Updated at: 2024-05-25 17:09:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mtoto wa miaka sita alimuuliza babake: MTOTO: Baa, eti sisi wanadamu tulikuja vipi duniani? BABA: Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa. Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na watoto wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika akamfuta mamake) MTOTO: Mma, eti sisi wanadamu tulikuja vipi duniani? MAMA: Wanasayansi wamesema sisi tulitokana na manyani baadae tukawa binadamu. (Mtoto akarudi kwa baba) MTOTO: Baa mbona mama ansema sisi tulikuwa manyani mwanzo?Au wanidanganya? BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo waoπππΆπΌπΆπΌπΆπΌ