima mchukue tahadhari. Tahadhari mojawapo ni uaminifu katika mapenzi, kwa maana wewe uwe mwaminifu na yeye awe mwaminifu. Lakini pia inabidi muwe na uhakika kwamba wote wawili hamjaambukizwa magonjwa wakati mnapojamiiana kwa mara ya kwanza. Tahadhari nyingine ni kutumia kondomu. Kondomu inazuia mimba pamoja na magonjwa ya zinaa. Kuwa mwaminifu pekee yake haitoshi kama mmoja wenu au wote wawili mliwahi kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi ambao haukuwa salama. Kama kweli mnataka kuwa upande wa uhakika wote ni vyema kwenda kupima Virusi vya Ukimwi kwa hiari.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, watu wanaoishi na hali ya ualbino wanaweza kuzaa watoto bila matatizo?

Je, watu wanaoishi na hali ya ualbino wanaweza kuzaa watoto bila matatizo?

Ulemavu wa watu wanaoishi na ualbino hauingiliani na uwezo
wa kuweza kuzaa. Tuelewe kwamba u... Read More

Je, kuna mambo ya haramu katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna mambo ya haramu katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna mambo ya haramu katika ngono/kufanya mapenzi? Hili ni swali ambalo linaweza kuwa na maji... Read More

Niende wapi kupima kama nina Virusi vya UKIMWI?

Niende wapi kupima kama nina Virusi vya UKIMWI?

Vituo vyenye utaalamu na katika hospitali i au Taasisis kama vile Shirika la Amref au CCBRT wana ... Read More

Je, Ni Vipi Kujilinda na Maambukizi ya Kisonono na Kaswende?

Je, Ni Vipi Kujilinda na Maambukizi ya Kisonono na Kaswende?

Je, Ni Vipi Kujilinda na Maambukizi ya Kisonono na Kaswende? 😊

Karibu, vijana wapendwa!... Read More

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Kutotaka Kufanya Ngono?

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Kutotaka Kufanya Ngono?

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Kutotaka Kufanya Ngono? 😊

Leo, ningependa kuzungumza ... Read More

Je, Ni Sahihi Kufanya Ngono na Mpenzi Wangu wa Mbali (Long-Distance)?

Je, Ni Sahihi Kufanya Ngono na Mpenzi Wangu wa Mbali (Long-Distance)?

Je, ni sahihi kufanya ngono na mpenzi wangu wa mbali? Swali hili limekuwa likiwasumbua vijana wen... Read More

Njia za Kuzuia Mimba

Njia za Kuzuia Mimba

Njia za uzazi wa mpango zinatofautiana sana na zinaweza kugawanywa katika makundi mengi:

Vizuizi... Read More

Mwanamume au mvulana anaweza kubakwa?

Mwanamume au mvulana anaweza kubakwa?

Ndiyo, mtu yoyote anayelazimishwa
kujamiina atakuwa
amebakwa, haijalishi kama
mtu ... Read More

Je, kuna umuhimu wa kuelewa na kuheshimu dini na imani za mwenza wako kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kuelewa na kuheshimu dini na imani za mwenza wako kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kuelewa na kuheshimu dini na imani za mwenza wako kuhusu ngono/kufanya mapenz... Read More

Nini matatizo ya macho ya Albino?

Nini matatizo ya macho ya Albino?

Mboni katika macho ya Albino haina pigimenti ya rangi. Kwa
hiyo, ni rahisi macho yao kuathir... Read More

Je, kuna tofauti za kitamaduni katika mtazamo wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti za kitamaduni katika mtazamo wa ngono/kufanya mapenzi?

Habari za leo wapenzi wa Kiswahili! Leo tutajadili suala la tofauti za kitamaduni katika mtazamo ... Read More

Je, ni muhimu kuwa na usawa wa ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano?

Je, ni muhimu kuwa na usawa wa ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano?

Habari za leo wapenzi! Sijui kama umewahi kujiuliza kuhusu umuhimu wa usawa wa ngono/kufanya mape... Read More