Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Mapishi ya Wali Wa Tambi Na Kuku Wa Sosi Ya Mtindi

Featured Image

Vipimo Vya Wali

Mchele - 3 vikombe

Tambi - 2 vikombe

Mafuta - ¼ kikombe

Chumvi

Vipimo Vya Kuku

Kuku kidari (boneless) aliyekatwa katwa vipande - 1 Kilo

Kitunguu maji kilichokatwa katwa - 2

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Paprika - 1 kijiko cha supu

Masala ya kuku (tanduri au yoyote) - 1 kijiko cha supu

Ndimu - 2 vijiko vya supu

Mtindi (yoghurt) au malai (cream) - 1 kikombe

Mafuta - ¼ kikombe

Majani ya kotmiri (coriander) - ½ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali:

Osha Mchele, uroweke.
Tia mafuta katika sufuria, kaanga tambi zilizokatwakatwa hadi zigeuke rangi kuwa nyekundu.
Tia mchele endelea kukaanga kidogo.
Tia maji kiasi cha wali kupikika kama unavyopika pilau. Kiasi cha maji kinategemea aina ya mchele
Funika katika moto mdogo mdogo hadi uive ukiwa tayari.

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku

Katika bakuli, changanya vitu vyote isipokuwa mtindi na kitunguu.
Tia mafuta katika karai, kisha tia kitunguu ukaange muda mdogo tu, usikiache kugeuka rangi.
Tia kuku na masala yake, endelea kukaanga, kisha tia mtindi au malai ufunike apikike na kuiva vizuri.
Nyunyuzia kotmiri iliyokatwakatwa ikiwa tayari kuliwa na wali wa tambi.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Mapishi ya chipsi

Mapishi ya chipsi

Mahitaji

Viazi (potato) 1/2 kilo
Mafuta ya kukaangia (veg oil)
Chumvi

Ma... Read More

Jinsi ya kupika Baklawa Za Pistachio Na Lozi

Jinsi ya kupika Baklawa Za Pistachio Na Lozi

VIAMBAUPISHI

Philo (thin pastry) manda nyembamba - 1 paketi

Siagi - ¼ Kikombe cha ... Read More

Utayarishaji bora wa chakula

Utayarishaji bora wa chakula

· Osha mikono yako kwa sabuni kabla na baada
ya kutayarisha chakula
· Tumia vyombo sa... Read More

Mapishi ya Tambi za sukari

Mapishi ya Tambi za sukari

Mahitaji

Tambi (spaghetti 1/2 ya packet)
Mafuta (vegetable oil)
Sukari (sugar 1... Read More

Mapishi ya mboga mchanganyiko

Mapishi ya mboga mchanganyiko

Mahitaji

Viazi ulaya 4 vya wastani
Hoho jekundu 1/2
Hoho la njano 1/2
Hoho... Read More

Jinsi ya kupika Donati

Jinsi ya kupika Donati

Viamba upishi

Unga
2 Magi (kikombe kibuwa cha chai)

Sukari
1/3 Kikombe ch... Read More

Jinsi ya kutengeneza Keki Ya Mbegu Za Mchicha

Jinsi ya kutengeneza Keki Ya Mbegu Za Mchicha

Viamba upishi

Unga ngano vikombc 3
Unga mbegu za mchicha kikombe 1
Baking powde... Read More

Vitafunio vya Afya kwa Kutosheleza Hamu Zako

Vitafunio vya Afya kwa Kutosheleza Hamu Zako

Vitafunio vya Afya kwa Kutosheleza Hamu Zako 🍇🍎🥕

Hakuna jambo bora zaidi kama kuf... Read More

Jinsi ya kupika Mgagani

Jinsi ya kupika Mgagani

Viamba upishi

Mgagani mkono 1
Mafuta vijiko vikubwa 4
Karanga zilizosagwa kikom... Read More

Mchemsho wa samaki na viazi

Mchemsho wa samaki na viazi

Mahitaji

Samaki mbichi (1)
Viazi mbatata (3)
Nyanya (1)
Kitunguu maji
Read More

Jinsi ya kupika Biskuti Za Tende

Jinsi ya kupika Biskuti Za Tende

Viamba upishi

Unga 4 Vikombe vya chai Sukari ya laini (icing sugar) 1 Kikombe cha chai Ba... Read More
Mapishi ya Sambusa za nyama

Mapishi ya Sambusa za nyama

Mahitaji

Nyama ya kusaga (minced beef 1/4 kilo)
Vitunguu maji vilivyokatwakatwa(dice... Read More