Updated at: 2024-05-25 17:03:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mama mwenye nyumba anajipodoa anashinda saloon kujipodoa lakini house girl hata mafuta usoni hapaki lakini akipita na khanga yake moja tuu nyumba inatetemekaππππππππππππππ huu mchezo hautaki mekapu
Polisi::: hodi, hodi
Jamaa::: kimya
Polisi::: hodi, hodi
Jamaa::: we nani kwani?
Polisi::: sisi polisi
Jamaa::: mnataka nini?
Updated at: 2024-05-25 18:08:23 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Polisi::: hodi, hodi Jamaa::: kimya Polisi::: hodi, hodi Jamaa::: we nani kwani? Polisi::: sisi polisi Jamaa::: mnataka nini?
Polisi::: kuongea na wewe Jamaa::: kuongea na mimi?! Polisi::: ndio Jamaa::: mko wangapi? Polisi::: tuko watatu Jamaa::: kama mko watatu si muongee wenyeweβ¦!!!
Updated at: 2024-05-25 17:05:33 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Trafik mlevi alisimamisha gari Mama akapaki pembeni akaona trafik anakuja akiwa anayumba! Alipofika akasema, "naomba leseni yako." Mama akasachi mkoba Wake akatoa kioo kidogo cha kujtazama akampatia! Trafik akakiangalia kwa dakika 2 Akasema sasa si ungesema kama wewe ni trafik mwenzangu! Haya nenda Ulevi sio mzuri ππππ
Updated at: 2024-05-25 17:46:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mtalii: Do you have vegetables here. Mtafsiri: Mnavyo vijimeza hapa. Waiter: Vijimeza vidogo hatuna. Mtafsiri: No sir, they don't have. Mtalii: OK, fine, do you have hot dogs. Mtafsiri: Sawa, je mnao mbwa wa moto. Waiter: Loh! Bwana we, hatupiki mbwa hapa. Mtafsiri: They don't cook here Mtalii: What type of snacks do you have here. Mtafsiri: Aina ngapi ya nyoka mnao hapa, Waiter: We bwana we hapa hatupiki aina yeyote ya nyoka, mwache akale nyumbani kwao. Mtafsiri: They don't cook any type of snacks here, maybe you can go back and eat at home. Mtalii: OK, at least give us a cocktail juice. Mtafsiri: OK, tupatie hata juisi ya mkia wa jogoo. Waiter: Hebu tokeni na bangi zenu hapa, tena sasa hivi kabla sijakasirika. Mtafsiri: Lets get out of here ππππππ Usicheke pekeyako
Updated at: 2024-05-25 17:15:58 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Pale unapokuwa umefulia sanaβ¦
Mgeni anakutembelea Maskani kwakoβ¦.Unaamua Kuchukua Ile Sh 600 iliyobaki na kwenda Dukani Kumnunulia Soda Unaondoka na Chupa Mbili Unanunua Fanta Moja kwaajil ya Mgeni na Ile Chupa ya Sprite Unaijaza Maji ili Ukirudi Uweze kumpa Kampani Mgeniβ¦β¦Unafika Seblen Unampa Ile soda ya Fanta Mgeni anakuambia Fanta huwa situmii Nipe hiyo sprite β¦..Bwanaβ¦.Bwana. β¦Bwanaβ¦.Weee ππππππππ
Hii mitoto mingine mijinga, cheki alichokifanya huyu
Updated at: 2024-05-25 17:07:59 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nimeamka asubuhi nikiwa na elfu 1 tu mfukoni, nikamtuma mtoto wa jirani akaninunulie maandazi nipate kunywa chai. Baada ya muda namuona anarudi huku analamba askrimu ya AZAM kama Simba vile. Nikamuuliza maandazi yako wapi? Akanijibu eti wakati anafika yanapouzwa maandazi akagundua kuwa kapoteza hela yangu, hivyo akaanza kurudi, ila bahati nzuri wakati anarudi ili kuja kunitaarifu kuhusu kupotea kwa hela yangu, njiani akaokota elfu 1 ambayo kuna mtu alipoteza ndio akaamua kununua askrimuβ¦.kwa sasa niko polisi na mtoto yuko dispensari na mamakeπππππππ