SMS nzuri ya mapenzi ya kimahaba ya kutuma kwa mpenzi wako umpendaye
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu.
Updated at: 2024-05-25 15:37:51 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu. Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.
Updated at: 2024-05-25 15:22:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mapenzi ni matamu napia yana raha, wewe hauni ishi hamu, siku zote wanipa raha, wewe kwangu ni mtu muhimu, unaeng'aa moyoni mwangu kama nyota ya jaha. "NAKUOMBA USINIACHE MPENZI WANGU"
SMS nzuri ya kumsihi mpenzi wako asikuchoke na asichoke kukupenda kwani unampenda sana
Updated at: 2024-05-25 15:22:28 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Thamani ya Mapenzi yako nikubwa kwangu, haifanani nachochote kwenye huu ulimwengu, sina budi kumshukuru mungu, kwa kunijaalia mpenzi mwema unaejali hisia zangu, USICHOKE KUNIPENDA MPENZI
SMS ya kumtumia mpenzi wako kumuahidi kuendelea kumpenda daima
Updated at: 2024-05-25 15:22:36 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Moyo wangu umehifadhi hisia zako, nakuahidi kamwe sintopunguza upendo kwako, tunza sms hii ya ahadi kwenye simu yako, iwe kumbukumbu kila uisomapo! "NAKUPENDA MALAIKA WANGU"
SMS nzuri ya kumtumia umpendaye kumwambia unavyompenda na kumridhia
Updated at: 2024-05-25 15:24:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Siku zote kwangu ni sherehe ni wewe unishereheshaye,ukweli usio na kejeli mapenzi yako yanatii kiu yangu,moyoni mwangu nimeridhia… .nakupenda daima mpenzi!