Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Jinsi ya kutumia Kondomu

Featured Image

Wakati wa kutumia kondomu ya kiume ni muhimu kufuata hatua zifuatazo. Hakikisha kwamba pakiti inayoihifadhi haijapasuka na kwamba tarehe ya kuisha muda wake haijafika.
Uume ukishadinda, fungua pakiti kwa uangalifu. Minya sehemu ya juu kutoa hewa ndani ya kondomu wakati wa kuvalisha uume, ili kuzuia kupasuka kwa kondomu wakati wa kujamiiana. Visha uume kondomu taratibu mpaka uufunike wote. Ukiwa na uhakika kwamba kondomu imevishwa inavyotakiwa, unaweza kukutana kimwili na mwanamke.
Wakati wa kutoa uume kutoka ukeni, uwe mwangalifu kwamba kondomu bado ipo sehemu inayopaswa kuwa. Baada ya kutoa uume kutoka ukeni, vua kondomu kwa uangalifu uume ukiwa bado umedinda, ili kuepuka shahawa zisimwagikie ukeni. Tupa kondomu iliyotumika kwenye choo cha shimo au uichome. Usitupe kondomu iliyotumika ovyo. Pia usitupe kondomu iliyotumika kwenye vyoo vya kisasa yaani vya kuflashi na maji.
Ukinunua “salama kondomu“ ndani ya pakiti, kuna maelekezo kuhusu matumizi ya kondom. Unapotaka kutumia kondom wakati wa kujamiiana, ni vizuri ukajaribisha kwanza ukiwa peke yako ili kuzoea jinsi ya kuitumia.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kwa nini watu wengine wanaamua kutoa mimba?

Kwa nini watu wengine wanaamua kutoa mimba?

Hapa Tanzania utoaji wa mimba hauruhusiwi kisheria. Hata hivyo watu wengine wanaamua kutoa mimba ... Read More

Kupasuka kwa kondomu

Kupasuka kwa kondomu

Kupasuka kwa kondomu mara nyingi kunasababishwa na kondomu kutowekwa vizuri uumeni. Ni muhimu san... Read More

Wanawake wanaweza kulewa haraka kuliko wanaume?

Wanawake wanaweza kulewa haraka kuliko wanaume?

Wasichana na wanawake wanaweza kulewa kwa ujumla.
Mara nyingi, hulewa pombe haraka kuliko wa... Read More

Je, ngono/kufanya mapenzi ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kimapenzi?

Je, ngono/kufanya mapenzi ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kimapenzi?

Je, ngono/kufanya mapenzi ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kimapenzi?

Kwa wengi, kufanya ma... Read More

Je, uke wa mwanamke unaweza kupanuka kiasi gani?

Je, uke wa mwanamke unaweza kupanuka kiasi gani?

Wakati wa kujifungua, uke wa mwanamke mzima hupanuka kuanzia kipenyo cha sentimeta kumi mpaka kum... Read More

Je, watu wanapendelea kujaribu kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kujaribu kufanya mapenzi?

Habari za leo wapendwa wasomaji! Leo, tunajadili kuhusu je, watu wanapendelea kujaribu kufanya ma... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Tarehe ya Kimapenzi na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Tarehe ya Kimapenzi na Msichana

Kama wewe ni miongoni mwa wanaume wanaotaka kuwa na tarehe ya kimapenzi na msichana, kuna vidokez... Read More

Kuna fikra kuwa Albino ni watu wa kawaida je, kisayansi hii ni kweli?

Kuna fikra kuwa Albino ni watu wa kawaida je, kisayansi hii ni kweli?

Hii ni kweli kabisa. Watu wanaoishi na ualbino ni watu wa
kawaida kama binadamu wengine wote... Read More

Je, mimi ni msichana Albino ninaweza kupata mimba kama nikijamiiana mara moja tu?

Je, mimi ni msichana Albino ninaweza kupata mimba kama nikijamiiana mara moja tu?

Ndiyo msichana anaweza kupata mimba kwa kujamiiana mara
moja tu bila kujali ana rangi gani y... Read More

Je, Ni Vipi naweza Kukabiliana na Hisia za Kutokuwa Tayari kwa Ngono?

Je, Ni Vipi naweza Kukabiliana na Hisia za Kutokuwa Tayari kwa Ngono?

Je, Ni Vipi naweza Kukabiliana na Hisia za Kutokuwa Tayari kwa Ngono? 😊

  1. Kwanz... Read More

Je, serikali imechukua hatua gani kudhibiti hali hii ya mauaji ya Albino? Tutaishi vipi?

Je, serikali imechukua hatua gani kudhibiti hali hii ya mauaji ya Albino? Tutaishi vipi?

Kifungu cha 14 cha Katiba ya Tanzania kinaeleza kwa ufasaha
kuwa: “Kila mtu ana haki ya ku... Read More

Haki zinazokiukwa iwapo mvulana au msichana wamelazimishwa kuoa au kuolewa

Haki zinazokiukwa iwapo mvulana au msichana wamelazimishwa kuoa au kuolewa

Nani na lini unaoa ni maamuzi yako binafsi wewe mwenyewe,
hata kama rafiki na wazazi wanakus... Read More