Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Madhara yanayotokea kwa unyanyasaji wa jinsia kwa mtu

Featured Image

Unyanyasaji wa ujinsia una matatizo mabaya ya kimwili na
yanayochukua muda mrefu kwa mwathiriwa kupona. Unyanyasaji
wa jinsia mara nyingi humuumiza mwathiriwa, matendo ya
ubakaji, majaribio ya ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia kwa mtoto,
na ukeketaji kwa wanawake yanamhusu moja kwa moja mwili
wa mwathiriwa. Mwathiriwa anaweza kupata maumivu makali
wakati wa kitendo, viungo vyake vya uzazi akiwa mwanamume
au mwanamke kuna uwezekano ukapata majeraha wakati wa
ubakaji. Zaidi ya hayo mbakaji anaweza kumuumiza mwathiriwa
katika sehemu nyingie za mwili. Na jambo baya zaidi ukatili
wa kijinsia wakati mwingine unaweza kusababisha ulemavu wa
maisha na mara nyingine hata kifo cha mwathiriwa. Ubakaji
unaweza kusababisha mimba, na uenezaji wa magonjwa hatari
kama Virusi vya Ukimwi.
Watoto wanadhuriwa zaidi na vitendo vya ukatili wa ujinsia
katika miili yao kwa sababu ukubwa wa viungo vyao vya sehemu
za siri ni vidogo kuliko vile vya watu wazima.
Athari za kisaikolojia kwa mwathiriwa pia ni hatari sana. Uonevu
wa ujinsia kwa mwathirika unaweza kusababisha kuchanganyikiwa
na kupata kiwewe na hali ya hatari sana inayoweza kusababisha
mtu akapata kichaa katika miezi ya kwanza. Baada ya uonevu
wa ujinsia na hata baada ya miaka, mwathiriwa bado atakuwa
na kumbukumbu ya maumivu aliyopata na hivyo kukumbuka
katika akili yake. Waathiriwa wengi wa ubakaji wana matatizo
ya kutokuwa na uhusiano mzuri wa kujamiiana, kwani kila mara
atahusisha kujamiiana na alipobakwa. Ndiyo maana waathiriwa
wa ubakaji wanahitaji msaada, uelewa na uvumilivu toka kwa
wazazi wao, wenzi wao na marafiki.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, kuna jukumu la kijamii katika maoni ya watu kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna jukumu la kijamii katika maoni ya watu kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna jukumu la kijamii katika maoni ya watu kuhusu ngono/kufanya mapenzi? Jibu ni ndiyo, kuna... Read More

Sheria zinazohusiana na ndoa za kulazimishwa

Sheria zinazohusiana na ndoa za kulazimishwa

Sheria ya msingi ya ndoa nchini Tanzania ni Sheria ya ndoa ya
Bunge, iliyopitishwa mwaka 197... Read More

Je, ni muhimu kuwa mwaminifu kuhusu upendeleo wako wa ngono/kufanya mapenzi kwa mwenza wako?

Je, ni muhimu kuwa mwaminifu kuhusu upendeleo wako wa ngono/kufanya mapenzi kwa mwenza wako?

Je, ni muhimu kuwa mwaminifu kuhusu upendeleo wako wa ngono/kufanya mapenzi kwa mwenza wako? Jibu... Read More

Je, nini imani ya watu katika kuelewa na kuheshimu mchakato wa uponyaji wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, nini imani ya watu katika kuelewa na kuheshimu mchakato wa uponyaji wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, umewahi kufikiria jinsi watu wanavyoelewa na kuheshimu mchakato wa uponyaji wakati wa ngono a... Read More

Vidokezo vya Kufurahia Safari za Pamoja na Msichana

Vidokezo vya Kufurahia Safari za Pamoja na Msichana

Kila mwanamume anapenda kukutana na msichana ambaye anaweza kuwa rafiki wa karibu na kuwa na uhus... Read More

Kumbadilisha mtu aliyeathirika na dawa za kulevya

Kumbadilisha mtu aliyeathirika na dawa za kulevya

Endapo rafiki au jamaa anaomba msaada wa kuacha kutumia dawa za kulevya unaweza kumsaidia kwa kum... Read More

Kwa nini watu wengine hupenda kujamiiana na watu wa jinsi sawasawa? mapenzi ya jinsia moja

Kwa nini watu wengine hupenda kujamiiana na watu wa jinsi sawasawa? mapenzi ya jinsia moja

Ni vigumu kutoa jibu kamili kwa nini hisia hii i ii inatokea kwa watu wengine, kwa sababu wataala... Read More

Je, wasichana wana viungo gani vya uzazi na kazi zake ni zipi?

Je, wasichana wana viungo gani vya uzazi na kazi zake ni zipi?

Viungo vya uzazi vya ndani vinaonekana katika michoro inayofuata:
Read More
Je, kuna madhara msichana akifanya mapenzi wakati akiwa katika hedhi (siku zake)?

Je, kuna madhara msichana akifanya mapenzi wakati akiwa katika hedhi (siku zake)?

Kufanya mapenzi wakati msichana yuko katika hedhi hakuna madhara yoyote kiafya kwa mwanaume wala ... Read More

Unyanyasaji wa kijinsia

Unyanyasaji wa kijinsia

Kuna aina nyingi za unyanyasaji wa jinsia na unaweza kutokea kwa wote wanaume na wanawake. Kwa kawai... Read More
Je, kuna umuhimu kuweka mazingira ya kimapenzi kabla ya kufanya ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu kuweka mazingira ya kimapenzi kabla ya kufanya ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kuweka mazingira ya kimapenzi kabla ya kufanya ngono au kufanya mapenzi? Ndio... Read More

Je, kuna madhara gani usipooga baada ya kujamiiana?

Je, kuna madhara gani usipooga baada ya kujamiiana?

Hakuna madhara yoyote ya msingi anayopata mtu asipooga baada ya kujamiiana. Isipokuwa kwa ajili y... Read More