Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.

UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Kuishi na Tofauti za Kijinsia: Kuelewa na Kuheshimu Uwepo wetu Wote

Kuishi na Tofauti za Kijinsia: Kuelewa na Kuheshimu Uwepo wetu Wote

Kuishi na Tofauti za Kijinsia: Kuelewa na Kuheshimu Uwepo wetu Wote

Leo hii, dunia ina ida... Read More

Jinsi ya Kudumisha Umoja na Kuishi kwa Amani katika Familia

Jinsi ya Kudumisha Umoja na Kuishi kwa Amani katika Familia

Jinsi ya Kudumisha Umoja na Kuishi kwa Amani katika Familia

Kuishi katika familia yenye um... Read More

Njia za Kujenga Urafiki Mzuri na Msichana Kabla ya Kuwa na Uhusiano

Njia za Kujenga Urafiki Mzuri na Msichana Kabla ya Kuwa na Uhusiano

Karibu ndugu yangu kwenye makala hii ambao inazungumzia njia mbalimbali ambazo utaweza kutumia ku... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kuheshimu matakwa ya kiroho na imani ya mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kuheshimu matakwa ya kiroho na imani ya mpenzi wako

  1. Tambua Imani Yake Ni muhimu kujua imani ya mpenzi wako ili uelewe matakwa yake ya kiroh... Read More

Kujenga Ushirikiano wa Karibu na Wazazi na Familia katika Mahusiano

Kujenga Ushirikiano wa Karibu na Wazazi na Familia katika Mahusiano

  1. Kuwa wazi na Wazazi na Familia Kujenga ushirikiano wa karibu na wazazi na familia ni mu... Read More

Jinsi ya Kuendeleza Ushirikiano wa Timu katika Mahusiano

Jinsi ya Kuendeleza Ushirikiano wa Timu katika Mahusiano

  1. Weka malengo sawa: Kabla ya kuanza kazi yoyote, ni muhimu kwa kila mtu katika timu kuwa... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya usawa na haki za wafanyakazi katika mahusiano ya ajira

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya usawa na haki za wafanyakazi katika mahusiano ya ajira

Mahusiano ya ajira yanatofautiana na mahusiano mengine ya kimapenzi. Kwa kawaida, katika mahusian... Read More

Jinsi ya Kujenga na kudumisha urafiki na marafiki wa mpenzi wako

Jinsi ya Kujenga na kudumisha urafiki na marafiki wa mpenzi wako

Kujenga na kudumisha urafiki na marafiki wa mpenzi wako ni muhimu kwa ustawi wa uhusiano wenu na kuj... Read More
Jinsi ya Kuvunja Tabia Mbaya na Kujenga Mazingira ya Mabadiliko katika Familia

Jinsi ya Kuvunja Tabia Mbaya na Kujenga Mazingira ya Mabadiliko katika Familia

Kwa kila familia, tabia mbaya zinaweza kuwa tatizo kubwa. Hata hivyo, kutokuwa na mazingira mazur... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kijinsia wenye Kuridhisha katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kijinsia wenye Kuridhisha katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kijinsia wenye Kuridhisha katika Familia

Familia ni chanzo cha ... Read More

Kuvunja Vizuizi vya Aibu katika Kufanya Mapenzi: Njia za Kuweka Urahisi na Utulivu

Kuvunja Vizuizi vya Aibu katika Kufanya Mapenzi: Njia za Kuweka Urahisi na Utulivu

Kuvunja Vizuizi vya Aibu katika Kufanya Mapenzi: Njia za Kuweka Urahisi na Utulivu

Kufanya... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya afya na mazoezi ya mwili

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya afya na mazoezi ya mwili

Habari wapendwa! Leo tutaangazia jinsi ya kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya afya na ma... Read More