Updated at: 2024-05-25 10:34:45 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Soda ni kiburudisho ambacho si muhimu sana kwa afya.
Aina nyingi za soda zina kafeini ambayo huzuia usharabu (ufyonzwaji) wa madini ya chuma mwilini hasa yatokanayo na vyakula vya mimea Hata hivyo soda zinaweza kutumika kwa kiasi kidogo kama kiburudisho, ila tunapotaka ubora zaidi wa afya zetu inafaa kupunguza matumizi ya soda na badala yake kutumia vinywaji vyenye virutubishi muhimu kama vile maji ya matunda, maziwa, madafu au asusa kama vile matunda, karanga na aina mbalimbali za mboga mfano karoti.
Hii inasaidia pia kutumia fedha kidogo tuliyo nayo kwa vyakula muhimu, hasa ukizingatia badala ya soda moja unaweza kupata mayai matatu au nusu lita hadi lita moja ya maziwa.
Updated at: 2024-05-25 10:22:57 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kidali cha kuku 1 (chicken breast) Kitunguu maji 1/2 (onion) Kitunguu swaum/tangawizi (garlic and ginger paste) 1 kijiko cha chai Limao ( lemon)1/4 kijiko cha chai Curry powder 1/4 kijiko cha chai Pilipili ya unga kidogo (Chilli powder) Coriander powder 1/4 kijiko cha chai Soy sauce 1kijiko cha chai Mafuta 2 vijiko vya chai. Chumvi kiasi (salt) Vijiti vya mishkaki
Matayarisho
Osha kidali kisha kikaushe maji na kitchen towel na ukate vipande(cubes) vidogodogo na uweke pembeni. Baada ya hapo changanya vitu vyote (kasoro vijiti )na utie vimaji kidogo kisha visage katika breda kupata paste nzito. Baada ya hapo changanya hiyo paste na kuku na uache zimarinate kwa muda wa saa moja. Baada ya hapo zitunge kuku katika vijiti vya kuchomea na uzichome katika oven mpaka ziive (inaweza kuchukua kama dakika 10). Baada ya hapo chicken satay yako itakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:44 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Viazi (potato) 1/2 kilo Mafuta ya kukaangia (veg oil) Chumvi
Matayarisho
Menya viazi kisha vioshe na vikaushe maji yote kwa kutumia kitchen towel.Baada ya hapo katakata katika shape ya chips uzipendazo either nyembamba au nene kisha zikaushe tena maji na uzitie chumvi. Baada ya kuzitia chumvi tu zitie kwenye mafuta ya kukaangia straightaway (hakikisha mafuta yasiwe ya moto sana kwani utazibabua) Zipike upande mmoja ukiiva geuza upande wa pili. Baada ya hapo endelea kuzipika uku ukiwa unazigeuzageuza mpaka kwa nje ziwe light brown na crisps.Baada ya hapo zitoe na uziweke kwenye kitchen towel ili zichuje mafuta na zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:07 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga 6 Vikombe
Sukari ya kusaga 2 vikombe
Siagi 500 gm
Baking powder 1 Kijiko cha chai
Kastadi ½kikombe
MAPISHI
Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy). Mimina mchanganyiko uliopiga kwa mashine kwenye bakuli. Tia unga na baking powder na Kastadi. Kata usanifu (design) unaopenda halafu panga kwenye sahani ya kupikia (baking tray). Pika (bake) katika oven moto wa 350° F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kabichi 1/2 kilo Nyanya ya kopo 1/2 Kitunguu 1 Curry powder 1/2 kijiko cha chai Chumvi Olive oil
Matayarisho
Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu. Baada yahapo tia katika sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na upunguze moto. Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.
Menya viazi na kisha vikate katika vipande. Tia mafuta kwenye chuma cha kukaangia, yakisha pata moto tia viazi nauviache vikaangike mpaka upande mmoja uwe wa brown na kisha geuza upande wa pili na upike mpaka uwe wa brown. Vikisha iva ipua na uweke kwenye kitchen towel ili vikauke mafuta. Kachumbali: Katakata vitunguu katika bakuli na kisha tia chumvi kwa ajili ya kuondoa ukali wa vitunguu. Baada ya hapo vioshe mpaka chumvi yote iishe. osha nyanya, Pilipili tango na kisha katakata slice nyembamba na uchanganye na vitunguu. Baada ya hapo tia chumvi, kamulia limao na uchanganye zote pamoja .Baada ya hapo viazi na kachumbali vitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Filigisi (chicken gizzard) 1/2 kilo Carrot iliyokwanguliwa 1 Nyanya 1/2 kopo Vitunguu maji 1 kikubwa Tangawizi/swaum 1 kijiko cha chai Hoho 1 iliyokatwakatwa Limao 1/2 Chumvi Curry powder 1/2 kijiko cha chai Turmaric 1/2 kijiko cha chai Chilli powder 1/4 kijiko cha chai Mafuta Chopped coriander
Matayarisho
Safisha filigisi kisha zikate vipande vidogo vidogo.Zichemshe pamoja na chumvi, limao na nusu ya tangawizi na swaum mpaka ziive (hakikisha unabakiza supu kidogo). Baada ya hapo kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia tangawizi na swaum iliyobakia na kaanga kidogo kisha tia nyanya. Zipike mpaka ziive kisha tia spice zote pamoja na chilli. Zipike kidogo kisha tia filigisi (bila supu kwanza) Zichanganye vizuri na uzipike kidogo. Baada ya hapo tia carrot na hoho na supu iliyobakia. Vipike pamoja mpaka viive na supu ibakie kidogo sana. Malizia kwa kutia coriander na uipue na hapo firigisi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:02 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Nyama ya kusaga (minced beef 1/4 kilo) Vitunguu maji vilivyokatwakatwa(diced onion 2 vikubwa ) Kitunguu swaum/ tangawizi (garlic and ginger paste 1 kijiko cha chakula) Chumvi (salt) Pilipili iliyokatwakatwa (scotch bonnet 1) Limao (lemon 1/2) Curry powder 1/2 kijiko cha chai Cinnamon powder 1/4 kijiko cha chai Coriander powder 1/4 kijiko cha chai Cumin powder 1/4 kijiko cha chai Unga wa ngano (all purpose flour kidogo) Manda za kufungia (spring roll pastry) Giligilani (fresh coriander kiasi) Mafuta ya kukaangia
Matayarisho
Changanya nyama na limao, chumvi, pilipili,kitunguu swaum, tangawizi na spice zote, kisha pika katika moto wa kawaida mpaka nyama iive na maji yote yakauke. Baada ya hapo kabla hujaipua nyama tia vitunguu na giligilani na uvipike pamoja kwa muda wa dakika 2 na uipue weka pembeni na uache viipoe. Baada ya hapo tia unga kidogo katika bakuli nauchanganye na maji kidogo kupata uji mzito kwa ajili ya kugundishia manda. Baada ya hapo tia nyama katika manda na kisha zifunge kwa kugundishia na unga wa ngano.Ukisha maliza kuzifunga zote zikaange mpaka ziwe za brown na uzitoe. Na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:22:57 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ulezi (millet flour vijiko 3 vya chakula) Maziwa fresh (milk 1/2 kikombe) Sukari (sugar 1/4 ya kikombe cha chai) Siagi (butter kijiko 1 cha chakula) Maji (vikombe 4 vya chai) (serving ya watu wawili)
Matayarisho
Chemsha maji ya uji, Kisha koroga unga na maji ya baridi kiasi na uchanganye kwenye maji ya moto yanayochemka. Endelea kukoroga mpaka uchemke ili kuhakikisha uji haupatwi na madonge. Ukishachemka tia, maziwa, sukari na butter. Kisha acha uchemke kwa muda wa dakika 10 na hapo uji utakuwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Mayai 5
Sukari 450gm (1 lb)
Unga wa Ngano 1 kg
Siagi 450gm (1 lb)
Baking powder ½ Kijiko cha chai
Unga wa Custard Vijiko 2 vya chakula
Karanga za kusaga 250gm
Jam ½ kikombe
MAANDALIZI
Chukua bakuli la kiasi, weka sukari na siagi. Changanya sukari na siagi kwa kutumia mashine ya kukorogea keki (cakemixer), mpaka sukari ichanganyike na siagi. Vunja yai moja moja na weka kiini chake kwenye mchanganyiko wa sukari na siagi, endelea kuchanganya mpaka ichanganyike vizuri. Hifadhi ute wa mayai ndani ya kibakuli. Mimina unga wa ngano ndani ya mchanganyiko wako huku ukichanganya Changanya unga wa custard na baking powder. Tengeneza viduara vidogo vidogo. Vichovye viduara ndani ya ute wa yai kisha zimwagie unga wa karanga na kuzipanga kwenye tray ya kuchomea. Weka dole gumba kati kati ya kila kiduara na uweke jam. Washa jiko (oven) 350F na uchome vileja vyako kwa dakika 20. Toa vileja vyako vipoe na uviweke ndani ya sahani tayari kwa kuliwa.