Updated at: 2024-05-25 17:16:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
1) gari la kuvutwa halina overtake 2) kisigino hakikakai mbele 3) wimbo wa taifa haupgwi disko 4) feni haiwashwi beach 5) mshkaki hauchomwi kwa jiko la ges 6) mganga haagiz tembele 7) hata bibi alikuwa bint 8) mke wa mtu sumu,mume wamtu maziwa 9) kipara bila pesa ni kovu 10) mbwa hanenepi migiuu 11) picha ya rais haina bodyguard 12) mjini shule kijiji tuition 13) saa ya ukutani haivaliwi mkonon 14) heshima pesa shkamoo makelele 15) ulinz pesa bastora mzgo 16) kuku ni kuku jogoo mbwembwe 17) kusoma kuelewa kukesha mbwembwe
Updated at: 2024-05-25 17:04:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
😎 Jamaa kamuaga mkewe anaenda semina Songea kwa wiki nzima kumbe kahamia kwa demu nyumba ya pili toka kwake. Siku ya 1 kalala asubuhi alipoamka kachungulia kwake kukoje,
Si kamuona jamaa yuko nje ya nyumba yake kavaa taulo lake anapiga mswaki. Akapiga kelele, 'We nani?', Jamaa akajibu, 'Mshikaji mambo ya mjini, mume wa huyu demu kasafiri kaenda Songea mi ndo najivinjari hapa'. Mume kajibu kwa uchungu, Shenzi mkubwa, ngoja nirudi toka Songea nakuua.😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆
Updated at: 2024-05-25 17:04:27 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo nimeenda mahakamani, mara judge akasema.. Order! Order… Mimi na kiherehere changu nikasema.. Chapati .. Maziwa na ovacado tatu … Nimewekwa kwa karoom kengine hapa kanagiza.. i think wananiandalia chapati 😀😁😀😁😀😁😀😁😂
Jamaa kaingia Bar; Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,
Updated at: 2023-04-29 22:53:32 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Jamaa kaingia Bar; Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,
Jamaa: Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu. Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi. Jamaa: Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake. Zogo lilianzia hapo…….
Soma huyu mtoto anachosema sasa, Ndoto za watoto bwana! Kazi ipo!
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
Updated at: 2023-04-29 22:53:28 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae. MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani? JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo. MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga. MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi. MWAL: Na wewe Nehemiah ?? Nehemiah : mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiwe……" Akameza mate kisha akaendelea…. "Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali." MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani?? JENNY: Nataka kuwa mke wa Nehemiah .!!
Jambazi mmoja aliingia kanisani na bunduki akapiga risasi juu ya bati akasema "asiyempenda YESU atoke nje" wakatoka wote ispokuwa Mchungaji na Wazee wawili.
Updated at: 2024-05-25 18:07:09 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jambazi mmoja aliingia kanisani na bunduki akapiga risasi juu ya bati akasema "asiyempenda YESU atoke nje" wakatoka wote ispokuwa Mchungaji na Wazee wawili.
Jambazi likamwambia Mchungaji "unaweza kuendelea na ibada, nilikuwa nakuondolea wanafiki", Mchungaji akasema "ungewaacha kwanza nichukue sadaka…!
Updated at: 2024-05-25 18:11:36 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hii ndio Bongo
Ilikuwa Ijumaa mida ya saa 10 jioni, mzee mmoja aliingia na kibinti kizuri kwenye yard ya magari mapya.
MZEE: Chagua gari unalotaka mpenzi….kabinti akazunguka yard yote mwisho akachagua Verrosa metallic .
BINTI: Mi naitaka hii
MZEE: Hakuna tatizo kabisaaa, mtoto mzuri kama wewe lazima upate gari uloichagua mwenyewe. Mzee akatoa kitabu cha cheki na kuandika palepale na kumpa mwenye yard
MUUZAJI: Sasa Mzee kwa kuwa umetoa cheki, gari utakuja chukua Jumatatu tukishahakikisha kuwa Account yako ina pesa benki. Naomba namba yako ya simu Mzee
MZEE: Hakuna tatizo (akampa namba). Haya twende zetu sweetie Jumatatu tunakuja wote kuchukua gari lako…
Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee.
MUUZAJI: We Mzee kavu sana, akaunti yako haina hata senti tano.
MZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana.