2. Unaweza kutwanga kwa kutumia kinu au kuchemsha kidogo na kisha kusaga kwa kutumia mashine. Ukitumia mashine uwe makini usije ukasaga sana ukaharibu.
3. Kaanga karanga kidogo na kisha zisage ziwe unga unga.
4. Chemsha kisamvu chako hadi kiive.
5. Katakata kitunguu, karoti na na nyanya
6. Anza kuunga kisamvu kwa kukaanga vitunguu, weka karoti na kisha nyanya na vikishaiva weka kisamvu na koroga pamoja kisha weka karanga. Acha vichemke kwa muda na unaweza pia weka na nazi tui la kwanza.
7. Baada ya muda mfupi epua na kitakiwa tayari. Waweza kula kwa ugali, wali, chapati, makande n.k
Updated at: 2024-05-25 10:23:02 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Nyama ya kusaga (minced beef 1/4 kilo) Vitunguu maji vilivyokatwakatwa(diced onion 2 vikubwa ) Kitunguu swaum/ tangawizi (garlic and ginger paste 1 kijiko cha chakula) Chumvi (salt) Pilipili iliyokatwakatwa (scotch bonnet 1) Limao (lemon 1/2) Curry powder 1/2 kijiko cha chai Cinnamon powder 1/4 kijiko cha chai Coriander powder 1/4 kijiko cha chai Cumin powder 1/4 kijiko cha chai Unga wa ngano (all purpose flour kidogo) Manda za kufungia (spring roll pastry) Giligilani (fresh coriander kiasi) Mafuta ya kukaangia
Matayarisho
Changanya nyama na limao, chumvi, pilipili,kitunguu swaum, tangawizi na spice zote, kisha pika katika moto wa kawaida mpaka nyama iive na maji yote yakauke. Baada ya hapo kabla hujaipua nyama tia vitunguu na giligilani na uvipike pamoja kwa muda wa dakika 2 na uipue weka pembeni na uache viipoe. Baada ya hapo tia unga kidogo katika bakuli nauchanganye na maji kidogo kupata uji mzito kwa ajili ya kugundishia manda. Baada ya hapo tia nyama katika manda na kisha zifunge kwa kugundishia na unga wa ngano.Ukisha maliza kuzifunga zote zikaange mpaka ziwe za brown na uzitoe. Na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:44 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Pilipili hoho (Red pepper 3) Cougette 1 Kitunguu (onion 1) Uyoga (mashroom 1 kikombe cha chai) Carrot 1 Nyanya (fresh tomato 1) Nyanya ya kopo iliyosagwa (tomato paste 3 vijiko vya chai) Giligilani (fresh coriander) Binzari manjano (Turmaric 1/2 ya kijiko cha chai) Curry powder 1/2 ya kijiko cha chai Chumvi (salt) Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Kata hoho kati na utoe moyo wake kisha ziweke pembeni, Kisha katakata cougette, kitunguu, uyoga, carrot, nyanya katika vipande vidogo vidogo, Weka sufuria jikoni na uanze kupika uyoga kwa muda wa dakika 5, kisha weka curry powder, turmaric na chumvi na kaanga kidogo kisha weka vegetable zilizobakia pamoja na nyanya ya kusaga pamoja na giligilani. Zikaange kwa muda wa dakika 5 kisha zitie kwenye hoho na kisha uzibake kwa muda wa dakika 20 na hapo zitakuwa tayari kuseviwa na wali. Wali: angalia katika recipe zilizopita
Updated at: 2024-05-25 10:34:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Nyama (kata vipande vidogodogo) - ½ kilo
Maharage - 3 vikombe
Mahindi - 2 vikombe
Kitunguu - 1
Nyanya - 2
Kabichi lililokatwa - 2 vikombe
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha chai
Vidonge vya supu - 2
Chumvi - kiasi
Mafuta -1au 2 vijiko vya chakula
Namna Yakutayarisha
Chemsha mahindi mpaka yawive na maji yakauke kiasi. Chemsha maharage pembeni nayo mpaka yawive na maji yakaukie kiasi. Tia mafuta kwenye sufuria anza kukaanga vitunguu , thomu na vidonge vya supu koroga kiasi. Kisha mimina nyama iliyokatwa vipande acha ikaangike kidogo na chumvi. Nyama ikishakaangika tia nyanya funika kwa moto mdogo mpaka nyama iwive. Kisha mimina mahindi na maharage yaliyochemshwa na maji yake kiasi koroga mpaka ichanganyike na mwisho mimina kabichi funikia mpaka kabichi iwive onja chumvi kama imekolea Halafu malizia kukoroga mpaka ichanganyike na ikaukie kisha pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa.