Kwa hiki kilichonikuta sitadanganya tena kuanzia leo
Updated at: 2024-05-25 16:58:54 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Juzi nikitoka church nilipanda kihiace na kulikuwa na mrembo mkali hujawahi kuona,kila kijana alikuwa akimtupia macho,so me nilikuwa na wepesi wa kuongea naye kirahisi coz nilikuwa kando yake,,, Sasa kama unavyojuwa wanaume kwa kujikosha Nikaimigine mtto ananiangalia so nikaamuwa kupiga fake phone "Hello Mr. Supervisor,nitachalewa kidogo coz kuna mahali nitapitia, so nipelekee tu hyo Ferrari yangu nyumbani"
Nikaona mrembo ameniangalia kwa macho ya husda apo nkajua nimeuwa ndege kwa jiwe moja, nkaamua kujikosha mtt wa kiume , "niaje mrembo", akanikazia macho kisha akaniambia, "Shika battery yako uliangusha ukitoa simu"
Icho kicheko watu walicheka hujawahi ona jooo adi ikabidi dereva aegeshe gari watu wacheke kwanza ๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐ Nikaona isiwe tabu nikashukia pale pale๐ถ๐ฟ๐ถ๐ฟ๐ถ๐ฟ
Tujifunze kusema ukweli kwani uongo sio mzuri hata kwa Munguโฆ ๐๐๐๐๐
Kilichotokea baada ya mzungu na mbongo kukaa siti moja, bongo wasanii wengi
Mzungu akamdharau sana Mbongo nakujiona anajua kila kitu duniani!,
Akamwambia Mbongo waulizane maswali na Mbongo akishindwa anatoa sh.500 na endapo yeye atashindwa atatoa 100,000/=.
Mzungu akauliza ni nchi ipi ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya Dunia?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hajui.
Updated at: 2024-05-25 18:06:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mzungu akamdharau sana Mbongo nakujiona anajua kila kitu duniani!,
Akamwambia Mbongo waulizane maswali na Mbongo akishindwa anatoa sh.500 na endapo yeye atashindwa atatoa 100,000/=.
Mzungu akauliza ni nchi ipi ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya Dunia?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hajui.
Na yeye akamuuliza Mzungu ni kitu gani kikienda juu kina miguu minne na kikirudi chini kina miguu mitatu?
Mzungu akafikiria akakosa jibu akatoa 100,000/= kuashiria hajui ila akataka kujua, akauliza ni nini hicho?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hata yeye hajui!.
SHARE na marafiki kama umemkubali Mbongo kwa ujanja. Lakini unafikiri Mbongo huyu kwa akili hizi atakuwa ametokea mkoa gani!?.
Updated at: 2024-05-25 18:10:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kakubaliana vizuri na msichana fulani hivi kuwa aibuke gheto, mchizi kajipanga vizuri kabisaโฆ. mara saa nne hivi mdada kasema hana nauli. Mshkaji kajikunja kamtumia Elfu tano maana mwenye shida alikuwa ni yeyeโฆโฆ Baada ya nusu saa yule dada akamtumia meseji. "Jamani mpenzi, kumbe baba hatoki nilijua atatokaโฆ sorry bae sitaweza kuja kwa leoโฆ sooo sorry!" Mshkaji jiii! hajajibu kituโฆ..
Baada ya muda kidogo meseji ikaingia katika simu ya binti, akajua mchizi kajibu. Mh! kutazama ni meseji kutoka Mpesa.
"CA90F0511 IMETHIBITISHWA Tshs 5000 ILIYOTUMWA KIMAKOSA KATIKA ACCOUNT YAKO IMETOLEWA SALIO LAKO NI Tshs 5"
Halafu ndo ikaingia meseji ya mshkaji. "BASI POA SIKU NYINGINE KAMA VIPI"
#dada wa watu mashavu yakamshukaโฆ hakuamini kilichotokeaโฆ. yaani jamaa keshawapigia Voda na pesa fasta imezuiliwaโฆโฆ
Updated at: 2024-05-25 17:51:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
UTOFAUTI KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME 1. Kwenye mshituko; mwanaume hushituka halafu huangalia nini kimemshitua, mwanamke hushituka halafu huzimia hivyo ataambiwa na mwanaume kilichomshitua๐๐ 2. Kwenye kupenda; mwanaume huanza kutamani alafu hupenda, mwanamke huanza kupenda moja kwa moja bila kumjua vizuri huyo ampendae๐๐๐ 3.Kwenye kusaidia; mwanaume hutoa msaada alafu uhuzunika, mwanamke huuzunika badae ndo anakumbuka km msaada unahitajika๐๐๐ 4.Kwenye maamuzi; mwanaume hufikiri ndipo hutenda, mwanamke hutenda halafu hufikiri๐๐๐ 5.Kwenye kudanganya; Mwanaume hudanganya ili kumlinda mwanamke, mwanamke hudanganya ili kumkomoa mwanaume๐๐๐ 6.Kwenye ugomvi; wanaume hupigana halafu hueshimiana, wanawake hupiga mikelele alafu kila mmoja hurud kwake, kexho tena๐๐๐ 7.Kwenye ndoa; mwanaume hutafuta maixha ndipo huoa, mwanamke huolewa ndipo atafute maisha๐๐๐ 8.Kwenye kukata tamaa; mwanaume hukata tamaa mapema ili jambo lisimsumbue, mwanamke hajui kukata tamaa hadi aumizwe๐๐๐ 9.Kwenye kula;Mwanaume hushiba alafu huanza madoido, mwanamke huanza na madoido alafu badae hujilaumu hakushiba๐๐ 10.Kwenye siri; Mwanaume hutunza siri hasa za aibu, mwanamke humueleza shoga yake badae hugombana nae baada ya kumrudia mwenyewe kwa siku 2 tu๐๐๐ Hizi ni baadhi tu ya sifa tofauti kati ya mwanaume na mwanamkeโฆ.. VIVA GENTLEMEN๐๐ฝ๐
Updated at: 2024-05-25 16:57:53 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ukimchoka mkeo, waweza kumtaftia sababu za kumuacha kama hizi
_ 1. Missed calls 16? Umeua betri la simu yangu. Kwa hiyo hata mimi unaweza kuniuaโฆ It's Over!!! _ 2. Hata hunieshimu. Mi naongea na wewe lakini we upo bize unavuta pumzi? It's over! _ 3. Nimekupigia umepokea simu hapohapo. Huna subira. Itโs over!! _
4. Nilikwambia huwa napenda chakula cha moto lakini hujanipashia ice cream. Hunijali. It's over! _ 5. Nimekupa mayai mawili, moja uchemshe jingine ukaange. We umekaanga ambalo ulitakiwa kuchemsha na umechemsha ulilotakiwa kukaanga. Huniheshimu, Itโs over! _ 6. Nimekuita DARLING na wewe ukaniita HONEY. Yani kwa maana nyingine unamuita mama yangu NYUKI. Huheshimu wazazi wangu, fungasha kilicho chako. its over.
Mume akamwambia mke wake:
"Funga macho yako tufanye maombi"
Akaanza kwa Kimombo:-
"โฆ Lord I pray for Grace, I pray for Mercy, I pray 4 Joy, I pray 4 Love, I pray 4 Hope, I pray 4 GLORY, I pray 4 Faith, I pray 4โฆ."
Updated at: 2023-04-29 22:53:26 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Mume akamwambia mke wake: "Funga macho yako tufanye maombi" Akaanza kwa Kimombo:- "โฆ Lord I pray for Grace, I pray for Mercy, I pray 4 Joy, I pray 4 Love, I pray 4 Hope, I pray 4 GLORY, I pray 4 Faith, I pray 4โฆ."
Mke akadakia, "Unadhani mimi sina ee" akaanza:- I pray 4 Felix, I pray 4 Temu, I pray 4 Rweyemamu, I pray 4 Masawe, I pray 4 Benson, I pray 4 Onyango, I pray 4 Swai, I pray kwa wote niliowasahau!! Chezea mchepukoโฆ!!