Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
"Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana."
Padri, "Endelea…"
Updated at: 2023-04-29 22:53:14 (3 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani peke yake. Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama {confess} "Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana." Padri, "Endelea…"
"Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa kufungwa. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu,nikatoa bastola nikamuua….. Yesu atanisamehe?"
Padri: "Utasamehewa." "Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona kilichotokea akasema anapiga polisi simu. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye pia… Yesu atanisamehe hilo?" Padri: "Utasamehewa."
Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe?" Padri:"Utasamehewa."
"Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua? Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.
Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe na hilo?"
Kimyaa…. "Padri yesu atanisamehe?" kimya….
Jamaa akatazama kwenye confession booth padri hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.
Jamaa, "Sasa baba mbona umekimbia?" Padri kwa taabu akajibu, "Nilitazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu……."
Haya ndiyo madhara ya kutowapeleka watoto kanisani ⛪
Updated at: 2024-05-25 17:08:53 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MTOTO aliibiwa yeboyebo KANISANI akawa analia sana kwa uchungu mpaka MCHUNGAJI akamwambia usilie mwachie MUNGU. MTOTO akajibu Mungu hazimtoshi zile yebo ni ndogo! Usicheke,
Huu ni Mtihani Tuwapeleke Watoto KANISANI Wamjue MUNGU.
Pale umapofanya interview huku ukijua hutapata kazi
Updated at: 2024-05-25 17:16:20 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Pale unaitwa kufanya interview na unajua tuu hutapata kazi tuu….. Interviewer: where were u born? Guy: Tanzania Interviewer: okay which part? Guy: what do u mean which part, the whole body was born in Tanzania.. 😂😂😂 Cpendagi ujinga mim
Updated at: 2024-05-25 17:45:32 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Et jana usiku mwiz kavunja mlango kwangu akaanza kutafuta kitu kila kona ikabid na mie niamke namuuliza unatafuta nini ananijibu hela ndipo nilipoanza na mie kutafuta nae maana hta hela ya kula Jana sikua nayo alichoka zaid nilipomuliza una uhakika uliweka humu?
Updated at: 2024-05-25 17:17:44 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa alikuwa kwenye daladala pembeni kuna dada mrembo kakaa. Kamlia timing kwa muda kisha halafu akamuuliza "Samahani dada unaitwa Google?". Dada: "hapana, kwanini umedhani naitwa hivyo?". Jamaa: "Una kila kitu nnachokitafuta "😅😃😃😃😃😃😃😃😃😃
Updated at: 2024-05-25 17:46:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mtalii: Do you have vegetables here. Mtafsiri: Mnavyo vijimeza hapa. Waiter: Vijimeza vidogo hatuna. Mtafsiri: No sir, they don't have. Mtalii: OK, fine, do you have hot dogs. Mtafsiri: Sawa, je mnao mbwa wa moto. Waiter: Loh! Bwana we, hatupiki mbwa hapa. Mtafsiri: They don't cook here Mtalii: What type of snacks do you have here. Mtafsiri: Aina ngapi ya nyoka mnao hapa, Waiter: We bwana we hapa hatupiki aina yeyote ya nyoka, mwache akale nyumbani kwao. Mtafsiri: They don't cook any type of snacks here, maybe you can go back and eat at home. Mtalii: OK, at least give us a cocktail juice. Mtafsiri: OK, tupatie hata juisi ya mkia wa jogoo. Waiter: Hebu tokeni na bangi zenu hapa, tena sasa hivi kabla sijakasirika. Mtafsiri: Lets get out of here 😝😝😝😂😂😂 Usicheke pekeyako