Madhara ya kubeba nauli kamili tuu. Cheki kilichonipata
Updated at: 2024-05-25 17:49:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kubeba nauli kamili nayo ni shida Yani nimepanda daladala Kondakta mmoja akaingia kwenye Gari amevaa suti za blue za daladala na miwani Kisha akakusanya pesa Gari Zima alafu akakaa siti ya nyuma baade Kondakta mwingine akaanza kukusanya pesa watu wakalalamika na kusema tayari tumelipa na kumuonyesha tuliemlipa Kondakta akacheka na kusema huyo tuliemlipa ni kipofu na alikuwa anaomba msaada..!!
Namna wazazi wanavyoongea na mabinti katika umri tofauti
Updated at: 2024-05-25 17:57:54 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Miaka 13: Usipende wavulana ni wabaya. Miaka 18: Sitaki nikuone na yule mvulana tena! Miaka 23: Lini utatuletea mchumba wako? Miaka 26: Wenzio wanaolewa. Miaka 30: Tumekuambia kwamba acha kuchagua sana wanaume, hutaki kusikia! Miaka 33: Kuna mtu wa Mungu yupo kule anaombea unaweza kupata mchumba Miaka 36: At least pata mtoto mmoja. Miaka 39: We will take care of all the wedding billsβ¦yeyote ni sawa sisi tutagharamia kila kitu mwanetu wee mlete tu . Miaka 45: hivi kweli nani alikuroga.?
Updated at: 2024-05-25 17:17:50 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mzee moja alikuwa kila usiku anapita mbele ya bank anasimama,kisha anapiga honi,akitoka askari mlinzi,anaondoka.Hilo jambo likamkera sana askari mlinzi, askari akawa na mvizia yule mzee wa kichaga ,siku alipokuja tena akamkamata, akamuuliza kwa nini unakuja unapiga honi kisha unakimbia? Mzee akasema: Haki ya mungu babaangu , Nina pesa zangu ktk account hapa bank naogopa usilale usingizi ndo maana kila siku usiku napita kukuangalia kama umelala!! ππππππ
Cheki huyu mwanamke anavyomkomoa mme wake baada ya kumsaliti
Updated at: 2024-05-25 17:16:59 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MKE: Mbona unanukia pafyumu ya kike? MUME: Yaa kuna mwanamke tulikuwa tumeminyana ndani ya daladala MKE: Na lipstiki kwenye shati? MUME: Tulikumbatiana na wageni toka Zambia walitembelea ofisi yetu MKE: Na ile kondom iliyotumika kwenye mfuko wa suruali? MUME: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi MKE: Lazima niulize mie huwa nahakikisha nimeacha kila kitu hukohuko ndio narudi nyumbani MUME: Umesema nini wewe? MKE: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi. ππ
Updated at: 2024-05-25 17:15:38 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna mchepuko nilimtumia nauli jana ili aje,.kwang sasa leo kaniambia eti " nimesahau ile line yenye M-pesa home plz nitumie tena kwa tigo mpenz""!! Me nikajifanya chizi nikatuma Kule kule kwenye voda (aliosema kaacha home) Nikatuma huko message ivi "nikuongezee Sh. Ngapi tena mpenz..!!" Akanjbu "elfu 20,000 tu mpenzi" Mtuhurumie jamani πππ
Updated at: 2024-05-25 17:03:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mama mwenye nyumba anajipodoa anashinda saloon kujipodoa lakini house girl hata mafuta usoni hapaki lakini akipita na khanga yake moja tuu nyumba inatetemekaππππππππππππππ huu mchezo hautaki mekapu
Jamaa aliamua kumtoa demu wake out kwaajili ya chakula cha usiku kufika hotelini wakakaa mezani mhudumu akaja,
Mhudumu: kaka nikuhudumie nini,
Jamaa: afathal NILETEE MENU LISTI
Updated at: 2024-05-25 18:03:52 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa aliamua kumtoa demu wake out kwaajili ya chakula cha usiku kufika hotelini wakakaa mezani mhudumu akaja,
Mhudumu: kaka nikuhudumie nini,
Jamaa: afathal NILETEE MENU LISTI
Mhudumu: dada na wewe?
Demu akajibu kwa pozi tena kwakujishaua, "NA MIMI NILETEE MENU LIST ILA USIWEKE CHUMVI NYINGI"
Chezea mbulula weweβ¦!!!