SMS ya mapenzi kutakia maisha marefu siku ya kuzaliwa au birthday
Updated at: 2024-05-25 15:26:21 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Happy birthday mpenzi, nakuombea kwa mwenyezi akupe maisha marefu na kukuepusha na maradhi, pongezi kwa wako wazazi kwa kukuzaa mpenzi, nakupenda la azizi.
SMS nzuri ya mapenzi ya kimahaba ya kutuma kwa mpenzi wako umpendaye
Updated at: 2024-05-25 15:36:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu. Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.
Ujumbe wa kimahaba wa kumtumia mpenzi wako aliyeko mbali na wewe kumwambia unavyommisi
Updated at: 2024-05-25 15:27:09 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mawingu yametanda napanda kwenye kitanda, macho nayaangaza, taratibu navuta shuka na kujitanda, mishumaa pembezoni inaniangaza, mziki laini wanibembeleza kitu pekee nilichokikosa ni joto lako na vijimambo vyako kunako kitanda!
SMS nzuri ya kumtumia mpenzi wako aliyekuacha kumuomba akurudie
Updated at: 2024-05-25 15:22:20 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
ni bora mnara ukitikisika kuliko kupata pengo lisilozibika moyoni umeniachia jeraha lisilotibika na ufa usiozibika.rudi mpenzi unautesa mtima wa moyo wangu.
Meseji ya kumwambia mpenzi wako asiwaze hata siku moja kuwa unawea kumuacha
Updated at: 2024-05-25 15:25:03 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Asali wa moyo wangu, fahamu kuwa unaweza kuamini kwamba mwanga wa nyota unaweza kuunguza nyumba, jua linaweza kusimama, lakini usiwaze hata siku moja kuwa naweza kukuacha.
Updated at: 2024-05-25 15:36:30 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Katika maisha nimejifunza mambo mengi ikiwemo,. Kupendwa, kupenda, kusamehe, kuvumilia, lakini nimeshindwa kujifunza kukusahau wewe kwa sababu umekuwa ukinikumbuka sana.. nakutakia ASUBUHI NJEMA